Tuesday, September 30, 2008

JE WADAU MNAMKUMBUKA DADA AMINA CHIFUPA??


Yapata mwaka na miezi michache tangu dada ye2 Marehemu Amina Chifupa atutoke duniani !
Kwa wale wapenzi wa Clouds FM tutakumbuka sauti yake nzuri na wale Wanaharakati za za Siasa mtakumbuka harakati zake wakati akiwa Mbunge wa Jamhuri ya Muungano.
MUNGU AZIDI KUNEEMESHA PEPO YA DADA YE2
J e mdau unakumbuka nini au nini kilikufurahisha kwa Dada Amina?
Pichani Akila kiapo mbele Bungeni kma Mbunge na nyingine akila pozi kisela home kwake !


Huyu ni mtangazaji Dina Marios wa
Clouds FM. Ndio hivi sasa anakalia kiti alichowahi kukalia Marehemu Amina Chifupa .Dina Marios anaendesha kipindi cha Leo Tena kinachorushwa na radio hiyo Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saba mchana.

Kama asingekuwa anajitambulisha kipindi kinapoanza wasikilizaji tungeendelea kuamini kuwa mtangazaji bado ni Amina.Voko mlemle mwanangu! Naona kisura wanashabihiana !Kama mdogo wake vile !

No comments: