Hello there again!!! students of the Institute of Finance Management i hope you are doing well enough with your holiday right hommies?.On 23rd september 2008 i received a text from the minister of education of IFMSO saying `Ndugu wanafunzi wenzangu wa IFM nikiwa kama waziri wa elimu wa IFMSO ninaomba ushirikiano wenu kwenye maandamano yatakayofanyika chuo kitakapofunguliwa hapo mwezi wa kumi` ujumbe mkubwa uliobeba message hiyo ni `kwa nini tusipewe Degree wote?, ikiwa wanafunzi waliodahiliwa mwaka huu kuanza mwaka wa kwanza chuoni hapa wanachukua Degree!!!!!!.ujumbe huo uliendelea kuwaomba wanafunzi wote wa IFM kuonyesha ushirikiano wa kutosha katika suala hilo kwani bila ushirikiano wao jambo hilo haliwezi kufanikiwa!!!!!! swali kubwa katika mchakato huu ni je inawezekana?? hakika jibu la swali hili lipo mikononi mwa wadau wote wa chuo hicho maalufu cha usimamizi wa masuala ya fedha hapa nchini, Management ya chuo ikiongozwa na professor Doliye mna kazi kubwa kutufanikishia suala hili,wanafunzi wenyewe you do have a great role to play!!.wanafunzi wa IFM uwanja ni wenu katika suala hilo wenzenu wa ustawi wa jamii wameshaanza mapemaa!!!.
francis philip,
Institute of finance management.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
31 comments:
Jamani imekuwaje tena, si huwa mnasema advance diploma ni sawa na degree (kizio) mwataka nini tena?
Hii ndo inaonyesha hata IFM si sawa na UD wala SUA.
Nachokubali tu ni kwamba IFM japo ni advance diploma, lakini zina nguvu zaidi ya degree za tumaini na wengine kama hao maana si unajuwa watu wanaingia na EE tuu.
kuandamana is not solution.
im not agree with this
Mshikaji wa sep 23, tatizo siyo jina la Advanced diploma mkubwa!!!,tatizo ni mabadiliko yakukurupuka yasiyo na mipango ya muda mrefu ambayo wadau wa elimu ya juu wanayafanya!!!,kumwambia mtu kuwa Advanced diploma tunaifuta katika kipindi cha mwaka mmoja tuu bila taarifa yoyote ile ya awali na hasa katika ushindani huu mkubwa wa soko la ajila mjini hapa ni kukosa nidhamu katika taaruma ya watu, siyo kwamba hatutaki mabadiliko hapana!!!,mabadiliko yafanywe katika mpangilio ambao kila mtu ataukubali.tunaangalia mbali mjomba siyo kwamba tunakurupuka tuu.
lakini wakati mwingine huwa nashangaa sana tabia iliyo jengeka miongoni wa watanzania kwamba kila jambo basi suluhu yake ni kugoma na kuandamana.
hebu fikiria kiurahisi tu. ulipochukuwa fomu ya kujiunga na ulipo fanya application zako uliomba kusajiriwa ktk mafunzo ya advanced diploma. sasa leo hii chuo kinaanza mfumo mpya na mkataba mpya na watu wapya wewe unaandamana inakuwa imekaaje?inaeleweka wazi kwamba ili degree iitwe ni degree kunavitu vinahitajika.ambavyo ktk advanced diploma huwa haviwekwi kwakuwa A.D inalenga kutoa watu waliobobea ktk utaalam wa fani ya utendaji tu na sio na mambo mengine ya ziada ambayo degree inaweza kutumika ku cover mathalani vitu kama kuwa kiraka ktk eneo fulani.
sipingi watuhawa kupenda wapewe degree lakini sikubaliani na huu utaratibu wa kugoma na kuandamana na kwa kila jamba.kama msomi lazima ukubali kuheshimu mikataba unayo ingia. kwanza AD ktk nchizingine haipo kabisa wala haitambuliki,sasa kwanini basi uliiomba kama unajuwa kabisa soko lake sio ktk level ya dunia,ulikjuwa kabisa uko limited ktk baadhi ya nchi tu.
nawashauri tu wamalize then waaombe hizo masters kama wanaruhusiwa kuzifanya,maana ktk university nyingi za nje hicho kitu cha AD hawakijui wala hata master wahatakupeni kufanya.siyo kosa la chuo kabisa,wewe chukuwa ulichoomba na ukapewa ukasoma,waache wapya wapate degree!
samahani kama nitakuwa nimewagusa ,japo nafahamu muda unaotumia chuoni ni muhimu lakini pia ustaarabu wa kisomi nimuhimu ufuatwe kuheshimu sahihi yako uliyo saini kwa hiari na ufahamu.
kama mngetaka degree toka mwanzo si mngekuja udsm,mzumbe,sua n.k?We mwenyewe ulijaza fomu kuomba advanceed diploma and u complied to all regulations and requirements.leo ugomee mkataba uliosaini mwenyewe na udahili ulioukubali mwenyewe.hamuoni kua mnakua mnaonekana vilaza wakati mimi naamini kabisa akili za kutumia mnazo?
mnaotaka degree anzeni upya mwaka wa kwanza,(fresh from the begining).its acceptable, and at the end u'll all get ur degrees.if u applied for advanced diploma how comes ur claiming for a degree? does it make sense??
