Thursday, February 19, 2009

MAVAZI YA WANAFUNZI WA VYUO!!

Nadhani wadau mlifuatilia bunge la Dodoma,

Kati ya maswali yaliyoulizwa na wabunge mojawapo ilikuwa ni mavazi ya watoto wa kike na kiume wa vyuo vya Elimu ya ju,hasa hasa walisisitiza mavazi ya watoto wa kike kuwa si ya tamaduni zetu na yamejawa vishawishi vitupu.

Naibu waziri wa Elimu mama Kabaka alijaribu kuwatetea watoto wa kike na akasisitiza hakuna aliyewahi kufeli kisa mavazi yao.....Mimi bado halijanikaa kichwani nikichukulia mfano wa vyuo vya Dar es Salaam ka mfano.Hivi ni kweli ni kitu ambacho cha kawaida kwa mtu kuvaa mavazi ambayo si muda wake au ambayo hayafai wakati wa lecture au shughuli nyingine za chuo!!

Ukirudi katika mzingira ya kawaida tunayotoka katika familia zetu za kiTZ watoto wa kike na wa kiume huvaa kwa heshima kabisa,ila tatizo hutokea pale wanapokanyaga vyuoni na ndipo vituko huanza ili waende na wakati....mimi nahisi ni balaa na kupoteza utamaduni wetu na pia kujenga picha mbaya kwa jamii!!

Mavazi mazuri kama sketi na magauni ya heshima yamekwenda wapi wadada,au ndiyo sare yenu ya vinguo vya kubana na kuvaa nusu uchi, si usomi wal si kwenda na wakati nahisi ni ulimbukeni na kukosa maadili..tabia hutabiriwa kupitia mavazi pia...hii ndio hufanya hata wazinzi wa mitaani kuhisi watoto wa kike wazuri wapo vyuoni, kumbe ni mavazi mabaya huvutia ngono na uzungu tunaouiga hauna faida!!
Chukueni hatua na badilikeni jamani,hii hufanya nyie kuuza utu wenu ili mpate vitu vya thamani na viwalo vya thamani ili mu sustain kwenye competition zenu na fashion shows zenu za vyuoni!!

Monday, February 16, 2009

SCHOLARSHIP NYINGINE WADAU!!

Full-Time MBA in International Business
The School and company sponsors fund scholarships, awarded as a full or partial exemption from MBA tuition fee.

Scholarships are awarded based on merit and on specific requirements indicated by the School or company sponsors. For specific requirements, download specific scholarship information.
Evaluation criteria


Among evaluation criteria preference is given to:
Significant professional experience
proficiency in Foreign languages
Demonstrated managerial skills
TO be considered for scholarships, candidates must:

Complete and send the on-line application or the PDF application form to the MBA in International Business Meet the requirements stated in the scholarship description
Send all relevant documentation indicated in the competition for scholarship Admission to the MBA program is independent from the scholarship process.
When outcomes for MBA admissions are announced, candidates will be informed if they receive a scholarship and the amount.

Deadline:EU Citizens: 20 August, 2009
Non EU: 31 July, 2009
SOURCE: http://www.mib.edu/cms/data/pages/000039.aspx
MAKULILO Jr,www.makulilo.blogspot.com

MASOMO YAMENOGA,WENGINE WAKO LIKIZO,WENGINE HAWAJUI MUSTAKABALI WAO!!

SAlam wadau,
Ninatumaini mu wazima na munaendelea vizuri na shughuli za kila siku,samahani sana kwa kuwa kimya ni kwamba shule ya UDSM imenoga,wametupokea kwa fujo sana ikiwepo matest,maassignment na mavurugu yote.
ila hatuna wasi kwani twamshukuru mungu kwa kurudi chuoni ili tuendelee kulisukumiza gurudumu la maendeleo liende mbele............

Wenzetu wa IFM wako likizo,twawatakia likizo njema marafiki,bila kusahau UDOM sina habari za MZUMBE ila ARDHI nao ndio wameruddi chuoni baada ya kukaa mtaani kwa muda wa miezi ipatayo sita,POLENI sana marafiki na hongereni mlio likizo.

Ila katika vyuo vilivyofungulia baada ya ile crisis ya mgomo kuna watu mpaka leo hawajui mustakabali wao kwani hawajarudishwa vyuoni sababu ya kutolipa ada au kutojaza fomu,kwa wale wa UDSM ambao hawajamalizia ada wameambiwa muda umekwisha warudi septemba kurudia mwaka, na wale ambao hawakujaza fomu wameambiwa wao elimu ya juu waisahau,poleni sana marafiki na laana iwarudie mliosababisha wenzetu wapatao 138 kwa mlimani tu kupoteza sifa za kuwa wanachuo,hasa hasa DARUSO mliopita,ndugu Mchibya, Owawa na Silinde damu za hao watu ziwe juu yenu!!...hawa watu hawastahili kurudishwa kwani kwa mawazo yangu ndio waliotupotezea marafiki zetu!! ufinyu wa mawazo yao ndio uliosababisha yote haya,athari nyingine walioileta ni kufutwa kwa mazoezi kwa vitendo kwa mwaka huu,yaani field....zitafanyika next year!!


mungu tubariki wanavyuo wote Tanzania......tupe hekima na tusaidie kutatua matatizo yetu kisomi,na tusaidie tulete mabadiliko nchini.....marafiki mliopotea poleni ila mungu hamtupi mja wake!!