Tuesday, January 6, 2009

VYUOTZ IS LIKE NON-ALIGNED MOVEMENT!!

Heri ya mwaka mpya wadau,

Ninaamini wote mko vizuri na tuko tayari kwa ajili ya kuukabili mwaka 2009,ninawashukuru sana kwa kuonyesha sapoti yenu na kuendelea kutoa maoni mbalimbali ni vipi tuiendeshe blog yetu na ipate kuwajumuisha wanafunzi wote wa vyuo ndani na nje ya nchi bila kusahau wale alumni!!
Ningependa kutoa msimamo wetu kuhusu migomo kwani kuna watu katika maoni yao wamesema eti tunatetea upande wa fulani na watu fulani tunawaponda ambacho ni kitu kisicho sahihi.......!!
Post hizo chini tuliweka kwa kutambua athari wanazopata wasiouhusika pindi pande mbili hizo za serikali na viongozi wa wanafunzi wanapohitilafiana.....!!
Nikianza na makosa yanayofanywa na serikali....Kwanza Serikali haiwasikilizi viongozi wa wanafunzi pindi wanapotumia njia za kidiplomasia na kuonyeshwa dharau ya hali ya ju......Pili sera yao mbovu ya uchangiaji wa gharama za elimu ya juu ambazio zinawakandamiza masikini na kuwanufaisha matajiri,kwani huwezi kumpima mtu uwezo wake kwa kutumia makaratasi...Tatu Viongozi wa nchi kutowatembelea wanafunzi vyuoni na kujua matatizo yao na kuwasikiliza katika public talks wala kutobadilishana nao mawazo,wana assume vitu maofisini na kuja na maamuzi mabaya,hasahasa wanapaogopa UDSM mle Nkurumah hall.....Nne na si mwisho...Kutoshirikisha wadau wakuu ambao ni wanafunzi katika utunzi wa sera zinazowaathiri na kuwadanganya kuwa wamefanya utafiti ambao hau apply kwa mazingira ya TZ......!!
Ukija upande wa viongozi wa wanafunzi.....Kwanza Wengi wao hawawezi kutatua matatizo ya wanafunzi na badala yake huyaleta kwa wanafunzi wenyewe wayatatue kwa njia ya migomo.....Pili Wengine hufanya mambo ili kutafuta umaarufu na si kusaidia wanafunzi ili wa gain populatrity itakoyowasaidi kufulfill political interests zao hapo baadaye....Tatu Viongozi wengine wanatumiwa na vyama vya siasa kuchafua chama kingine ili ku fullfill interst za hivyo vyama!! Nne...Wengi wanaoongoza migomo si wale wanaofanya kweli zile kazi za kufuatilia utatuzi wa matatizo ya wanafunzi....yaani hawajawahi kufanya hizo diplomasia wala kufuatilia peacefull....wale ambao wanafuatilia unakuta wanashangaa tu migomo imekwishaanza!!
Hatupingi migomo ila athari zake ndio zinawaumiza wanafunzi ambao wanafukuzwa vyuoni na kurudi vijijini na vilevile kupoteza muda na kufanya vitu ambavyo havikutarajiwa...migomo ni mizuri pale unapofanya demonstration zisizo na athari kubwa kwa majority....si lazima tugoooome mpaka vyuo vifungwe hizo pande mbili zinafaidika lakini wanafunzi wengi innocent wanapata shida....!!
Hivyo kwa mwaka huu 2009 viongozi wa wanafunzi na serikali kuweni makini ili msisababishe athari kubwa kama zilizotokea mwaka 2008!!
Asanteni wadau na endeleeni kuisapoti blog kwa hali na mali!!

26 comments:

Anonymous said...

Hivi mnaacha jukumu la blog manataka ku-assume leading group na kutafuat support?

Nyinyi kama ni blogers wekeni mambo safi watu matapata.

Mbona mnajisafisha mna walakini nini?

Anonymous said...

Walakini wa nini wewe?
Hakuna anayejisafisha hapa,watu wanaongea vitu vya msingi wewe unaona wanaongea lending activities,kuna mtu amekuambia hii ni SACCOS?
Kwanza umetokea wapi wewe? unasoma?
Wewe unafikiri kugoma ni deal,hivi ungekuwa na Dada yako yuko UDSM pale ambaye ulikuwa unamtegemea akipokea boom lake akumegee kidogo na wewe,kisha akajiingiza katika mambo ya ajabuajabu kama yalivyokuwa yaki'reportiwa na vyombo vya habari mbalimbali ksbb ya kusimamishwa nafikiri ndo ungejua tunavyosema migomo ina athari tunamaanisha nini.
Big up VYUOTZ,mwendo mdundo am now working on my budget and see if I can support you kwa hali na mali.