Jibu liko rahisi, walipata admisheni ya AD ni kwa sababu walikosa za digree UD, SUA, na MZ. Waliamua kwenda IFM na kuacha TUMAINI kwa sababu digrii za TUMA na wenzake zimechoka bora AD ya IFM.
Hawakupenda AD bali hali iliwalazimu kutokana na pass zao za A-levo.
Jamani waambieni vijana wa sekondari wasome saana yasije wakuta haya. Ohooooo
Acheni mambo ya kusema degree za Tumaini hazina maana ukilinganisha na ADA ya IFM.
IFM imekuwepo miaka miongo mingi kabla ya Tumaini hivyo watu wengi bado wanaona ADA ya muhimu. lakini sasa katika ushindani ndo hapo sasa degree inaonekana ina umuhimu wake.
Tutakwenda na itafikia hatua kwamba hata Degree za IFM zitakuwa hazina maana kama jina la IFM litabaki hivyo hivyo bila kuitwa university.
Ni mambo ya wakati tu.
Nani alijua kwamba itafikia hatua kwamba degree ya chuo chochote kutoka nje itakuwa na jina kubwa katika soko la ajira TZ zaidi ya degree ya UDSM.
Makubwa, tuliyataka wenyewe na tuende nayo vile vile.
Digrii za Tuma zingekuwa na maana watu wasingeenda IFM. Na IFM ikisha anza toa degree hadhi yake itakuwa exponentially kama vile mzumbe, ardhi na muhimbili. Vyoote hivi ni vichanga kwa umri kuliko tumaini lakini vina human resources za nguvu (ma PhD).
Tumaini na wenzake tatizo lao ni human resources, hawana walimu kabisa. We tembelea website zao halafu linganisha na UD au SUA au Mzumbe au IFM.
Mi nashangaa hata watu kwanini bado wanasoma huko Tumaini na Augustini.
We annon wa mwisho hata hujui unachoandika. Humana Resources ina uhusiano gani na chuo. Ukimaanisha kwamba HR ni walimu basi inabidi ukarudi IFM kusoma vizuri.
Uelewe Chuo kama chuo kikuu ni cha serikali na State au Federal university zote dunia nzima zina taratibu zinazofanana. Yaani kufundisha kwa ajili ya kupata watu wakafundishe tena.
Na vyuo vingine vya private mara zote huwa na idadi ya walimu wenye PHD wanaotakiwa kwa ajili ya kuwa na chuo kikuu , halafu ma-tutorial assistant,Assistant lecturers au Part time professors. Ambao huwa na Masters degree tu lakini wenye uzoefu wa kazi na sio uzoefu wa elimu.
Walimu Tumani au St- augustine wengi utakuta ni mameneja Benki, ma-laywer, wahasibu katika makampuni na wanafundisha kwa uzoefu wa kufanyia kazi.Yaani vitu utakavyovikuta kazini kwa maaana wao wao kazini.
wakati walimu wengi wa chuokikuu dar, Sua Nk wao kazi yao ni kufundisha tu na hawana cheo au kazi yeyotee mtaani. Hivyo wanaonekana wakali lakini hawajui whats going on outside, or at work place.
Uelewe IFM ina kozi za biashara au zinazoendana na biashara na zaidi ya hilo hakuna zaidi. Vyuo kama IFM vingekuwa nje ya mchi vingekuwa na programs zaidi ya 40, ila kikubwa vinajulikana kwamba ni wakali wa uhasibu. Ni sawa na St-augustine wana programs nyingi lakini wanajulikana ni wakali wa Uandishi wa habari, sawa na Tumaini Sheria kwa sasa, NK.
Badilika maana sasa utakuta vyuo vikuu kibao nje vina branch hadi high-school na heshima iko pale pale. Hata nyinyi Chuo kikuu Dar mnaweza tumia madarasa ya Shule ya msingi mlimani, iliyo hapo jirani kati ya saa 12 jioni hadi saa nne usiku na bado mkawa mko chuo.
