Samahani wadau wangu wa vyuotz...hili swala limeniumiza kichwa kwa muda mrefu sana kwa hiyo nimebidi nililete kwenu.......
Mwaka 1961 wakati nchi ya Tanzania inapata uhuru...inavyosemekana tulikuwa sawa kiuchumi,miundombinu na vinginevyo na nchi kama Malaysia,Singapore,Korea na nchi nyingi za Asia....Lakini ukiangalia kwa sasa wametuacha mbali mno katika nyanja za uchumi,miundombinu na maendeleo kwa ujumla na huwezi kuamini kama hapo mwanzo tulikuwa sawa!!
Sasa ni nini kinachosababisha wao watuache sana kiasi hicho....Iweje wao wanakimbia sisi tunatambaa??....Wasomi jamani hebu ongeleeni hili kidogo...nanyi mlio nje ni nini hasa kinachofanya sisi tuwe nyuma...sera za huko zikoje?hebu angalia picha za jiji letu la DSM hapo juu...jiji ambalo linaaminika kuwa mwaka 1961 lilikuwa sawa na jiji la Seoul la Korea!!
NASUBIRI MICHANGO YENU WADAU!!
4 comments:
Kikwete, Membe wanavyotuburuza OIC tusikubali
M. M. Mwanakijiji
KATI ya mambo ambayo sikutaka kuyagusa kwa kina ni suala la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC). Inaonekana serikali ya Rais Jakaya Kikwete imedhamiria kuwa liwalo na liwe Tanzania itakuwa mwanachama wa jumuiya hiyo.
Wamechukua uamuzi huu wa woga baada ya kushindwa kuchukua msimamo wa kijasiri kuwa Tanzania kama nchi huru isiyo na dini haiwezi na haipaswi kujiunga na jumuiya hiyo, kwa kuwa jumuiya hiyo ina malengo na misimamo inayokinzana na maslahi ya taifa letu.
Sababu kubwa ambayo watawala wameitoa inayoonekana ndiyo pekee inayowafanya kuiingiza nchi yetu kwenye OIC ni kutaka kusaidiwa. Yaani tumekuwa wategemezi kiasi kwamba kutokana na kupenda kusaidiwa tuko tayari kuuza hadhi yetu kama nchi na uhuru wetu ili tupate misaada.
Inaonekana serikali yetu mbele ya wanaotoa misaada inanywea na kufyata mkia na kukubali kuburuzwa alimradi tupewa misaada. Huu ni msimamo wa watu waoga.
Baadhi ya watu wanapinga Tanzania kujiunga na taasisi hiyo kwa sababu wanafanya hivyo wakiangalia Tanzania na kusema Katiba yetu hairuhusu hivyo.
Hiyo hoja kwa kweli inaweza isiwe na nguvu sana. Binafsi napinga Tanzania kujiunga na taasisi hiyo kama nchi, kwa sababu taasisi hiyo ni nini, ikoje na ni ya nani.
Hoja yangu ni kuwa Tanzania haipaswi kujiunga na OIC kwa sababu malengo na dira ya jumuiya hiyo ni kinyume kabisa cha kila kitu kinachoifanya Tanzania kuwa Tanzania.
Hata hivyo, hilo haliondoi uwezekano wa jumuiya yoyote ya Kiislamu nchini kuwa mwanachama au mshiriki wa aina fulani ndani ya OIC au kuizuia serikali kufanya kama walivyofanya Marekani yaani kuwa na mwakilishi mtazamaji (observer).
Uamuzi wa kujiunga na OIC ambao umechukuliwa na Rais Kikwete ni uamuzi ambao lazima upingwe na kila Mtanzania mwenye kutaka umoja, usawa na haki kwa kila raia.
Je, kutojiunga na OIC ina maana Tanzania isipewe misaada na nchi wanachama wa OIC? Jibu la swali hili linaonesha ni jinsi gani Tanzania imepoteza ujiko wake wa kidiplomasia.
Ina maana ya kwamba Wizara yetu ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa chini ya Bernard Membe, imeshindwa kuingia majadiliano na hatimaye makubaliano ya nchi na nchi (bilateral agreements) kati ya Tanzania na nchi moja moja wanachama wa OIC.
