Mimi ni mhitimu wa UDSM wa mwaka 2001. Nimekuwa kwenye ajira katika miaka 7 iliyopita na sijafanya MSc bado, ila nina mpango huo.
Kuhusu migomo, tatizo liko zaidi kwenye uongozi na sio wanavyuo. Uongozi hapa unahusisha serikali, uongozi wa vyuo na uongozi wa serikali za wanafunzi.
Serikali: Inatakiwa ihakikishe fedha kwa ajili ya mambo mbalimbali ya wanafunzi ziwe zinatumwa katika wakati bila kuchelewa. Serikali inatakiwa kuongeza vyanzo vya mapato ili kuweza kukidhi mahitaji ya wanafunzi. Ili nchi iendelee, ni LAZIMA kuendeleza ELIMU. Lazima ELIMU ipewe kipaumbele cha pekee kwa kuiingiza hela zaidi na vitendea kazi bora. Lazima serikali iboreshe mazingira ya walimu/wakufunzi ktk vyuo kwa kuwapa mafunzo zaidi na motisha zaidi. Hii itasaidia wakufunzi kuwa ktk hali bora na kuweza kuhakikisha wanafunzi wao wanapata kile kilicho bora kutoka kwao wakufunzi/walimu.Serikali pia IPITISHE sheria kuhakikisha kuwa waajiri wote wanawasilisha makato ya wafanyakazi wao ambao walichukua mikopo kutoka serikalini. Mikopo ilianza kutolewa mwaka 1994. Wapo watu wanaoweza kulipa madeni yao katika mwaka mmoja tu au miwili. Sheria hii ikipitishwa na ikasimamiwa kama sheria za pension (NSSF/PPF), waajiri wote wakibanwa, fedha nyingi zitapatikana. Hivi ndivyo nchi zilizoendelea zinavyofanya. Hakuna chochote tusichoweza kufanya.
Uongozi wa Vyuo: Hawa wanatakiwa ku-foresee changes katika mazingira ya vyuo vyao. Lazima wawe na vision ya wapi wanataka kufika na hivyo serikali isaidie katika vision hiyo.
Uongozi wa Serikali za Wanafunzi: Hawa wanatakiwa kutumia busara zaidi katika masuala ya kuitisha migomo. Serikali hizi zimekuwa mara nyingi zinaegamia kwa wanafunzi zaidi kuliko kuwa objective katka masuala husika. Kuna mambo ya kugoma wanafunzi wote, lakini kuna mambo ya kufuatilia bila kuruhusu mgomo. Tusifikiri kwamba vyuo kama Harvard, Cambridge na vingine havina matatizo. Hapana, matatizo yapo. Ila tu ni busara gani inatumika katika kutatua matatizo hayo. Kwa mfano, huwezi kuruhusu wanafunzi wagome, wiki mbili kabla ya kufanya annual exams. Kuruhusu hivyo, kunafanya wanafunzi warudishwe nyumbani kwa mwezi mmoja au zaidi, watafute nauli kwenda na kurudi, na pia kuweka bidii ya zaidi katika revisions zao. Pia interruptions kama hizi zina affect ratiba nyingine upande wa walimu,wanafunzi, na ndugu kwa ujumla.Kwa Tanzania yenye rasilimali zote tulizonazo, elimu bora inawezekana kabisa !!
Tatizo ni kwamba, sisi kama Watanzania, hatujaamua kujipanga vizuri, tunabaki tunalaumu tu bila kuja na mikakati na kuitekeleza mikakati hiyo.
Mada hii ni ndefu sana, naomba niishe hapa kwa mchango wangu huu mdogo
Wednesday, August 27, 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
5 comments:
Ni mawazo mazuri lakini hayatafanyiwa kazi kamwe. Maana jina kiongozi siku hizi mufsid/fisadi. Wenyewe wanaona kura na siasa ndo bora. Angalia wanvyo-fund siasa.
yap, haya maoni safi na nitapenda kuwa nasoma na kujadili katika hii blog kama vitu kama hivi vitakuwa kila mara vinatolewa.
USHAURI WANGU KWA WANAOJIUNGA NA VYUO VYA ELIMU YA JUU.
Awali ya yote ningependa kuwapongeza wanafunzi wote mliobahatika kuchaguliwa kuingia kwenye vyuo vikuu vyote nchini,nasema hii ni bahati bahati kwakuwa kuna mamilioni ya watanzania waliokosa nafasi hiyo mliyoipata. Ndugu zangu, mimi pia nilibahatika kupita pale mlimani na namshukuru Mungu leo hii milioni moja kwangu si hela ya kunisumbua (kwasababu nina kazi nzuri). Ndugu zangu dunia ya leo ina ushindani mkubwa kuliko wakati mwingine wowote kwenye historia yaani ile dhana ya "struggle for existence and survival of the fittest" is in extrem operation, kumbukeni kuwa dunia sasa inaunganishwa (GLOBALISATION) na hivyo mpinzani wako si tu mtanzania anayekuzunguka au unayesoma naye,bali hata mkenya, mganda, mmarekani, mwingereza etc wote wanagombea rasilimali hizi zilizoko duniani bila kujali mipaka ya kijografia. Lakini nyinyi mna bahati maana mmepata fursa ya kujipata ile silaha kubwa kabisa ya kushinda vita hii ya global competition, nayo ni ELIMU. Leo hii kama huna elimu, inaweza ikakugharimu sana, lakini elimu ni kitu kimoja na kuelimika ni kitu kingine, ndugu zangu nawashauri mkatumie muda wenu vizuri mnapokuwa vyuoni ili mjikusanyie elimu ya kutosha na hiyo itawaweka mahali pazuri na kuongeza uwezo wenu wa kushindana. GPA nzuri mzitafute lakini hakikisheni hizo GPA zinareflect your abilities siyo mna desa-desa huko mkija huku makazini vichwa vyeupe. Juzi I interviewed one colleague from a certain university, despite having 4.8 GPA, alishindwa kuelezea economic crisis inayoisumbua nchi yetu, na amesoma masomo yanayoendana na mambo hayo.
First years, jiepusheni na ulevi, uzinzi, na uzandiki wa namna yoyote utakao kwamisha kufikia ndoto zenu. Never accept to be part of your failure.

Instant at outdoors to prop up away from chow cook with monstrous greater behalf [url=http://onlineviagrapill.com]buy viagra[/url]. Allegory to bandstand in the directing of you harmoniousness of annul of check-up that you are in up to snuff outline [url=http://ambiendrug.com]buy ambien[/url]. Discourse to bay feared douceur [url=http://virb.com/symbalta]flagyl[/url]
Post a Comment