Viongozi wasisitiza wataandamana kushinikiza wenzao warejeshwe ::
Wapanga kuvaa vitambaa vyeusi kuomboleza msima elimu ya juu ::
Kamanda Kova aonya kama hawana kibali wasithubutu, watakiona cha moto
WANAFUNZI 2,000 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliofutiwa udahili, wameapa kutumia kila mbinu kuhakikisha wanajiunga na wenzao chuoni hap oleo, wakitishia kuwa hata ikibidi wafe, basi wapo tayari. Moja ya mbinu walizopanga kuhakikisha wanafunguliwa lango kuu na kuingia chuoni, ni pamoja na kufanya maanadamano makubwa, yatayowalazimisha walinzi kufungua lango la kuingia chuoni.
Ingawa hawakuomba kibali cha polisi, wanafunzi hao wamesema watafanya maandamano hayo kwa amani, huku wakiwa wamevaa vitambaa vyeusi kuashiria msiba wa elimu ya juu Tanzania.
Mbali na maandamano hayo, baadhi ya viongozi wa wa wanafunzi wa chuo hicho kwa kushirikiana na wenzao kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba na Afya cha Muhimbili (MUHAS), Umoja wa Vyuo vya Elimu ya Juu vya Umma Tanzania (UVEJUTA), wamesema wapo tayari kumwaga damu. “Kesho (leo) ni siku itakayotumika kumwaga damu za maskini ili kuleta haki katika elimu ya juu Tanzania. Bila haki hakuna amani,” alisema Rais wa Chama cha Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO), Anthony Machibya, huku akiungwa mkono na viongozi wenzake ambao jana walikutana kupanga mikakati ya kufanikisha maandamano yao leo.
Aliwataka wanafunzi na wananchi walio jirani na chuo hicho kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono pale watakapoandamana kudai haki zao. Wakati wanafunzi hao wakijiandaa kwa maandamano hayo, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limesema maandamano hayo ni batili na kuwataka viongozi hao wa wanafunzi wasijidanganye kufanya hivyo. “Sisi hatujiandai kwa ajili ya wanafunzi, sisi tuko tayari muda wote kuzuia uhalifu usitokee.
Kama wamesema wanaandamana wafanye hivyo kama wana kibali, vinginevyo watawajibika kwa kitakachotokea kwenye maandamano hayo,” alionya Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova. Kamanda Kova alisisitiza kuwa nchi lazima iendeshwe kwa kufuata sheria na kwamba hakuna mtu mwenye mamlaka ya kuamua anachotaka kufanya, hata kama kinapingana na sheria za nchi.
Kamanda Kova alisisitiza kuwaonya viongozi hao wa wanafunzi akisema kama hawana kibali, wasithubutu kuandamana kwani madhara ya kufanya hivyo wanayajua. Kutokana na matangazo ya chuo hicho, leo wananchi wa kawaida hawataruhusiwa kukanyaga ardhi ya Chuo Kikuu bila kuwa na kibali maalumu, ingawa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wataruhusiwa kuingia ili mradi tu wavae sare za shule zao. Hata hivyo, hadi jana mchana, mabasi yalikuwa yakiendelea kupitia katika eneo la Chuo Kikuu kama kawaida, tofauti na tangazo la chuo hicho lililotangaza kusitishwa kwa utaratibu wa kawaida wa usafiri hadi Januari 23, 2009.
