Wa-Tanzania kama tunavyosifika kwa Amani na ukarimu duniani hilo pia limejitokeza kwa wanafunzi wanaosoma Algeria!!
Kama nilivyoambiwa kuwa pale chuoni kwao wanasifika sana kwa dhana yao ya urafiki na ukarimu kwani hawajawahi kukutwa na kesi kama ya uvutaji bangi,umalaya,ulevi na kadhalika.... Hapo kulia ni bwana Ibrahim Rashidi akiwa na rafiki zake waarabu wa Algeria na rafiki yake Mnamibia na wote wameahidi kuitembelea Bongoland waone hizo sifa zetu!!..Na hiyo picha ya pili katikati ni msichana wa Msumbiji nae kaahidi kuja Tanzania...
Je hizo sifa ni za kweli??..Na hizo sifa za mabonde na milima tutaendelea nazo mpaka lini wakati tu masikini siku zote??...Je tujivunie kwa nini waTanzania??.....Si mmesikia watalii wetu tuliowatuma huko Beijing kwenye Olimpic hawajarudi hata na medali ya shaba??..Sasa tujivunie nini??....Basi sababu walienda kutalii basi warudi hata na bidhaa walizonunua huko China!!
TOA COMMENTS ZAKO HAPA CHINI MDAU......
2 comments:
Hi! mimi ni mwanafunzi kutoka chuo cha ufundi Karume Zanzibar (karume Institute of Science and technology), ni mpya katika hii blogs, so nahitaji maelezo zaidi kuhusu ushiriki katika hili. thanks..
Hi! mimi ni mwanafunzi kutoka chuo cha ufundi Karume Zanzibar (karume Institute of Science and technology), ni mpya katika hii blogs, so nahitaji maelezo zaidi kuhusu ushiriki katika hili. thanks..
Post a Comment