Tuesday, January 20, 2009

SIDHANI KAMA WATASOMA VIZURI....SINA UHAKIKA!!

Salamu Wadau
Samahani kwanza kwa kutoonekana kwa muda mrefu wala kutopata updates kwa muda mrefu!!
Ila ninafahmu wengi wenu mnaelewa kilichokuwa kinaedelea na hamtanilaumu kwani nilikuwa katika kipindi kigum mdau wenu,kipindi hicho kigumu kimesababishwa na viongozi wa chuo changu na wanaharakati feki kwa kuanzaisha migomo wasiyojua itatupeleka wapi.....kwani mpaka leo hii ninavyoongea mdauu wenu jina langu halijatoka na sijasajiliwa na masharti yote nimetimiza ila kwa mbinde.....!!

Nimepitia uzoefu flani mgumu katika maisha yangu ya elimu,uzoefu wa kugombana na chuo na serikali....na mwishowe nime concede defeat kwani chuo na serikali ndio vimepata ushindi na wenzetu wengi bado wako nyumbani hawajui hatma yao!!mungu wasaidie kwa sababu sio kosa lao kosa ni la siasa ilivyoingia vyuoni na viongozi wa wanafunzi wabovu na wanaharakati feki wasiotumia hoja na usomi bali nguvu!!wanafunzi wapatao 2000 inasemekana wamefutiwa udahili japo bado sijaaminiamini vile,na wengineo masikini wasioweza kulipa ada bado wako nyumbani....laana kwa viongozi mlioandaa mgomo na wanaharakati feki,na nyie chama cha siasa cha CHADEMA muwe makini siku nyingine mkiandaa mgomo,mmetupotezea marafiki wengi,vita vyenu na CCM pelekeni nje ya chuo!!vyama vyote vya siasa tawala na msio tawala tuko chini ya miguu yenu msitupotezee muda wetu wa masomo kama ni haki zetu tunazijua na tutaidai wenyewe hatutaki mikono yenu!!

Swali langu ni kwamba fujo zote zilizofanyika na masharti magumu yaliyowekwa na chuo..je wanafunzi watasoma vizuri kweli....maanayake wengi wako affected psycologically.........hata hao endapo chuo kitakuwa na huruma ya kuwarudisha sidhani kama watakuwa kawaida...mungu tusaidie!1Nakuja kwenu chuo kikuu cha Dar Es Salaam....Salamu kwako proffesor mkandala...baba naomba uwarudishe marafiki zetu chuoni,wengi sio kosa lao wanakuwa punished kwa kitu ambacho hawajafanya,kosa ni la wanaharakati feki na wachochezi ambao mimi siwaungi mkono na niko tayari hao wapoteze chuo na sio hao 2000 wasio na hatia,na nina mifano ya baadhi yao ambao hawakugoma kabisa...lakini inaonyesha hawatarudi chuoni...ninaomba uwasamehe mkuu!!
ninaongea haya kwa uchungu sana na ntaongea tena post ijayo!!

waliotimiza masharti ndio hivyo tayari wanarudishwa na wameshapewa vitambulisho vipya na karibia wanaanza masomo!!...mungu wangu wasaidie waliobaki ba wasaidie waanzae masomo vizuri ili wasiathirike na uzoefu mgumu waliopitia....!!...na ninaomba wanafunzi wabishi mpunguze ubishi wenu na tusolve matatizo yetu kisomi!!

Asanteni,Mdau Wenu
William!!

13 comments:

Anonymous said...

we dogo fala sana.yaani watu tunaangaika tupate haki yetu we unatuita viongozi feki.Fala m kubwa we.

Anonymous said...