Mtindo huu upo duniani na unatumiwa na nchi nyingi, Kama Canada imekuwa ikifanya majadiliano ya kulinda wawekezaji wake kwa kuzungumza na nchi moja moja badala ya kundi zima. Na zaidi si lazima kwa nchi hizo kujiunga katika ushirika fulani ili zipatiwe misaada na Canada.
Inashangaza kuona kuwa OIC - aidha kwa kututega au kwa kutumia nguvu zake za kiuchumi - zimetubania na kutuwekea ngumu kuwa pasipo Tanzania kuwa mwanachama wa OIC basi hakuna misaada kutoka jumuiya hiyo.
Kama hili ni kweli, basi yawezekena walioiteka nyara Tanzania si mafisadi tu bali pia kikundi cha nchi fulani ambacho hakipo tayari kuisaidia Tanzania na watu wake wote isipokuwa kwanza tupige magoti na kujiunga nacho! Hili linatisha.
Lakini kabla ya kuwalaumu OIC hebu tuangalie wao wenyewe wanasema nini kuhusu jumuiya hiyo.
OIC imekataa kutambua Azimio la Umoja wa Mataifa Juu ya Haki za Binadamu. Nchi wanachama wa OIC kutokana na kuunganishwa kwao na imani ya dini ya Kiislamu ililikataa Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu (ambalo Tanzania imekubali) na kupitisha Azimio lao la Cairo, Misri, kuhusu haki za binadamu.
Kukataa kwao lile la Umoja wa Mataifa kumetokana na kutambua kuwa baadhi ya mambo yaliyomo kwenye Azimio la Umoja wa Mataifa yanapingana na mafundisho ya dini ya Kiislamu.
Ibara ya 24 ya Azimio la Cairo inatangaza wazi kuwa “Haki zote na uhuru unaotangazwa kwenye Azimio hili vyote viko chini ya Sharia za Kiislamu” na ibara ya 25 inasema “Chanzo pekee cha kuelezea na kufafanua vipengele vya Azimio hili itakuwa ni Sharia ya Kiislamu”.
Hii ni haki ya jumuiya ya OIC kuchukua msimamo unaoendana na lengo na makusudio yake. Je, Tanzania ikiwa mwanachama kamili wa jumuiya hii inalitambua Azimio la Cairo kuhusu haki za binadamu?
Lakini zaidi tuangalie makusudio na malengo ya OIC ili tuone kama yanaendana na makusudio ya nchi yetu na kama yanalinda maslahi ya Watanzania wote (si kikundi kimoja cha Watanzania).
Ibara ya kwanza ya Katiba ya OIC ina vipengele vinavyoelezea majukumu yake na malengo yake. Inataja malengo yapatayo 20, ambayo ni ya kutufanya tufikiri ni kadhaa.
La kwanza ni lengo namba nane linalosema mojawapo ya malengo ya OIC ni “kuwaunga mkono na kuwawezesha wananchi wa Palestina kuweza kutumia haki yao ya kujiamulia mambo yao wenyewe na hatimaye kuunda taifa lao hakimiya (sovereign), likiwa na Al-Quds Al Sharif (Yerusalemu) kama makao yake makuu na kulinda alama za Kihistoria na Kiislamu pamoja na maeneo matakatifu yaliyomo”.
Tunapojiunga na OIC ina maana ya kuwa Tanzania sasa imechukua msimamo wa kupigia kampeni kuwa Palestina iwe na makao makuu Yerusalemu na kulinda mambo ya “kihistoria” na alama za Kiislamu lakini kutotambua na kulinda alama za Wayahudi. Tukijiunga na OIC kama nchi tutakuwa tumeamua kuwa wenye haki ya Yerusalemu ni Wapalestina na Wayahudi hatuwatambui.
Lengo la tisa linasema kuwa ni “kutilia mkazo mahusiano ya Kiislamu katika biashara na uchumi baina ya wanachama; lengo likiwa kufikia muungano wa kiuchumi (economic integration) na hatimaye kufikia soko la pamoja la nchi za Kiislamu”.