Uongozi wa chuo hicho ulitangaza kuzifunga barabara zote zinazoingia katika chuo hicho ili kupisha usaili na udahili wa wanafunzi wanaorejea chuoni hapo kuanzia leo. Lango lililopo jirani na Chuo cha Maji lilitajwa kuwa litatumika kwa watu wanaoingia chuoni hapo tu na lile lililopo Chuo Kikuu cha Ardhi kuwa litatumiwa na wanaotoka. Wananchi watakaoathirika zaidi na zoezi hilo la siku tano ni wale wanaoishi maeneo hasa, Changanyikeni, Msewe na jeshini ambao njia zinazokwenda huko kupitia Chuo Kikuu zitafungwa. Godbless Charles, ambaye ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa MUHAS, alisema damu itakayomwagika ni ya wanyonge na ndiyo itakayotumika kuikomboa elimu ya juu ya kizazi kijacho. Charles ambaye pia ni Mwenyekiti wa UVEJUTA, alisema hawatanyamazishwa kwa milio ya bunduki, bali wataandamana kwa amani na kama ni vurugu zitaanzishwa na polisi walioandaliwa kuwazuia. Katibu wa Mtandao wa wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania (TSNP) ambaye pia ni Mbunge wa DARUSO, Owawa Stephen, aliwataka wanafunzi kuvaa nguo nyeusi au kufunga vitambaa vyeusi mikononi kuashiria msiba wa elimu ya juu nchini. “Hatutaingia chuoni kwa nguvu, tunachotaka ni haki yetu ya kudahiliwa, maandamano ni ya amani, wakitumia nguvu watupige tu, watawaua labda wawili na hata 10, lakini hatutasita kuidai haki yetu,” alisema huku akiungwa mkono na viongozi wenzake. Wakati wanafunzi hao wakiendelea na msimamo wao huo, menejimenti ya UDSM nayo imeendelea kushikilia msimamo wake wa kuwazuia wanafunzi walioshindwa kujaza fomu wasikanyage eneo la chuo ama sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Baadhi ya wakazi wanaoishi katika maeneo yanayozunguuka chuo hicho, ambao ili wafike ofisini kwao kwa urahisi, ni lazima wakanyage ardhi ya chuo, wameeleza kusikitishwa kwao na adhabu hiyo, ambayo walidai hawastahili. Jumaa Husein, mkazi wa Changanyikeni, alisema hali hiyo itawaathiri kwani watalazimika kuchelewa kazini kwa kuwa watalazimika kupita njia ndefu na mbovu. Madereva wa daladala zinazofanya safari zake Ubungo-Mwenge kupitia Chuo Kikuu, walisema hawajui wataishi vipi na familia zao katika kipindi cha siku hizo tano za kutopita chuoni hapo. Nacho Chama cha NCCR-Mageuzi kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kuhakikisha wanafunzi wote wanarejea chuoni na kuendelea na masomo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Samuel Ruhuza, alisema Serikali imeshindwa kuweka wazi vipaumbele vya taifa katika kuboresha huduma muhimu za jamii. “NCCR-Mageuzi haichukulii kuwa wanafunzi waliotimiza masharti ya kulipa ada kama walivyoelekezwa kuwa ni kigezo cha kuamini kwamba wazazi waoa wana uwezo wa kulipia gharama za elimu ya juu. “Kwa sababu hii, tunaitaka Serikali iachane mara moja na utumiaji wa sera yake mbovu ya uchangiaji wa gharama za elimu ya juu na mikopo, wale wote wenye uwezo wa kufika Chuo Kikuu waweze kupata kile walichokikusudia,” alisema Ruhuza.
Monday, January 19, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
22 comments:
TZ yawa gaza? Yaani inaonyesha wanafunzi wako radhi wafe kuliko kukosa udahili? Kuandamana ukiwa unajuwa utauliwa ni sawa na wanaojitoa muhanga kwa kuvaa mabomu. Acheni kujikatili maisha.
Kwani watu wasio na digrii mbona wanaishi tuu? Si bora muombe nafasi za masomo hata Tumaini au IFM? Ila msitoe roho zenu kwa ajili ya udahili. UDSM sio chuo pekee.
Au mnaona noma kupeleka wani zenu vyuo vingine?
Halafu na askari nao wako tayari kuuwa waandamanaji wasiouwa na watulivu ili mradi hawakuwapa kibali? Msijidai nyie mmebarikiwa kuuwa mtaenda jehanamu.
Rekebisha msemo wako "au mnaona noma kupeleka wani zenu vyuo vingine" hivyo vyuo vingine kuna wani pia za kumwaga tu...futa hako ka'kasumba kalikojengeka kuwa wani zinapatikana UDSM tu,kwanza una habari kuwa hata hapo UDSM kwenyewe III zipo? kama huna get hiyo!
By the way,tupeni taarifa ilikuwaje hiyo jana,mwenye taarifa atupatie hapa.
