Watalii wetu wapatao kumi ambao tuliwatuma huko Beijing China kutuwakilisha kwenye Olimpiki wapo njiani kurudi nyumbani bila medali yoyote wakati wenzetu Kenya wanarudi na medali za dhahabu tano,Nahisi watakuja na bidhaa walizonunua huko...Hebu soma habari hii kidogo.......
`KENYA kwa mara ya kwanza jana ilitwaa medali ya dhahabu katika mbio za marathon katika michezo ya Olimpiki, baada ya mwanariadha wake Sammy Wanjiru, kutimuka kwa saa 2:6:32, huku wanariadha wa Tanzania wakichemsha.
Katika mbio hizo, Tanzania iliwakilishwa na wanariadha watatu ambao ni Samson Ramadhani, Getul Bayo na Samweli Kwan’g, ambao jana walishindwa kuonyesha makali.
Tanzania katika michezo hiyo iliyofungwa rasmi jana, iliwakilishwa na wachezaji 10 katika mchezo wa riadha na kuogelea, ambao wote hawakuambulia chochote, hivyo kudhihirisha kuwa Tanzania ingali na safari ndefu katika medani ya kimataifa.
Licha ya hali ya joto, Wanjiru alifanikiwa kumaliza wa kwanza akimshinda Jaouad Gharib wa Morocco, aliyemaliza wa pili, akiwa nyuma kwa sekunde 84.
Wanjiru aliyekuwa miongoni mwa wanariadha waliokuwa wakiongoza tangu mwanzo wa mbio hizo, alifanikiwa kuongeza kasi zikiwa zimesalia kilomita chache kabla ya kufika mwisho.
Nafasi ya pili katika mbio hizo ilikwenda kwa Jaouad Gharib wa Morocco, alishinda medali ya fedha baada ya kuachwa nyuma na Wanjiru, huku Tsegay Kebede wa Ethiopia akinyakua shaba.`
Sasa sisi Watanzania tujivunie mchezo gani?..Je ni mchezo gani tukiwekeza tutafanya vizuri?..Au tutumie mbinu gani na sisi tufanikiwe michezoni?..Soka tumejaribu lakini nako bado kabisa?..Au watanzania tunaweza nini?Hongereni sana Wakenya..TOENI MAONI YENU WADAU ILI WAHUSIKA WAYAONE!!

9 comments:
Watanzania tutaendelea kuwa wa mwisho kwenye kila nyanja ya maisha.
Hii inajumuisha elimu,michezo,utajiri, n.k
Mimi nadhani hii ni kwa ajili ya kuingiza siasa kwenye kila kitu na kutokuwa na mipango ya muda mrefu,tumezoea kuzima moto.Si unaona hta wanafunzi wenyewe vyuoni hawasomi mpaka ikaribie mitihani kwa hiyo huo ndio uzimaji moto,na mashindano yakikaribia ndio timu huenda kambini basi kama ndio hivyo tutaendelea kufeli kwenye kila kitu,
ni hayo tu.
natumaini watalii wetu watarudi hom salama na hawatakamatwa na madawa ya kulevya huko china kama wale mabondia wetu........
si mnakumbuka wadau???
muhimu ni kuandaa viapaj .kuandaa watu wakiwa wadogo sio watu wameshakomaa wanawaza kutoka kimaisha unazani watafanikiwa?si mmeona vipaj vya china ni watoto kabisa wale lkn cheki mambo yao.angalia hata kwenye timu ya taifa mijitu mizima ile inawaza maisha tu na kufanikiwa na ndomaana hwazingatii .siku iz timu ya taifa imeboreshwa wanapewa pesa nzur wana kula vema na pata gudtimekambi wanaweka nje sana lkn wapi hakuna lolote zaid ya kututia aibu tu.wakenya wanafanya vema hata izi mech zinazoendelea wapo pazur lkn ss tayar tumetoka.cha msing waandaliwe watoto mapema sio watu wazima ambao akili yao ni staree na upuuzi.vichwa vishakomaa havifaham tena.la sivyo tukubali hali hii
Serikali haina uwezo wa kuandaa wachezaji wadogo ona inashindwa hata kuangalia yatima.
Serikali itamsaidia mtu aliyejiivisha mwenyewe kwa kumpa nauli kwenda kushiriki.
What have been said can never be unsaid!Naheshimu maoni yenu wadau wengine!Mlioyasema tayari mmeyasema!
Ila naomba sana tusiwaite watalii wawakilishi wetu wa olympic kwani kushindwa kwao si wao bali serikali haikuwandaa
Kilichofanyika ni kuwapa tiketi na posho kidogo sana na wala hakukuwa n a kambi za mazoezi.
Mabondia wetu wengi ni watumishi wa umma!Mtu huyohuyo atumikie umma then atafanya saa ngapi mazoezi y akutosha?
Kama Mkenya ambaye mke wangu atoka Tanzania, nawarudishieni ahsante kwa hongera. Kenya ilifanya vizuri kwa Olimpiki na Africa nzima imefurahia. Watu weusi hoyee!
Tusiwalaumu hawa watu tunaowatuma. Kwanza tujiulize ni maandalizi gani tunawapaga? na ni kwa muda gani.
Wenzetu wanaenda kambini miaka hata minne. Siye kambi ya miezi kadhaa itatusaidia nini?
Tatizo sio watu wanaoingia kwenye michezo hiyo tatizo ni uwezo wetu wakuwatrain hawa watu
MBONA HUJAWAAMBIA WATU HUYU MKIMBIAJI WA KENYA ALIYESHINDA GOLD ALIKUWA JAPANI ANAFANYA TRAINING YAKE HUKO NA ALIKUA NA COACH WAKE KWA ZAIDI YA MWAKA MZIMA...???????
umitashunta zimeishia wapi? wizara ya michezo inafanya nini? Kwenye bajeti inapewa asilimia ngapi? Hizo hela zinatumikaje?
Hayo ni baadhi ya maswali inayobidi tujiulize. Ni aibu sana kila siku kurudi na kapu tu! Mara ya mwisho kushinda medali ni enzi za Bayo 1980. Kweli inabidi tukuze michezo zaidi. tunahitaji kubinafsishwa kwa sekta ya michezo...maana ikiendelea serikalini ni ufisadi tu!
mimi na thani watanzania wanafaa kufanya kazi bila ubaguzi wa dini. pia wakuwe active.
Post a Comment