Je, Tanzania tuna malengo hayo? Je, Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ina malengo ya kuifanya Tanzania siku moja tuwe kwenye soko la pamoja la nchi za Kiislamu? Inaonekana CCM wameamua hilo tayari na sasa ni kulitekeleza tu.
Lengo la 11 la OIC linasema kuwa “ni kutangaza, kueneza na kuyatunza mafundisho ya Kiislamu na tunu ambazo msingi wake ni kiasi, kuvumiliana, kueneza utamaduni wa Kiislamu na kutunza urithi wa Waislamu”.
Lengo hili ni zuri na linaendana kabisa na jumuiya yenyewe. Tunapotaka kujiunga nao ina maana tumelikubali na tutafanya hivyo. Je, hilo ndilo serikali ya CCM iliwaahidi Watanzania kwenye kampeni zake za 2005 chini ya rais Kikwete?
Jibu inaonekana “ndiyo”. Kuwa serikali ya Tanzania kwa kukubali kuingia kama mwanachama kamili wa OIC inataka kutimiza lengo hilo.
Ibara ya pili ya Katiba hiyo inaelezea kiujumla kuwa malengo yote 20 (hata yale yasiyotaja moja moja Uislamu) yataongozwa na mafundisho ya Kiislamu.
Hivyo, hata malengo yanayohusu kusaidiana kiuchumi, sayansi, na teknolojia yote yanazunguka kwanza katika msingi wa mafundisho ya Kiislamu. Je, tuko tayari kuyashika hayo kama taifa?
CCM na serikali zake mbili inaonekana imeamua kutoa jibu la ndiyo. Hivyo ni kama uzugaji kwa Balozi Seif Iddi kudai kwamba OIC haihusiani na sharia za Kiislamu, naomba aangalia hiyo Katiba ya OIC vipengele nilivyovitaja.
Swali ambalo nilikuwa najiuliza ni Tanzania itajiunga kwa misingi gani kwenye OIC wakati yenyewe siyo nchi ya Kiislamu?
Jibu linapatikana ibara tatu kipengele cha pili cha Katiba ya OIC. Kipengele hicho kinasema kuwa “Nchi yoyote ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa, yenye Waislamu wengi kuliko dini nyingine (Muslim Majority) na inakubali katiba hii, ambayo itatuma maombi ya kujiunga itaweza kukubaliwa unachama pale tu itakapopitishwa na Baraza la Mawaziri wa Nchi za Nje kutokana na vigezo vilivyowekwa na baraza hilo”.
Kwa vile serikali yetu chini ya rais Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje, Membe, wameamua kuliingiza taifa letu kwenye OIC ina maana ya kuwa wametambua na kukubali kuwa Waislamu ni wengi zaidi kuliko watu wa dini nyingine nchini na hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Waislamu wengi (muslim majority).
Kama hili ni kweli, swali langu kwa Membe ni lini walifanya sensa ya kutambua dini za watu?
Baada ya kuisoma katiba hiyo na kuielewa vizuri na nyaraka nyingine naweza kusema kwa uhakika wa wazi kabisa kuwa Tanzania kama nchi haipaswi, haistahili na isilazimishwe kamwe kujiunga na OIC.
Hili kwangu halina mjadala isipokuwa kwa wale wanaotumia hoja za nguvu (dola); kwamba kwa vile wao wana vimulimuli na wanapigiwa saluti nchini basi wanaweza kuiingiza Tanzania kokote kule kama alivyosema Balozi Seif hivi karibuni.
Je, niseme kuwa Tanzania isishirikiane na OIC katika mambo ya maendeleo na kupokea misaada kutoka OIC? La hasha. Ninaamini kuna njia kubwa mbili za Tanzania kuweza kushirikiana na OIC kwa mujibu wa Katiba ya Jumuiya hiyo ambazo nina uhakika Watanzania hawatakuwa na matatizo nayo.
