Ilikuwa ni siku ya jumamosi tarehe 06 August nikiwa nimetoka kuona onyesho la muziki wa Joh Makini pale mabibo hostel,nikaamua kupitia chakula ili kidogo nipunguze njaa iliyokuwa imenielemea!!
Baada ya kuchukua chakula nikaanza kujikokota kuelekea chumbani kwangu huku mawazo ya kumaliza chuo na mustakabali wa maisha yangu vikiwa vimetawala kichwa changu......mara nikaona kundi la watu kama 20 mbele yangu wakiwa kama wameduwaa huku wakipiga kelele....nikahisi kuna tukio litakuwa limetokea.
Mara nikamsikia mmoja kati ya wale kadamnasi akisema masikini sijui kama yule dada atapona.......!!
Mara nikasikia kuwa kuna kijana amemchoma kisu na ameelekea mitaa ya ukutani tayari kwa kuruka ukuta....nikaona kweli hili jambo ni anuai...nikawahisha chakula chumbani na kurudi haraka eneo la tukio......nikakuta yule kijana akisulubiwa na watu wenye hasira kali....nikahisi ni kisu cha kawaida,basi nikaambiwa nikashuhudie damu ghorofa ya pili...nilipofika tu nikashika kichwa na kujiuliza amechinjwa ng`ombe au binadamu??
Mara nikasikia nyeti kutoka kwa rafiki kuwa dada Bertha hajafika hata Ubungo akawa amekata roho....(RIP)
Nilihuzunika sana na nikatamani nijue nini hasa mkasa wa mwanajamii mwenzetu wa chuo kikuu kufanya unyama huo??Wakati huo muuaji alikuwa katika zahanati ya hostel akiwa amepoteza fahamu huku wanajamii wakiomba wafunguliwe mlango wammalizie......!!
Ndipo nikapata nyeti kuwa......walikuwa ni wapenzi ila penzi lilikuwa limeingia hitilafu...na msichana akasema hamtaki tena bwana msiba kwani anakunywa pombe na kuvuta bangi....ndipo mkuu huyo alipoamua kufanya kitendo hicho cha kinyama.......ilikuwa nia majira ya 3:45 usiku ndipo aliposhika begi lake la kutorokea na kutumia kisu hicho kumchoma maeneo ya tumbo na moyo kwa zaidi ya mara tatu...nilipoangalia yale matonge ya damu na bwawa lile la damu ndipo nilposhindwa kutambua ni unyama wa namna gani.....hakupata nafasi ya kutoroka kwani tulimdhibiti ipasavyo na yuko jela kusubiri hukumu kali aka maximum sentence!!
Ndipo nilipoamnini kuwa kweli mapenzi yanaua.....na sumu ya penzi ukishairamba huponi hata kwa maziwa.
Watch out guys!!
REST IN PEACE SISTER BERTHA MWARABU.......!!
Thursday, June 11, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
8 comments:
li bulogu lafwa!!!!
hello... hapi blogging... have a nice day! just visiting here....
li bulogu lafwiile!!!
One post a year
JAMAA KASUP, HANA MUDA
Supp siyo mchezo,isikieni hivyohivyo kwa wenzenu
Anselemu una matani wewe. teh teh. Hata hivyo jamaa anasoma chuo kigumu.
Labda kaenda bize akirudi ataposti tuu, unaweza kukuta kasahu laptop yake.
na wewe anse umemaliza?
nimerudi..............twendeni kazi sasa!!
Hahahaaaa.....si nilimalizaga chuo jamani halafu kukawa hakuna succession plan
Post a Comment