Ujue wanafunzi wengi hao wanaokurupuka hawajui nini maana ya STATE. Ujue kuna tofauti kati ya STATE na GOVERNMENT. Unapozungumzia mambo ya mikopo, sera ya elimu hapo unazungumzia GOVERNMENT, ila inapokuja suala la amani hapo ni STATE. Kwa sisi ambao tunafaham nini maana ya state, tunawashangaa hao vijana.State sifa yake kubwa huwa haionekani siku za kawaida, huwa inaonekana inapokuwa ktk operation zake za amani nk.Sasa fungua link hii uone State ilivyofanya http://www.globalpublisherstz.com/2009/01/19/chuo_kikuu_leo_noma_tupu.html#comment
Sasa unapokujan ktk masuala ya sheria...hawa vijana sio wanafunzi.Hivyo wanashitakiwa kama raia wa kawaidia, kwani wanafunzi wameshapewa vitambulisho vipya na udahili upya kabisa.Makosa yao ni pamoja na Traspacy, uchochezi na uvurugaji wa amani.Wasitumie kigezo eti wana haki ya kujieleza, wachukue mabango yao wabandike ktk nyumba zao watoe maelezo tuone nani atawafata huko.Unapokuja ktk eneo la chuo, ni eneo lingine hilo, unaiingilia state, pale unapozuiliwa.Sasa tuone nani mwenye hasara, kati yako na serikali.
Kitu kingine, huwa wanajifariji kuwa wako radhi kufa...nani yupo radhji kufa??Si walisema kipindi cha mgomo wakija FFU watagoma kuondoka, mbona walipotea ghafla??Sasa ngoja state iwaoneshe kuwa yenyewe ni nani.Mtu anayesema yupo radhi kufa, akimuona tu Auxiliary Police wa UDSM anatetemeka, je hao wenye ukame FFU wakiongozwa na Kamanda TOSI, wataona.Na wanapandishwa kizimbani waone sasa
Hakuna sehem iliyoandikwa kusoma chuo kikuu cha Umma wewe ni mtoto wa masikini...kusoma private universities kama Tumaini etc hakumaanishi wewe ni mtoto wa tajiri.Fanyeni analysis acheni ubaguzi na ulaza huo.Hapo DARUSO ilishafutwa, huyo anayejiita eti rais wa DARUSO au mbunge nani tena huyo.???Hiyo ni aibu kubwa wameipata kuona imekula kwao, wanataka kuonesha kuwa hawajashindwa...sasa kuvaa vitambaa vyeusi na maandamano ya amani unadhani ndio yatabadilisha maamuzi ya serikali??Fikirieni vijana, sio kukurupuka..hayo mambo ya amani mngefanya kipindi kabla hamjafanya mgomo, sasa vimewatokea mapuani ndio hivyo..
Mbona huyo Machibya na Owawa hawajaonekana kwenye hayo maandamano yao?Wanajifanya akina maalim Sefu, wanasema maandamano then wanakimbia, si unaona wao waliopandishwa ktk Defenda ya FFU, kanunue gazeti la Global Publisherz uone mambo..STATE OYEEEEEEEEEEEE.
Hilo gazeti la Publishers linapatikana wapi?
Ninavyoelewa mimi hakuna gazeti la Global Publishers,huo ni mtandao wa Bwn Shigongo na Crew yake ofcourse ume'cantain magazeti yake ya udaku na sidhani kama ni busara tuki'rely kwenye magazeti ya namna hiyo anyway ngoja na mimi nifungue nione.
By the way tunashukuru kwa taarifa U guys.
Habari,
I think a lot of students in Tanzania especially those at the Hill who calls themselves Vipanga have failed to see the wind of change in how the world is run and how the country is going today!!Ona sasa wanavyolialia!!The issue is this,kuna watu waliona dalili za mgomo tangu mwanzo ila hawakujishughulisha kuchukua hatua kutatua tatizo hilo.Cost sharing is innevitable!!Nothing will be a 100% in your life hata siku moja!!Tuko katika finacial crisis kubwa sana,mfumuko wa bei umecross 12%,siasa uchwara zinatafuna nchi,badala ya kufikiria jinsi ya kunusuru nchi mnayodhani mnaipenda,mnaongeza matatizo,tumieni dialogue,sijawahi kusikia au kusoma kwamba kiongozi wa wanafunzi amefuata procedure zote za kukutana na waziri au mkubwa yoyote akatimuliwa!!Tunajenga picha gani?Miaka ya 80,Tz haikuwa na job seekers kiwango tunachoona leo!!Mzumbe,Tumaini,Augustine,Dodoma,kuna utitiri wa vyuo,watu wanaoenda nje kusoma ndo si kidogo!!UDSM na wengine mnaojiita vipanga,upepo umebadili mwelekeo,if itatokea mrudi chuoni,tafakarini haya,msiporudi jifunzeni!!One day nitaandika makala ndefu hapa kuwapa reality kidogo ya hali halisi ya soko la ajira na mwelekeo wa elimu ya juu Tz muone mnavyopima kina cha maji ya mto kwa kidole!!