Njia ya kwanza inapatikana katika ibara ya nne (1). Katika ibara hiyo katiba ya OIC inasema kuwa wapo wanachama watazamaji ambao wanaweza kukubaliwa nafasi hiyo. Inasema hivi “Uamuzi wa kuipatia nchi yoyote mwanachama wa Umoja wa Mataifa hadhi ya Uangalizi (Observer status) utatolewa kwa makubaliano ya Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje tu kwa vigezo ambavyo Baraza hilo limeweka”.
Kipengele hiki ndicho kilichoziwezesha nchi kama Bosnia na Herzegovina, Urusi, Marekani, Jamhuri ya Afrika ya Kati kuwa watazamaji wa OIC. Naamini Tanzania inaweza kuhusiana na OIC kwa Rais Kikwete kumteua balozi maalumu wa Tanzania kwenye Jumuiya ya OIC bila nchi yetu kuwa mwanachama.
Naamini hili litakuwa ni ‘compromise’ kati ya wale wanaotaka tuwe na uhusiano rasmi na OIC na wale ambao hawataki kabisa kuwa na uhusiano huo. Endapo tutakuwa na uhusiano wa utazamaji na wakati huo huo kuingia mikataba ya ushirikiano na nchi wanachama kati ya nchi na nchi (kama ambavyo tumekuwa tukifanya) basi hatutakuwa na matatizo mengine mengi ya kikatiba.
Hapa naomba nijibu baadhi ya mapingamizi ambayo yamekuwa yakitolewa na wale wanaotaka Tanzania iwe mwanachama rasmi wa IOC.
Pingamizi la kwanza; Lazima tujiunge OIC kwa sababu mbona hatulalamiki kwa Vatican kuwa na ubalozi wake nchini? Hoja hii ina lengo la kugusa hisia na vionjo vya watu kuliko kushawishi akili.
Mtu anayetoa hoja hii anafanya hivyo bila kugusia upande mwingine kuwa Iran, Palestina, Libya, Syria zina balozi zao nchini. Nchi hizi zote nne na hasa Iran ni nchi za Kiislamu.
Iran hasa kiongozi wake wa juu kabisa ni kiongozi wa kidini kama alivyo Papa. Kwa nini basi wanapouliza swali hili hawaulizi uwepo wa ubalozi wa Irani nchini?
Jibu ni jepesi. Wanafahamu kuwa Vatican kama vile Iran ni nchi kamili licha ya kuwa ina viongozi wa dini kama wakuu wake. Lakini kosa jingine ni kuwa wanapolinganisha OIC na Vatican ni kulinganisha machenza na ndizi.
Moja ni jumuiya ya nchi mbalimbali na nyingine ni nchi kamili. Endapo Tanzania ingekuwa mwanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kikristu duniani basi hoja ya kujiunga na OIC isingekuwa na utata wowote ule.
Mojawapo ya jumuiya za kimataifa za Kikristo ambazo zinafanya kazi nchini na kutoa misaada ya kila aina kwa Wakristu, Waislamu, na Wasioamini ni Caritas. Tanzania si mwanachama wa Caritas na misaada yao haiitaji tuwe wanachama kwanza. Kwa nini misaada ya OIC itutake tuwe wanachama kwanza?
Pingamizi la pili; Tukijiunga na OIC tutapata misaada mingi kwa Waislamu pia kwa ujumla tunaweza kupata bei nafuu ya mafuta na misaada mingine ya kiuchumi. Hoja hii nayo ina lengo la kuchezea hisia za watu.
Kama kuna jumuiya ambayo tungetakiwa kweli kujiunga nayo ili kupata unafuu wa mafuta ingekuwa kama OPEC na si OIC. Hadi hivi sasa sijasikia ni nchi gani mwanachama wa OIC ambayo imepata unafuu wa mafuta kwa sababu ni mwanachama wa OIC na si vinginevyo. Ingekuwa bei ya mafuta inaweza kufanywa rahisi kwa kujiuinga na OIC basi nyingi duniani zingeshajiunga.
