Wednesday, August 20, 2008

SALAMU KUTOKA ALGERIA!!

Wanafunzi wa kitanzania wanaosoma algeria wanawasalimia wanafunzi wote mliopo nyumbani Tanzania na wengine wote mliopo nje ya nchi...Wanasema wamewamiss sana lakini tutakua nao pamoja muda si mrefu.....
nilipata salamu zao na nategemea watatumia picha zao kupitia email yetu na tutaipost na majina ya vyuo vyao na majina yao pia... We wish you all the best there!!
Halafu mdau wa New York,ulikuwa unaomba specialization nyingine za Bcom apart from Accounting...ni Corporate Finance,Banking Finance,Marketing,Human resources,Management Science na International business..Ila kwa UDSM zinafanyiwa review..International business na Management science hazitakuwepo tena...Kwa University of Dodoma ntafuatilia kuhusu hizo mbili kama zipo au lah!!
Halafu kuna argument nimetumiwa kuwa DIT inatoa maengeneer bora Tanzania kuliko sehemu yoyote hata COET ya UDSM haifiki... ni kweli??...Kwanini isiwe COET iwe DIT??,,, Mimi sihusiki ngojea tusikie maoni ya watu!!
Ntafuatilia halafu ntaileta hii discussion mezani ikiwa clear..ila anzeni kwanza kutoa comments zenu hapa chini!!

9 comments:

Anonymous said...

Engineering inahusisha mengi sana. Sio tu kushika spana sana au kusoma sana(kukata nyanga) ndio Engineering. Ila combination ya kushika spana, surveying iliyoenda shule, programming ya kutosha etc na nyanga(kuwa na uwezo wa kuelewa) na kuwa creative ndio vinajenga engineer.
Hata Europe kuna polytechnics kama DIT na wanakuwa wazuri kwenye kazi haswa, lakini hii inabaki kuwa kazi ya technician. Engineer inabidi ajua tatizo, aweze kucreate solution na aiweke ile solution. Sasa kutoka hapo technicians na wengine ndio wanakuja kwenye kuiweka into action(spana kamili).

By the way Engineer bora ni mwenye combination, anayejua spana na mwenye uwezo wa kufikiri na kutengeneza suluhisho la tatizo.

Anonymous said...

Unajuwa tangu zamani kabala haijaanza kutoa degree, DIT ilitoa ADE na hao ADE wamekuwa wakidai kuwa ni wahandisi lakini hawakukubaliwa na bodi ya wahandisi kuwa wahandisi bali fundi-handisi (technician engineer). BSc. walikuwa na free ride kwenye board kwa sababu programu yao ni universal. Bado watu walikuwa wakisema ADE ni wazuri kuliko BSc na sababu zaidi ni kwamba Bsc walihitaji mishahara mikubwa based on their value. Hata hii degree ya DIT (BENG) ni inferior bado, BENG duniani kote huwa iko chini ya BSc. Eng na kuna vyo vinatoa zote mbili kwa wakati mmoja.

Hata wale waendao DIT huwa hawapati admission UDSM, kwa hiyo ni reject.

Pia nakubali ADE wanaweza kazi ya mikono kuliko BSc., sawa na ma-nurse wanvyofunga vidonda vizuri zaidi ya Daktari. Si kazi ya mhandisi kusimamia umwagaji wa zege na vibarua au utandazaji wa nyaya, hiyo ni ya DIT (FTC, ADE na BENG).

Na ukitaka kuona kuwa ubora wa DIT ni uzushi, angalia waajiri wanasema VETA ni bora kuliko DIT.

Bsc ni viongozi, ni wanasayansi, na ni watafiti. We chukua prospectus zao usome silabasi ndo utajuwa nani mzuri zaidi.

Ila bado nakubali ili tuendelee tunahitaji wataalamu wa juu(COE), wa kati (DIT) na wachini (VETA).

UDSM iko chini kwenye theology na divinity tuu, Vingine nobody beats it. UDSM is it!!!!

Anonymous said...

Lakini kwa nini wanafunzi wanoenda DIT hawana pass marks nzuri kama wa COE?

Anonymous said...

Thanks William for your good answer..Kumbe International Business inatolewa pia vyuo vya Dar?I didn't know that!Na mtu anae-specialize kwenye field hii anapossibilities za kufanya kazi gani coz I wanned to take International Business from one of the colleges here in New York but wasn't sure of its marketability back in Bongo..We uko BCom mwaka wa ngapi nataka nikupe salamu kwa wale niwajuao waliopo mwaka wa pili.

Hongera,this is the nice blog,keep it up buddy.Salamu Tanzania.

Mdau New York.

Anonymous said...

akili ya kuvunja/kugeuza mada, umeguswa?

Anonymous said...

UDSM will always be underated for all fields of study: arts, laws, education, science, engineering, sociology etc.

Chuo cha kizamani na kina mambo ya kizamani.

Kiko ukingoni kuzikwa. Kipe miaka 10 hivi, labda kilindwe na sirikali.

Anonymous said...

billijax usipime ma engineer wa udsm noma, hiyo wakubali, digrii ya mikiki na soup kunywa nje nje kwa hiyo watu wako makini.blog yako inatisha big up papaa

Anonymous said...

Saana tuu! We ukipita salama UDSM utaishi salama sehemu zoote duniani. Maana wanajeshi waliopitia Monduli kadeti wakija wanakubali wenyewe.

Anonymous said...

Naked celeb [url=http://www.123video.nl/members/gebruiker.asp?MemberID=9830106&Name=Nudecelebrities&CU=0] naked pictures[/url] Nakedcelebrity