Monday, August 18, 2008

KWA SITUATION HIZI BABA UWA UNAKUMBUKWA!!


Kama unavyoona picha ya baba wa taifa ikiwa hewani watu wanapodai haki zao....
Kwa nini migomo mingi inayotokea huwa baba wa taifa anakumbukwa?Reference ikiwa ni migomo ya UDSM na sehemu nyingine huwa wanatamani sana baba wa taifa awe hai...Je ni kweli angekuwa upande wetu au tunamsingizia...Hebu comment juu ya hilo!!
Hawa ni wanafunzi wa shule mbalimbali za dar es salaam walipokuwa wanapinga kuongezewa nauli kutoka Tsh 50 kwenda Tshs 100.
Kwa kweli Mtanzania anaendwa kuzikwa na mfumuko wa bei wa huduma na bidhaa.....
Tunaelekea wapi?? Baba fufuka kidogo japo kwa dakika na wewe utupe maoni yako.......
Poleni wanafunzi kwa sababu mlichopigania hakikufanikiwa!!
WEKA COMMENTS ZAKO HAPA CHINI.....

4 comments:

Anonymous said...

Mtu hawezi kupigana wakati hana uwanja wa kupigania. Those pupils had no grounds to stand on,they were fighting for the wrong cause. Maana gharama za maisha zimepanda, kutokupanda kwa nauli inamaanishi kuongeza mzigo kwa wtu wa daladala. Msimuingize baba wa Taifa katika mambo ya ajabu Labda kama mnataka kurudia ujamaa (Jambo ambalo alitakaa liwezekane)

Anonymous said...

Mtu hawezi kupigana wakati hana uwanja wa kupigania. Those pupils had no grounds to stand on,they were fighting for the wrong cause. Maana gharama za maisha zimepanda, kutokupanda kwa nauli inamaanishi kuongeza mzigo kwa wtu wa daladala. Msimuingize baba wa Taifa katika mambo ya ajabu Labda kama mnataka kurudia ujamaa (Jambo ambalo alitakaa liwezekane)

nangu said...

ama kwa hakika kuongezeka kwa nauli ya wanafunzi ni tatizo kwa sababu wale ambao wanaishi mbali kwa mfano anaishi tegeta alafu serikali imemchagua kusoma azania inamaana kwenda na kurud awe na sh.400 mbali na apo pengine mzee ni muuza samaki feri ina maana ili mzaz nae afike ofisini kwake anatakiwa awe na zaid ya sh.1000.sasa dhania mzaz ana watoto wawili wanaosoma mmoja azania na mwingine jangwani ina maana kwa siku upande wa nauli tu ni lazma awe na zaid ya sh.2500 je kwa ss ambao tunauwezo wa chin ni mzaz gan ambaye atawezo hayo.pengine kwa siku faida yake ni sh.2000 unazani ataweza kumudu nauli za watoto na chakula kwa pamoja?ama kwa hakika serikal inakosea kwa mawazo yangu madogo serikal ingejaribu kuweka nauli za wanafunz kam kawida yani 50.ili hata yule kayumba nae apate kuhudhuria masomo.kwa sababu hawa wanafunz ndio wasomi wa kesho na viongoz wa baadae.hakika kwa nauli hiz ,weng watashindwa kuhudhiria vipind week nzima kwa sababu ya uwezo mdogo wa wazee wetu.

Anonymous said...

Nangu, safi! Serikali imekosea saana kwa kushindwa kuweka muundo mbinu thabiti wa elimu ili pawe na shule zinazofikika kwa gharama nafuu na waalimu bora wa kutosha.

nakubali elimu ya sekondari si bora kiasi cha kulipa 1000 kila siku kwa nauli tuu. Elimu ni bora lakini haitakiwi kuwa ghali hivyo.

Lakini hao wazazi wacha wakome, wao ndo hawataki mabadiliko. Utawaona ukifika uchaguzi, wanachagua walewale waborondaji.

Daladala, pandisha nauli mtoe funzo dogo kwa gharama zaidi.