Lakini kubwa zaidi na nimelisema hapo juu ni kwamba tayari tumekuwa na ushirikiano na nchi nyingi zilizomo kwenye OIC. Tumekuwa na ushirikiano na Qatar, Saudi Arabia, Oman, Iran, na nyinginezo nyingi, kati ya hizo zimekuwa zikitoa misaada ya aina mbalimbali.
Kwa maneno mengine ni kuwa nchi nyingi za OIC zinatoa misaada tayari kwa Tanzania bila kutulazimisha kuingia OIC. Ni kitu gani zaidi tutakipata kwenye OIC ambacho hatuwezi kukipata kwa kujadiliana na nchi kwa nchi?
Ninaamini kuwa uamuzi wa kuiingiza OIC ni uamuzi wa kibabe ambao lengo lake halihusiani na mafanikio yoyote ya kiuchumi isipokuwa kuwaridhisha watu wachache ambao wanaona pasipo kupewa hicho basi “Waislamu wanapigwa vita”.
Kama lengo la kujiunga OIC ni kuwasaidia Waislamu (kama Katiba ya OIC inavyosema) basi jumuiya ya Bakwata au nyingine ya kimataifa ya Waislamu nchini inaweza kujiunga OIC kwa mujibu wa ibara ya nne (2) ya Katiba ya OIC.
Sidhani kuna Mtanzania yeyote ambaye atapinga Bakwata au jumuiya nyingine ya Watanzania kujiunga na OIC kwa kutimizia malengo ya jumuiya hiyo.
Vinginevyo, tuseme ukweli kuwa uamuzi huu ni wa papara, woga na wenye msingi wa kuendeleza mgongano usio wa lazima kati ya Wakristo na Waislamu. Ni uamuzi unaokwepa kushughulikia matatizo ya kweli ya Waislamu na badala yake kuwageresha kama kwa pili kwa kuiingiza nchi kwenye OIC.
Waislamu wanaofikiri kuwa kujiunga na OIC kutatatua matatizo yao na jamii yetu wanajidanganya. Tayari Tanzania ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa na mashirika mengine mengi ya kimataifa yanafanya kazi nchini.
Kama tungekuwa na uongozi wenye kujali maendeleo ya wananchi tungekuwa tumeendelea zamani. Tulichozoa ni kuzugwa na hatuwezi kukaa bila kuzugwa.
Sasa wamefikia mahali pa kuwazuga Waislamu kwa kuwapatia OIC kama pipi tofi ili wanyamaze kulalamika. Binafsi ningewasihi ndugu zetu waislamu kudai Tanzania iingie makubaliano na nchi kadhaa ambazo zina lengo la kutoa misaada kitu ambacho ni bora na rahisi zaidi kuliko kujiunga na jumuiya kubwa yenye malengo mengi.
Vinginevyo wakati umefika wa jamii nzima kupinga uamuzi wa serikali kuliingiza taifa letu kwenye OIC kinyume cha katiba yetu, tukipingana na Katiba yenyewe ya OIC na kwa hakika ikichochea mgongano usio wa lazima.
Tutawakatalie watawala wetu hawa ili wajue kuwa hatukubali. Ikibidi maandamano ya mshikamano kufanyika basi yafanyike, vinginevyo huko mbeleni msishangae bendera ya nchi nyingine ikipeperushwa Ikulu. Ndipo tutakuwa tumechelewa na kugundua kuwa Taifa letu tayari limeuzwa.
Unaweza kusoma Katiba ya OIC kupitia
We jamaa unaevalia njuga OIC, ukiangalia vizuri utagundua mchakato mzima wa mawazo ya kujiunga au laa yana msukumo wa kidini kabisa.
Wakristo wanasema hapanaaa, waislmu wanasema ndiyooo.
Kwa hiyo haya ni sawa na mabishano mengine ya kidini kama mke mmoja wake wengi? au Yesu Isa? Mungu God?
Zitatolewa sababu za kisiasa na kiuchumi lakini lengo lake ni kukidhi imani za kidini.