Pamoja mkuu, kuwapata viongozi ambao wana misimamo ya ukweli ni jambo zito, viongozi wengi wa serikali za wanafunzi ni wanafiki, wanatangaza migomo amboyo matokeo yake ni kama ulivyoona hapo UDSM hata huku UDOM viongozi pia ni feki, walianzisha mgomo wakatuweka juani lakini baada ya siku moja wenyewe wakausitisha bila hata matokeo tuliyotarajia. Migomo ni njia ya kudai haki, lakini kabla ya mgomo unapaswa kufikiria kwa mapana nini hatma yenu!!
James
College of informatics and virtual education
UDOM

Anonymous said...

matusi ya nini sasa mkuu....toa pointi tuone umesimama wapi na sio kutoa matusi,hayo ni mawazo ya mkuu na wewe toa yako tuone ukweli uko wapi!!

Anonymous said...

aliyeandika comment ya kwanza sidhani kama ni mwanafunzi wa chuo kikuu,hata kama wewe ni kiongozi unadai haki,kweli umethibitisha msemo wa nyakua ya kuwa nyie ni feki,mtu gani mwenye akili anatokwa na matusi mdomoni??
inaonyesha hapo UDSM hata kwenye migomo hampambanui na kuchambua hoja,bali mnatukanatukana tu
zinduka wewe usiye na akili za kupambanua hoja!!

Anonymous said...

Kama mwanafunzi wa Chuo Kikuu anaweza kuwa kama wewe basi hakuna mtu asiyeweza kuwa Chuo Kikuu katika nchi hii.

Tumekuwa tukilaumu mfumo wa elimu katika nchi hii na pengine wapo waliodhani hapakuwa na ushahidi wa wazi. Nadhani wakisoma kijiblogu hichi wataelewa tunazungumzia nini.

Kitendo cha kuandika vitu ambavyo kila mwenye akili timamu anashakia uwezo wako wa kufikiri ni udhahidi tosha kwamba wewe ni fala. Kumbuka fala sio tusi. Fala ni mtu mgonjwa kimawazo japo yeye anadhani ni mzima.

Kuwa Chuo Kikuu, maana yake ni kwamba unakuwa na uwezo wa kuchambua mambo kimantiki na sio kupayuka payuka kama unavyofanya wewe. Kuwa Chuo Kikuu maana yake si kuhitimisha kwa kutumia nguvu. Hitimisho linakuja kwa hoja zinazotegemeana.

Niseme mapema kabisa: Kama kweli wewe ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu, basi tuna tatizo kubwa mno la kimfumo.

Tatizo lenyewe ni la kuwa na wanafunzi wasioelimika na wasiotaka kuelimika. Wanafunzi wasiojua kinachoendelea hata baina ya wenzao. Wanafunzi wasioweza kuleta faida yoyote kwenye jamii hata ile ndogo inayowazunguka madarasani.

Umekuwa ukifanya kazi ya kuwashutumu wanafunzi wanaotetea maslahi ya vizazi vijavyo. Hujui kwamba serikali ya CCM ina fedha za kutosha kuwasomesha watoto wa wanyonge wa nchi hii. Ni kwa sababu tu kwamba fedha zote zinaishia kwenye mitandao yao ya kisiasa, eti wanadai hawawezi kutusomesha! Mwanafunzi wa Chuo Kikuu kipi usiyejua kuwa matumizi ya nguvu ni matokeo ya ubeuzi? Yaani kwako kutetea maslahi ya wengi maana yake ni kuwa CHADEMA? Ujinga uliopitiliza.

Na ni kwa sababu hujui wanachofanya wenzako ndio maana umebaki kujigamba kizembe zembe eti ile tu kuwa kwenye korido za Mlimani maana yake wewe ni kipanga kuliko wenzako wa vyuo vingine. Huu ni uzembe wa mawazo.

Umekuwa ukiendesha dharau dhidi ya wenzetu walio kwenye kozi za kati kama IFM. Eti wao ni vilaza. Kisa? Inawezekana hawakupata madaraja unayofikiri yanamaanisha kuwa na akili. Huu ni ujinga uliopitiliza.