Anonymous said...

Anselm, nina dada yangu hakupata point za kwenda UD, sasa yuko IFM, kila jioni huripoti pale OHIO mtaani, na ananilipia karo. Kila mtu mtaani kwetu anajuwa.

Egidio Ndabagoye said...

Kama wadau mnaonaje tatizo hili la migomo vyuoni.Nini kifanyike?

Tupunguze vijembe vya Division 1 na matambo ya UDSM na IFM.

Anonymous said...

Anony wa Jan 7 huyo Dada yako hata hiyo admission ya IFM atakuwa kaipata kwa kuvua chupi pia,kwani yuko mwaka wa ngapi ksbb labda aendelee kuvua chupi kila end of semister ksbb akileta ubishi tu ataishia semister fulani,manake pale hakuna longolongo la muda mrefu

Anonymous said...

"Hatupingi migomo ila athari zake ndio zinawaumiza wanafunzi"

Mnataka Migomo isiyo na athari?!

"Hivi ungekuwa na Dada yako yuko UDSM pale ambaye ulikuwa unamtegemea akipokea boom lake akumegee kidogo na wewe"

Hilo boom mnafikiri serikali ingewapa ikiwa wenzenu waliowatangulia wangefanya migomo isiyi na athari?

Wanafunzi wa vyuo vikuu wa sasa mnanyimwa hakizenu hata mkigoma kwa sababu zifuatazo.

1. Mnagoma bila malengo maalumu na yanayotekelezeka

2. Mna migomo ya vurugu yenye kuharibu mali na kuathiri watu wasiohusika. kwa mfano kuvamia swimming pool, kupiga vioo vya magari, kuvaimia baa nakuiba pombe, kuteka barabara n.k

3. Mmepoteza heshima ya vyuo kwa kutatua matatizo yenu ya kifedha na kijamii kwa njia zisizo za kisomi kwa mfano ukahaba.

4. Kuingiza taasisi zenu kwenye mambo ya kimtaani kama urembo n.k, na hata hivyo kutofanya vizuri hata mkishindana na wasio na shule huko mitaani. Miss university, Mr. University nk. Sioni sababu ya kutumia jina kama University au higher learning institution kwenye mambo ya urembo. of course mabinti wanaotaka kufanya urembo wangeweza kufanya hivyo bila kuhusisha taasisi za taaluma. Mengine ni kama ukisikiliza radio unakuta wanafunzi wa vyuo wakitumiana salaam za mapenzi na mambo ya ajabu, wakichangia hoja zisizo na msing na mambo yasiyohusiana na taaluma huku wakijinadi kuwa wao ni wasomi wa UDSM, IFM nk. Mambo haya yanapoteza sana heshima za vyuo na wasomi, hivyo kukosa support ya jamii.

5. Wasomi kutotoa mchango wa maana katika mataizo ya jamii na kuwa miongoni mwa watu wanaotumia nafasi zao kujinufaisha.

6. Wengine endelezeni list hii maana ni ndefu.

Tukumbuke tu kuwa serikali haiwaogopi wanafunzi, ila inaogopa wananchi. Kama migomo ya wanafunzi haita kuwa na hoja za msingi, na wanafunzi hawatakuwa na 'credibility' kwa wananchi, migomo itaendelea kuwa na hasara siku zote kwa sababu serikali haitakuwa na sababu ya kuwajibika.

pipi

Anonymous said...

Anselm,unamaanisha pale IFM kuna wanafunzi ambao hawana sifa lakini wapo mkwa sababu ya kuvua chupi?

Anonymous said...