Hapa hapatakuwa na mawazo huru kuhusu suala hili labda tuwasikilize wapagani.
bad administration.uongozi mbaya!
tunasingizia umaskini,lkn mı huwa najiuliza ni umaskini unodhoofisha uchumi au mipango mibaya ya utumiaji fedha ilokuepo?
inasikitisha kuona viongozi wetu wa tanzania wakisha kuingia madarakani wanachofanya ni kuweka mikakati jinsi gani watashinda chaguzi zifuatazo!
hilo lipo zahiri badala ya kutafuta miundombinu ya kuondoa umaskini sie tumekaa tu,tunasubiri viongozi wa nje watupe misaada!hıvyo mnafkiri ni nani asiyekua mtanzania akwa na uchungu wa watanzania ikiwa sisi wenyewe hatuna uchungu na nchi yetu na watu wetu?
leo hii tz mgeni kutoka nje ndio atapewa asimamie miradi mikubwa ya hapa nchini,kwanini asianzishe ya kwake ili nasi tukafaidika kwa kumtoza kodi,na kodi hiyo ikatumiwa kihalali kwa kukidhi mahitaji ya jamii kama maji.umeme usafi wa mji na makzi bora.
kuna fununu nmezipata kuwa viongozi wetu wakiona mzungu wanamnyenyekea sana hata pesa ya kuanzisha biashara wanatoa wao kumpa mzungu ili waonekane kama wageni wanawekeza,na pesa yenyewe ni ya mali ya serikali.
viongozi wapo sehemu mbalimbali wanashindwa kusimamia vizuri kazi zao matokeo yake walokuwepo chini nao hawashuhuliki wanatumia muda kutafuta hela zaidi ktk kampuni za binafsi.
hivyo viongozi wetu hawaoni kwanini kampuni za watu binafsi zinaendelea na kupata faida wakati za serikali zinafilisika?tatizo nini mi naona uongozi mbaya.
ingekua viongozi wote ni wakali kama wanavyosimamia biashara zao binafsi tungekua mbali zaidi,kila mtu angefanya kazi yake vizuri wala hakuna pesa inayopotea,lakini kiongozi anatumia pesa za umma mbali na mshahara wake,je wa chini yake unategemea atafanya nini!
tunabaki kuomba,sijui tuataomba mpaka lini.
mimi naamini watoke viongozi wa marekani watupishe wao huko na wao waje afrika,basi huko marekani baada ya miaka kumi kutageuka afrika na afrika kutakua marekani,sote tutakimbilia afrika..........
binadamu yeyote hapa duniani anauwezo karibiasawa na wa mwenzie,ila namana ya kuutumia uwezo wake inatofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine! wengine wana moyo wa kujituma wenyewe,wengine lazima wasukumwe kama punda kihongwe,na wengine wapo tu hadi waambiwe cha kufanya ndipo wanaweza kufanya!yaani usipo waambia hata kama wewe unaona hilo ni tatizo mfano kufagia chumba,basi yeye yuko radhi chumba kichafuke,kinuke ila hawezi chukuwa ufagio akafagia na kukipamba hata kutandika kitanda na kuosha vyombo pia.
ninacho jaribu kusema ni kwamba watanzania ugonjwa wao na waafrika wengine upo kichwani.siku watakapo amua kila mmoja kuwa na maisha mazuri kwa ajili yako na wanao,basi nchi itaendelea. lakini wewe unazaa watoto 10,vimada 3 kisha hata ada ya shule hujui wataitoa wapi ungali uko hai,wala hufikirii ukifa gafla wataishi vipi!unabaki unailaumu serikali unategemea kama kuna watu milioni 20 kati 38 wenye akili ya namna hiyo hiyo tz itaendelea? tutaendelea kusubiri waliopata taabu wakajifunza wakatafuta suluhisho waendelee kwenda mbele,huku sisi tuliokuta matunda,juwa,wanyama vipo njenje tukadumaa akili,hadi sasa kazi yetu moja tu!tafuta mademu,nyumba ndogo,n.k pata virusi vya ukimwi kisha omba ARV kutoka marekani!hahahaaaaaaa!wafwa! hhakuna maendeleo bila kuamua wewe kwanza kisha jirani yako n.k do something first,don't point on somebody else! the time is now!
Post a Comment