God Bless You
God Bless Our country,
Mdau-Tanzania
this is rediculous ,nonsense wanajua maana ya vita hao!!!
hali ya migomo ndo ilonifanya nisikutake udsm,hao viongozi wa daruso whatever u call them,they are all empty handed,halafu waseme wanaonewa damn fellows u a in danger.
tz ina system nzuri ya elimu kuliko kwengine kote duniani au kama nchi nyengine,hebu jaribuni kuchukua mifano kwa wenzetu walioendelea sio mkae kumwaga damu,africa siku zote wanaprefer kumwaga damu eti wananyimwa haki,
ukishakufa utaipata hiyo haki yako kaburini? au utapata moto kwa kujıdhulumu nafsi yako?!!
damn!! u better think about that,
nchi ngapi afrika zimeanzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa sababu za kipuuzi tz ina sifa ya utulivu wasitake kutuchafulia,watakaoandamana wakamatwe,wakawekwe gerezani kwavile weshapewa onyo!!!
hao ni wale walozoea vya bure na hata wakipewa hawatosheki...kudadeki!!
Good!
Hii ni ishara kuwa watu wamewachoka nyie mnaojiita Vipanga,mimi nafikiri kuwa Kipanga huku ukishindwa kuutumia U'kipanga huo katika kufikia malengo yako uliyojiwekea kwa faida yako,familia yako,ukoo wako na Taifa kwa ujumla hakuna faida,U rather be Non Kipanga.
U'pumbavu mtupu.
Anselemu na wenzanko acheni jilasi. Nyie kwa sababu siyo vipanga basi mnafurahia "aliye juu mngoje chini" au "mpanda ngazi hushuka", kwa nini na wewe usipande au uwe juu.
Kwa hiyo wasingegoma ungejuta kukosa point ya kuonyesha jilasi yako.
Anselm kinachokuuma ni kwamba hupati degree na unasoma chuo kidoo.
"Kwanini na mimi nisipande niwe juu" sijui juu gani unayoiongelea wewe,juu ya kugoma?
Siwezi kupanda juu ya namna hiyo,nilishasema na nitaendelea kusema kamwe siwezi kugoma kitaakhira,bahati nzuri mimi ni mtu mzima ninayeelewa thamani ya elimu moreover nasomea finance,economics ndani yake kwahiyo am very much aware of the financial crisis we are in na current inflation rate....nafikiri ufahamu wangu huu ndo unanifanya niamini kutowezekana kwa udhamini wa 100% kwa wahitaji wote,sasa kwanini nigome?
Anony wa Jan 22,8:31pm bahati mbaya sana si'aim Degree,naangalia mbele kabisa
Anselm, hu'aim degree bali equivalent, safi tuu. Lakini diploma yako itakuwa equivalent na digrii ya class gani?
Mbele si equivalent Anony,mbele ni mbele(Masters na kuendelea)...kwanini tuandikie mate na wino upo,tuombe uhai.
Diploma yangu ni sawa na Degree mkubwa,just know that these two things are equal.
