Tuesday, March 31, 2009

UCHAGUZI UDOM WAPAMBA MOTO!!

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa Serikali ya wanafunzi wa Seriklai ya Chuo kIkuu cha Dodoma (UDOSO) Mh.Dennis Mungai ametangaza kuanza rasmi kwa zoezi la kampeni za Uchaguzi.Kampeni hizo zimezinduliwa leo,alhamisi Machi 19,2009 wakati wa semina elekezi kwa wagombea waliopitishwa kugombea nafasi mbalimbali.Katika semina hiyo,Mh.Mungai aliainisha umuhimu wa taratibu nzuri za kampeni na kutaka zoezi zima la kampeni kuwa huru na haki.

Vitu vya msingi alivyoelezea Mh.Mungai kama angalizo kwa wagombea hao ni pamoja na kuepuka kampeni za matusi,kuepusha rushwa katika kampeni,rushwa na kampeni za amani.vitu vingine ni kutoingiliana katika kampeni,kuzingatia maadili pamoja na namna ya kupeleka malalamiko kwa tume,ambapo alisisitiza kupelekwa kwa tume ya uchaguzi zikiwa katika maandishi tena ikiwa imesainiwa.

Katika semina hiyo kwa wagombea Mh.Mungai alitangaza kuanza rasmi kwa kampeni ambapo uchaguzi wa kwanza utafanyika Machi 25,2009 kwa wawakilishi wa skuli (School Representatives) na viongozi wa Makazi (Block leaders).Kwa wagombea wa Uraisi au Mwenyekiti katika ngazi ya Chuo pamoja na Skuli,kura zitapigwa Machi 27,2009 siku ya ijumaa.Akisisitizia kwa wagombea,Mh.Mungai amewaasa kutofanya kampeni chafu,hasa za matusi na kashfa.Alisema, “Tunaomba kampeni ziwe za amani na kunadi sera…………ukingundulika,tunaku-nulfy(tunakuondoa) katika kinyang’anyiro”.

Aidha Mh.Mungai aliwakumbusha kuwa kampeni zote zitakoma saa 4:00 usiku kwa kampeni za vyumbani.Siku ya jumamosi na jumapili Umoja wa wanafunzi wanahabari wa Udom (UDOJA) uliandaa mdahalo kwa wagombea wa nafasi za juuu mbele ya wanafunzi ambapo wagombea wote wa nafasi za juu walionesha umahiri na uwezo wao wa kujibu maswali.Mchakato unaandelea .


Selemani Tambwe(UDOM)

6 comments:

Anonymous said...

Napata mshangao kidogo kuhusu tangazo hili.Kwa umakini ukilisoma uchaguzi umefanyika 27 March,2009 siku ya Ijumaa (Ijumaa iliyopita).Na tangazo hili limetolewa leo 31 March,2009. Na bado unasema mchakato wa kampeni unaendelea...naomba uniweke sawa nikupate Mdau

Anselm said...

Lack of seriousness!
Asante Mdau kwa kutuhabarisha hilo

Anonymous said...

Anselem ungekuwa siriazi usingekuwa IFM.

Anonymous said...

Anselm uko siriaz ndio maana unasoma Diploma. Hongera

Anonymous said...

Bulogu imekufaaaaaaa

Anselm said...

Hee,kumbe watu bado wako na Anselm,poleni...mwenzenu nipo napigana kuweka sawa GPA yangu,msione kimya