Wadau kama mmefuatlia vyombo vya habari nadhani mtakuwa mmesikia kuhusu hii skendo ya hapo chuoni mlimani.Uongozi wa wanafunzi DARUSO umetangaza mgogoro usioisha na utawala wa chuo kikuu cha Dar es Salaam kutokana na Utawala kugoma kutoa matokeo ya watu ambao hawajamalizia ada zao.......
Sijui itakuwaje huko mbeleni...japokuwa sisi hatutamani mgomo utokee kwa sababu tunaju athari za migomo.....Nadhani DARUSO watakuja na solution nyingine tofauti na migomo tuliyozoea.....na ninaamini uongozi wa chuo utatoa matokeo ili kuepuka migogoro zaidi...
Migogoro haitusaidii bali inashusha hadhi yetu na kutudhalilisha.....Nadhani mazingira salama kwa wanafunzi wageni kutoka nchi za nje yanapokosekana hadhi ya chuo inashuka sana...............
Kwa hiyo tunaamini pande mbili za DARUSO na UTAWALA watakuja na ufumbuzi wa maana ili tubaki salama na tuendelee na masomo!!
Friday, September 12, 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
2 comments:
Hivi vyuo vina hadhi tofauti?
Lipeni fedha mgogoro uishe.
Mnapenda kupata fedha halafu hamtaki kulipa mnapodaiwa mnataka msaada tu kila siku.
Wasomi halafu mnakuwa kama sio wasomi kwa kupenda dezo.
Iweje muone raha pale wazee wa EA hawajalipwa mpaka leo halafu nyinyi mlipwe kila siku kila mnachotaka.
Post a Comment