Nimefuatilia komenti nyingi humu ni za kwako mwenyewe kwa majina tofauti. Maana yake ni nini? Una umwa kimawazo bwana mdogo.

Kuna mtu anakulipa kuandika utumbo humu ndani? Na kwa maslahi gani?

Narudia tena: Kama kweli tuko wote UDSM basi tumekwisha! Habari ndio hiyo.

Nakushauri kutulia baada ya kusoma mawazo haya. Nitafute ukipenda kwa ushauri zaidi.

Nimeandika hapa kukusaidia na kwa nia nzuri. Kila la heri.

Anonymous said...

huyu aliyetoa comment hapa juu anazidi kuwaaibisha watu wa UDSM...
inakuwaje jamaa ana mawzo finyu hivi??
mdau hebu mtafute huyu mtu mumuelekeze bwana,tunapoteza wasomi

Anonymous said...

Nilivyokuwa nikilalamikia uelewa wa baadhi ya wanafunzi wa UD watu waliniona namna gani vp,haya sasa wengine wanazidi kujitoza.
Ndo maana this year hamjatoa Mwakilishi hata mmoja kwenye mashindano ya Vyuo vikuu vya Africa Mashariki,eeh...wacha Tumaini na wapi sijui wakatuwakilishe,kama vichwa vyenyewe ndo kama hiki hapa juu,hamna kitu hapo ni afadhali Masters yangu nikaichukulia hapahapa IFM nisije kuathiriwa na uoto'asili bure.

Anonymous said...

We anselm huna uwezo wa kutathmini vipanga wako bali wao ndo wakutathmini wewe, kilaza.

Japo UD hawamo katika uwakilishi, si tatizo, angalia vilaza wakiwakilisha panakuwa nini.

We huna uwezo wa kupata mastazi UD kwani lazima ufanye PGD. Na kujidai kwako kuichukulia IFM unajuwa kabisa UD huendi hovyo, lazima uwe tested kwa PGD ambayo unaikwepa kujidai hutaki UD. Nani asiyetaka UD?

Anonymous said...

"Japo UD hawamo katika uwakilishi si tatizo"
Jamani wadau mnaichukuliaje hii kauli ya Anony wa Feb 19, 10:05?
Ninazidi kupata mashaka na cream yote iliyo UD kwa wakati huu,lkn No,nisi'generalise pengine ni hawa wanaoingia kwenye Blog yetu tu,kwa mtazamo wangu lazima kutakuwa na walakini somewhere kama si recruitment ya wanafunzi UD imekuwa ya kisanii nowdays basi wimbi la wizi ya mitihani ya Form VI litakuwa kubwa sana,watu wanafaulufaulu tu na kuingia UD pasipo kustahili,huwezi kuniambia eti UD kushiriki katika mchakato wa uwakilishi wa nchi na kushindwa hakuna tatizo,wakati huohuo huyo aliyeshindwa anajiita "kipanga"..kipanga wa nini sasa? kugoma?

Anonymous said...

Anse, Hawakuwepo katika ushiriki kwa sababu walikuwa wamefukuzwa.

Na suala la enrolimenti ya UD inaangalia divisheni. Ni kazi kuacha wenye I wachukuwe III, kwa kigezo kipi?

Jinsi gani unaweza kuthibitisha mtu mwenye III anfundishika masomo magumu kirahisi zaidi ya mwenye I?

Anonymous said...

Atleast wewe(Anony wa Feb 20) umeongea kitu ambacho angalau kinamaana lkn siyo yule Anony aliyesema kushindwa hakuna tatizo,kama ni kweli by the way.

Anonymous said...

Anse, nimekupiga bao. Mtowa mawazo uliyesema afadheali, na yule uliyesema hovyo, woote ni mtu mmoja, mimi, huwezi kuona treand au beat?

Anonymous said...

free nude [url=http://www.picturetrail.com/buntingnakedl] nude shoots[/url] Nude celebrity