................
7. Kumpiga mtoto wa Waziri gani sijui(kama walivyofanya huko Mkwawa) kisa eti Baba yake ni Kiongozi wa hii serikali inayowanyima boom la 100%
8. Ku'express mawazo ya kipumbavu kabisa mbele ya hadhira kupitia Media kama alivyofanya kiongozi wao mmoja alipochukuliwa na vituo kibao vya TV walipoanza tu kugoma akitangaza namnukuu "Tunagoma na hata tukifukuzwa tukirudi tutagoma tena,mpaka kieleweke"
By the way,mimi nasubiri wanaporudi hiyo keshokutwa nione kama watagoma tena,ksbb najua bado hakijaeleweka.
9. Kwenda kuwaharibia soko akina Dadapoa wa watu wasiokuwa na elimu yeyote kwa vingereza vyao vya ku'negotiate bei.
10. Kina Dada ku'concetrate na uboreshaji wa GPA kwa njia ya kuchojoa.
11. Kushindana kununua Ma'flat screen,Sonny Wega,Home theatre,Ma'frdge na mazagazaga mengine yasiyo ya ulazima kwenye Hostel zao kwa kutumia boom na hivyo kusababisha boom kutotosha.
12. Kugeuza Hostel zao Madanguro yasiyo na leseni rasmi ie Mabibo.
13. Ongezeko la utumiaji Madesa katika mitihani ya ngazi mbalimbali.
14.Kuigaiga mambo bila kupima madhara yake kama vilivyofanya vyuo vyote vishiriki vilipoiga sehemu ya Mlimani kugoma.
Mimi mmenishangaza sana...wewe umepitapita mzunguko mpaka ukaikwaa Diploma yako ya Education uka'apply Chuo ukachaguliwa MUCCE.
Siku ya ku'report 1st Yr umepanda Upendo Bus Service kuelekea Iringa uko wewe na begi lako tu,iweje sasa kusikia Mlimani wamegoma na wewe ugome,hivi kabla ya kusikia Washikaji wamegoma hamkujua kama boom dogo?
15. Kushuka kwa ufanisi wa kitaaluma Chuoni,mfano ni jinsi mlivyotutia aibu kwenye mashindano ya Vyuo vikuu yaliyokuwa yamendaliwa na ZAIN kipindi hicho CELTEL ambayo yalishirikisha Vyuo mbalimbali East Africa.
Kwakweli from there mimi ndo nilianza kudharau elimu inayotolewa na hichi Chuo chetu,inawezekana kweli kikawa kinachukua wanafunzi bright,wenyewe wanajiitaga vipanga lkn mfumo wake pale ukawa unachangia kushika kutu kwa akili za Vipanga wetu ksbb kwa uwakilishi ule hata Mpwa wangu(anaingia Form IV) alisikitika sana na kama wale ndo walikuwa ndo best of the best basi................,ngoja niishie hapa kwanza,nitakuja tena baadaye.

Egidio Ndabagoye said...

Salama kaka Anselm,
Ukiwa kama msomi wa elimu ya juu wanachuo wenzako wangetumia njia gani mbadala zaidi ya kugoma ambayo hawakuifanya?

Anonymous said...

Anselm alikuwa anapenda UDSM akakosa akenda kuchukua diploma IFM, ana chuki binafsi tuu huyu. Angalia hata point zake hazijenda shule.

Anonymous said...

Anselm kakubali kuna wasichana IFM wanavuzwa chupi.

Halafu kawadhalilisha walimu wake kwa tuhuma hizo.

Anonymous said...

Anselm, kama una vijicenti kasaidie yatima kuliko kugawa kwa watu waso na shida.

Anonymous said...

Anselm, nimefatilia uchangiaji wako wa hoja, naona tone yako iko/ni nzuri kama ya mheshimiwa AUGUSTINE LYATONGA MREMA. Wewe una future safi.

Anonymous said...

"Eti point hazijaenda shule",kuna mtu anaweza kupinga mambo niliyoainisha katika list kuanzia namba 7 mpaka 15 kuwa hayajafanywa na Wanafunzi wa UD na Vyuo vyake vishiriki? ajitokeze.

Anonymous said...

Kaka Ndabagoye,
Njia ambayo nahisi ingekuwa ni muafaka Vipanga wangu hawa(natumia Vipanga ksbb wao ndo wanalotumia kuji'define) wangeitumia katika kufatilia madai yao ilikuwa ni vikao,kwasababu bahati nzuri Serikali yao ya Daruso inaheshimika sana hapa nchini kwahiyo wana nafasi kubwa tu ya kujadiliana na Serikali katka taratibu eleweka za kisomi lkn si kama walivyofanya,sawa wangeweza kugoma lkn si kwa style waliyotumia.Kila mtu anafahamu katika taratibu zilizowekwa kwa Higher Learning Institution zote,wanafunzi wakigoma siku 3 mfululizo hakuna majadiliano,wanafukuzwa na watarudi tu kama watakubaliana na masharti yatakayowekwa,hili liko wazi na Daruso pamoja na Vipanga wetu wote wanalifahamu hili,ninachoshindwa kuelewa kwanini hawakuchukua tahadhari?
Hivi wamegoma siku ya 1,ya 2 wamelala kuamkia ya 3 wakifahamu kabisa ndo siku ya mwisho,still bado wakaendela kugoma,kwanini wasifukuzwe? wamefukuzwa sasa wanalialia mitaani hizi kweli ni akili au matope?
Ukisoma gazeti la Habari leo la leo,au ukipitia kwenye Ukurasa wangu binafsi http://hans4real.blogspot.com/ utaona Serikali imetangaza kurudishwa Chuoni kwa wanafunzi 3000 tu kati ya 9000 wa sehemu ya Mlimani hii inamaanisha ni theruthi 1 tu ndo wamekidhi masharti yaliyowekwa,kwahiyo kuna hatari ya Wanafunzi wengi sana kukosa kumalizia elimu yao waliyokwishaianza,sasa embu tujadiliane siyo kama wasomi tu,kama watu wazima...maisha haya ya sasa hivi unapata nafasi ya kuingia Chuo kikuu halafu unaleta michezo ya kuigiza,hivi unafikiri miaka inawasubiri,siku hazigandi kweli kama alivyoimba Lady Jaydee.
Shauri yenu,nyie kazaneni Anselm ana'jelous alikosa nafasi ya kuingia Chuo,Anselm anatoa hoja zisizoenda shule,mwenzenu kila tarehe 25 ya kila mwezi Account inaneemeka,tarehe 26 January hii naanza mitihania yangu ya mwisho wa Semister ya kwanza,nyie kipindi hicho ndo kwanza mtakuwa na wiki 1 toka mrudishwe Chuoni,haya!

