Monday, October 13, 2008

DHANA YA MIGOMO NA MAANDAMANO HAIJAISHA!!

Wenzetu wa chuo cha Ardhi bado wako nyumbani..... Ukiacha hivyo tu bado masharti waliyopewa ili kurudi chuoni ni magumu kwani wameambiwa waandike barua inayojumuisha maelezo mengi sana................
Nilipopata nafasi ya kuongea na rafiki mmoja wa hapo Ardhi amenieleza kuwa migomo hajaona faida yake mpaka leo...zaidi ni stress na mawazo pamoja na kudisturb ratiba za vyuo na wanavyuo na kuwatesa wanafunzi...............
Hii imetokea kwao Ardhi kwani walikuwa walishapewa fedha za kujikimu kwa wale ambao walikuwa wamekwishalipa ada...baada ya kufukuzwa chuoni wengi wao walitumia fedha hizo kama nauli za kurudi kwao na matumizi madogomadogo safarini,na kuwa wazi tu ni kwamba wanaendelea kutumia fedha hizo nyumbani kwa kufutilia vyombo vya habari na mambo mengine.............bado wanatakiwa kuposti barua hiyo ya maelezo......!!
Sasa wakirudi chuoni wataishije angali hawana fedha mfukoni....??...Angalia athari za migomo jamani...!!..Halafu naomba unayejua faida za migomo uniandikie hapo kwenye comments nizijue halafu andika na athari tuone kati ya athari na faida kupi ni zaidi??

Nimeshindwa kushangaa juzi baada ya kuona UDSM wanajiandaa na maandamano na mgomo huo uliotangazwa na TAHLISO...Jamani jamani watoto wa masikini tutateseka sana...mkifukuzwa chuo balaa lake mnalijua...au mnapenda kukaa kwenu...............nanyi mwaka wa kwanza ambao hamjawahi kugoma...mnaielewa vizuri migomo??..Siku zote vyombo vya habari hutuchafua kupitia migomo hiyo kwa kuleta dhana ya kuwa wanachuo ni wahuni...!!
Viongozi hivi hamjui njia nyingine za kutatua matatizo...??
SIJUI ITAKUWAJE...MUNGU WABARIKI WENYE DHANA POTOFU ZIBADILIKE WAWE NA FIKIRA NJEMA...!!

4 comments:

Anonymous said...

ndo mana tz hatuendelei.hao wanaogoma ndo wanatarajiwa kua viongozi wa baadae

ni shame kushindwa kutatua matatizo yetu wenyewe bila ya migomo

Anonymous said...

Mungu alimbariki mwanadamu kwa kumpa free-will (utashi au uhuru wa maamuzi), ili aamuwe akitakacho na awe responsible kwa maamuzi yake.

Sihisi kama ni kazi ya Mungu kuwakunja watu woote wafikiri fikra moja, hatutakuwa watu sasa bali kundi la maroboti. Sala yako Jax inaweza kuwa na walakini kwani inalenga kuondoa baraka ambazo tumepewa tayari-free will.

Tukitaka tusigome basi tunaofahamu ubaya wa migomo tuwafundishe wenzetu, kwani uwezo wa maamuzi hukuwa kwa elimu.

emmino said...
This comment has been removed by a blog administrator.
Anonymous said...

Jax kuwa huru zaidi, waachie watu wacomenti, usizidishe utawala