Wednesday, October 22, 2008

BASI TUANGALIE NA SEHEMU NZURI KIDOGO!!

Hii ndio mabibo block D......Nadhani ni sehemu nzuri ambayo twaweza jivunia kwani majengo mengi ya vyuo vyetu Tanzania hasahasa ya Hostel yana hali mbaya..............
Chuo kikuu cha Dodoma wenyewe wana majengo mazuri kwa sababu ndio kwanza mapya japo sina uhakika na utunzaji huko mbeleni..kwani tunafahamu utunzaji wetu wa majengo watanzania ulivyo...............
IFM walikuwa wanajaribu kufanya marekebisho kidogo sijui uongozi umefikia wapi kwani bado kuna sehemu zina hali mbaya...hasahasa yale majengo yanayotazamana na BOT kule nyuma kuna hali mbaya sana..........ukija UDSM jengo la faculty of Arts yaani Tower Block lina hali mbaya hapo sijaongelea mahall yaliyochoka...yaani kuanzia hall one to hall six....angalau kidooogo hall seven!!
Lakini ni tatizo la nchi..kwani hata majengo ya idara fulanifulani za serikali yana hali sio nzuri kidogo...........Halafu na nyie faculty ya sheria pale UDSM hebu pakeni rangi kidogo hilo jengo lenu.....nyie faculty kubwa bwana!!
Big up kwa watu wa FCM kwani naona jengo lenu linaridhisha na mnaendelea na marekebisho na ujenzi...........!!

4 comments:

Anonymous said...

usafi udumishwe.

maji yakipatikanwa kirahisi

majumba kupakwa rangi kila mwaka.

uzuri utaendelea

otherwise tutajenga na kubomowa

Anonymous said...

UFISADI NDIO TATIZO.....NADHANI RUZUKU UWA ZINAPATIKANA KWA AJILI YA RENNOVATIONS ZA VYUO VYETU NA MASHULE....SWALA NI KWAMBA VIONGOZI WA VYUO WANAONA NDIO SEHEMU YENYEWE YA KULA

Anonymous said...

有一天,我一个炸药的朋友!

Anonymous said...

Mimi nimemaliza form six mwaka huu na matokeo yangu ni division 3 points 17 nina E ya Geograph E ya Economics na F ya Maths nilikua naomba kuuliza kwamba kwa kiwango hicho cha ufaulu nitapata chuo?