Anonymous said...

Anselm,ebu tetea hoja ya kujiunga VILAZA hapo IFM kwa kuvua chupi!

Anonymous said...

KSB muulize yule Anony aliyesema Dada yake hakupata point za kuingia UD akaja IFM,yeye anaweza akakuelezea vizuri zaidi alifanikiwaje?
By the way umeshakwenda kuangalia jina lako?

Anonymous said...

Ama kweli Anselm atakuwa AGUSTINO LYATONGA MREMA.

Anonymous said...

You can call me whichever,but I wont stop telling you facts,embu kwanza tushughulikie urejeshwaji wenu Vyuoni,someni gazeti la Habarileo la leo au tembeleeni Blog ya Ulimwengu wangu http://hans4real.blogspot.com/ na muone majaaliwa yenu ya kurudi kumalizia elimu zenu,maana naona Moderator wetu analala.

Anonymous said...

Mrema (Anselm) unachekesha saana.

Anonymous said...

...natoka UDSM lakini siungi mkono migomo kabsaaaaaa...nasisitiza siungi mkono migomo,coz ni upumbavu tu wa viongozi wetu ndio unatufikisha tulipo......
asnante nanselm kwa kuonyesha nia ya kutuchangia ili harakati ziendeleee...nakushukuru na thadey wa dar es salaam kwa kutusapoti....tumeupata mchango kwenye bank account na email yako tumeiona na tushajibu.....!!
karibuni wadau wote tuendeleze hili jahazi...just contribute!!
mdau mkuu,
william

Anonymous said...

wewe anslem adv dip yako haipo duniani huku ulaya ukija nayo unaanza first year

Anonymous said...

anselm mbona kimya mkuu,tupe mada bwana!!
vipi unaionaje hali inavyoendelea UDSM, wengine wanaendelea na masomo,wengine wako nyumbani...
goddamn wanafunzi mnapoteza dira!!

Anonymous said...

Anonymous wa lini sijui
Siyo tunapoteza dira,wanapoteza dira sisi watumia busara kidogo kwa kutumia akili zetu za wastani tulikuwa tunaendelea na shule kama kawaida na ndo maana ulikuwa hunioni kijiweni nilikuwa napiga zangu final za semister ya kwanza,zimepita sasa tupo likizo tukikusanya nguvu kwa ajili ya ngwe ya mwisho kama unavyojua ngwe ya mwisho ndo ngwe ya kusawazishia GPA.

Anonymous said...

We mawani unasumbuliwa na tatizo la inferiority complex ndio maana kila comment hukomi kutukumbusha kuwa uko IFM.

Una arguement za kilaza laza kweli bwana mdogo.

Anonymous said...

Yes jamaa anaonyesha kuwa infiriority imo nyingi kifuani na kichwani. Maana kila siku yeye ni kuponda watu wenye div I walio UD na kusema IFM na Tumaini ndo vyuo vya wasomi.

Hajui UD ndo chuo kinachotambulika duniani kuliko hiyo female institute.

Huwezi kwenda juu kwa kumkandia aliye juu, tafuta ngazi.

Anselm, wenzako wote wenye diploma wako kimya kuhusu diploma kwa sababu wanajuwa ni cheti kidogo, wewe wakikuza.

Afterall, at the end, hata kama una GPA kubwa vipi, unakuwa degree equivalent wa "class pass negative"