Sunday, September 14, 2008

SALAMU ZA WEEKEND KUTOKA RUSSIA....


Huyu ni Boniface Elphace Magina raisi wa wanafunzi wa kitanzania wanaosoma huko Urusi........
Nimezipata salamu zake weekend hii na zinawaendea wanafunzi wote wa kitanzania waliopo popote pale duniani!!
Kwa niaba yao namuambia zimewafikia...na ninatumaini wanafunzi kwa sasa wanaendelea vizuri mara baada ya matatizo yao ambayo yaliwakuta mwezi uliopita.
Anawaasa tuungane wanafunzi wote wa kitanzania popote pale tulipo duniani na njia ya kwanza ndio hii kwa kujua nini kinaendelea popote walipo wanafunzi wa kitanzania!!

1 comment:

Anonymous said...

wewe uliyepost hizi salamu,naomba uirekebishe na usahihishe usemi wako kuwa 'RAISI WA WANAFUNZI WA KITANZANIA WANAOSOMA URUSI'
kwanza unatakiwa ufahamu kuwa huyo ni RAIS WA WANAFUNZI WA KITANZANIA WALIOPO AMA MOSCOW AU PATRIC LUMUMBA PEOPLE'S FRIENDSHIP UNIVERSITY.[sina uhakika,maana hata moscow pia kuna vyuo vingi,sio patric lumumba pekeyake kama wengi walivyo kariri]. Na sio kwa urusi nzima.
kuna wanavyuo wakitanzania wapo ktk vyuo na miji mbalimbali ya hapa urusi,na kila jumuiya ya watanzania ktk miji hiyo ina RAIS WAKE. hivyo sahihisha kauli yako usipotoshe umma.na hakuna jumuiaya 1 inayo waweka wanavyuo wote chini ya uwakilishi wa huyo unaye muita rais wa watanzania walioko urusi.