Anselm, if they are equal why do they have to have different names.
kwanza niwasalimie wasomi wa humu!mm ni mgeni kidogo ktk swala la kutoa maoni ktk blog hii,ila nimfatiliaji mzuri sana wa hoja mbali mbali zinazotolewa na wasomi wa vyuo Tz na waliopo nje ya nchi
yetu! mm ni mwanafunzi wa mwk wa 3 ktk chuo cha uhasibu tazania TIA-Tanzania institute of accountancy, nachukua ADA,
Nimefuatilia hoja zenu za Adv dipl na degree kuhusu usawa wake!
kimsingi mm siamini kama ni kweli hv vitu viwili vinafanana ingawa kwa sababu fulani naweza kukubali kwa shingo upande.
kwa mfano graduates wa B.com (acct) ya pale UDSM na wa Adv dipl (acct) ya TIA na vyuo vingine vyenye mfumo km wetu tutaanza modules moja ktk paper za NBAA,Huo ni mfano mmojo tu lkn ipo mingi ya namna hiyo!
cha kunishangaza mm ambacho sielewi hata kwa nn ANSELM Asikubali kuwa ni kweli kabisa degree haiwezi kuwa sawa na Adv diploma ni nn?
mm kwa sasa nipo IFM nafanya PT,ambacho ndio chuo anacho soma kaka ANSELM,HAPA ifm kuna matangazo yamebandikwa na uongozi wa chuo kuwatoa ofu baadhi ya wanafunzi wa mwk wa kwanza waliodahiliwa ktk system ya shahada ambao NACTE imesema hawana sifa ya kupata hyo degree,wanafunzi wote hao watatakiwa kusoma kozi fupi and then wapate hzo sifa,KILICHONISHANGAZA NA KUHAMINI KUWA DEGREE NA ADV NI TOFAUTI NI PALE CHUO KILIPOSEMA KIMEWADAHILI WANAFUNZI HAO AMBAO NACTE WANASEMA HAWANA SIFA YA DEGREE KWA MTINDO WA ADV DIPLOMA,SASA USAWA HUO UPO WAPI? IKIWA SIFA ZINATOFAUTIANA?
kwakweli hapa tujiulize wadau wa Adv diploma!!!!
DIVisheni one zipo ktk vyuo vyote na si UDSM kama wachache wenye mawazo mgando wanavyosema!
kwa leo ni hivyo tu!
KIM, we naweza kufika mbali saana katika maisha yako maana unaonyesha unaangalia mambo katika jicho la uhalisia zaidi. Pia unaonyesha si shabiki bali ni mpiganaji.
Kuna kidogo umesahau kukitazama vizuri, je kuna uwezekano wa watu wenye wani kali (3-6 hivi) wakawa katika kozi za adv. diploma.
anony wa 7.48 pm, kwa kweli kukuta one hizo ktk Adv diploma ni nguma sana,huo ndio ukweli ktk vyuo vyetu hivi,
hilo halina ubishi kabisa!
Hii ndiyo mijadala ya wasomi! Tena wa elimu ya juu! Unataka kipi tena kujua kwamba elimu yetu inaelekea kaburini?
We materu, wacha iende kaburini, ni vilaza tu ndo watapata hasara. Ya vipanga itabaki duniani.
It is aѕ well connecteԁ to the ѕtellar physiсal structure itinегarу,
touch all the chakrаѕ that it finds.
Іn thаt reѕpeсt аre destіneԁ talked wіth manу
citizenry, from tantriс massage I grаduаtes
tο tantгic massage Masters, both tantric massаge coalition аnd non-tantric mаѕsage coalition.
creamy аnd cuddlesome Massage - manila papег ΡhilippinesWant to enjoy and gutеn
Rutsch ins Neue Jahr und freuе mich аuf ein baldiges Wiedersehen !
mechanics: GM's testament post be done.
Feel free to visit my web site ... web page
You Want your Fashion Design Present Wednesday nighttime, highlighting the ways in which styles at Hollywood's Halcyon ball Awards. http://kaspersuitsshop.com www.kaspersuitsshop.com [url=www.kaspersuitsshop.com/]kasper ladies suits[/url] [url=www.kaspersuitsshop.com]white suits for women[/url] [url=www.kaspersuitsshop.com/]kasper suits[/url] The Sex Pistols Hold reunited, so that you Get to Get told hoi polloi that multitude Reckon the Simpleness that's created an On-line Market for Self-governing fashion design. today fashion design is near recognised musical composition of jewelry. We real became a widefashion passim the Wintertime if you cast off out the new lede creative government agency. kasper suits kasper plus size suits kasper suits outlet And her Racecourse platter in building Illustrious UK fashion trade name holds a 75 per centum of U. There's latterly been called the reflexive, continuous fashion closing. some Technical school reviewers at the track during The Heart Truth 2013 fashion design Present hostess.
Post a Comment