Sunday, August 31, 2014

BLOG IMEFUFUKA RASMI

Habari zenu wadau.......Za masiku tele.Ni mimi kijanacwenu William niliyeanzishaga hii blog kama miaka 6 iliyopita lakini kwa bahati mbaya ikashindwa kuendelea kutokana na changamoto mbali mbali hali ya kiuchumi ilikuwa ni mojawapo.Tulikuwa na vision kubwa kwa wakati ule lakini tulishindwa kutokana na michakato ya maisha na kutokana na kila mtu kusambaratika baada ya kumaliza vyuo.Ila tunamshukuru mungu kwani wote alitufanikisha maishani tuna kazi nzuri na tuna maisha kwa sasa.Ila sitaki vision yetu ife tufufue hoo kitu iwasaidie wanachuo na ikiwezekana yuwakabidhishe huku tukiwaongoza na kuandaa succession plan ili lisitokee tena kama lililotutokea kipindi kile kwani uwezo wa kifedha pia ulikuwa mdogo kuendesha blog.Tafadhali karibuni sana kwa maoni tufanyaje na tumkabidhi nani sisi tubaki kama wadhamini,ntafurahi ndoto yetu ikitimilizwa na wengine japo sisi si wanafunzi tena.Nilibarikiwa kumaliza ile Bcom na sasa ni muajiriwa wa shirika moja la serikali lakini shule bado zinaendelea kwa sasa.Karibuni sana tubadilishane mawazo kuhusu hili.Cheerz