Nyinyi mnaangalia sana Mabweni, Madarasa, majengo ya CHUO TU na sio masaa ya kusoma masomo,uchaguaji wa masomo, na ubora wa hayo madarasa.
kama mtu hujachugua major , masomo yaliyobaki unaweza soma saa yoyote au muda wowote au semester yoyote na sio kulifanya liwe semester fulani tu, wakati mtu hata Progrma hajaanza.
Kujiita uko BBA mwaka wa kwanza huku unasoma vitu ambavyo sio Core ya BBA kwa miaka karibu miwili haileti maana.
Angalia sana kuleta dharau katika wasomi wenzako maana huo ni ulimbukeni wakati nyote ni wasomi na mna degree ambazo mtazitumia wote kusoma Masters.
Holder wa Degree zote za kwanza, ziwe za Tumaini, St-Augustine, nk wakitaka kujiunga na Masters UDSM wanakubaliwa. Sasa hiyo sentesi ya kwamba za UDSM ni kali kuzidi za Tumaini zinaonyesha utoto na ujinga wa akili.
kama kuna mtu alikuwa na E ,E, C na bado akaingia Tumaini, na hata kama walimu sio wengi na akamaliza na kupata Degree ya BBA hapo Tumaini haimzui kusoma MBA UDSM.hapo ndo ulewe degree zote sawa, zingekuwa sio sawa basi wangezuiliwa kusoma UDSM masters zao.
Kutokusoma UDSM first degree hakukufanyi wewe degree yako kuwa ndogo au finyu.
Zote ni degree tu.
Ila tatizo linakuja kwa Advanced Diploma, na ndio maana lazima usome Post graduate ili uingie MBA udsm.
yeah kama mnataka degree anza first year.hamna kugoma wala nini?chuo ndo kimeamua so nothing can change that.dont waste ur time,instead fight how u gonna get that admission for degree by applying again.
acheni tabia ya migomo haipendezi mnatia ila mbaya vyuo tz.
We kama unatetea uzuri wa chuo kwa kutokuwa na walimu ma-Ph basi hujui elimu ni nini, degree sio vocation education. We vyuo vina ma-TA tuu ndo unasema vyuo.
Eti Tuma wanaongoza kwa laws, niambie mwalimu hata mmoja gangwe wa laws tumaini anayeweza kuwafukuzia akina mvungi, shivji, au hata wa zamani lamwai. Wanafunzi wenyewe substandard.
Mi naona hao jamaa hata wakiomba tena IFM degree program inaweza kuwa ngumu admisheni kwa sababu vigezo vya kuadmiti degree vinaweza kuwa juu. Fikirieni Tumaini na Agustino.
Washaurini vijana wa seco wasome saana
anyway sijui ni kwanini mnawaita wanavyuo wenzenu eti ni sub standard. kwa sababu mtihani wa A-level unaweza ukakupaalia na usipate grade nzuri kutokana na sababu mbalimbali,ila haimaanishi kwamba ulikuwa ni mchovu tangu awali.
mfano ni mimi mwenyewe,nilikuwa fit sana class A-level,na nilikuwa nawakimbiza mkachakamchaka wenzangu na company yangu yote ilikuwa gado. lakini ktk mtihani wa mwisho nilikuwa ktk halimbaya kifikra kutokana na matatizo ya kifamilia,na sikufanya vizuri kabisa maana nili pata div TWO 12.
kwakuwa kozi niliyoitaka ilikuwa na ushindani mkubwa na NECTA ndiye alikuwa muamuzi basi niliachwa hewani.bila kupoteza muda nikaingia kufanya diploma,kisha kuna vijana walikuwa wamemaliza ktk special school kamamjuavyo na point zao 3 wengine 4, wakaingia university direct,lakini baadaye wakabadili mawazo ikabidi tukutane ktk anga zingine tena wote tukisaka nondo ktk fani ile tuliyo kusudia tangu awali.
lakini safari hii mimi sikuona zile AAA,AAB walizo tokanazo A-level zikiendeleza makali yake. maana ni uwanja tofauti,gemu tofauti na refa tofauti, sasa matokeo yake mimi na zile pt 12 zangu,japo na diploma lakini siyo ya fani tunayosomea sasa ,ila muda wote tangu tuanze mzigo hadi leo hii sikuzote wananivuta shati kwa nyuma tu.kwa ufupi mtihani wa A-level sio kipimo cha kuwa wewe ni mchovu na utaendelea kuchoka siku zote!!!
wewe sina uhakika ila nadhani ni muongo, yaani mtu wa 1.3 anavyojuwa nondoz aishe kiwango mpaka kufundishwa na mtu wa kidogo div 3? Labda hizo A 3, 2 zilikuwa za masomo ya dini huko seminari.
Wewe anon wa September 25, 2008 3:51 AM, usilete za kuleta. Kwanza hizo degree daraja la pili usiziguse kabisa.
Hao jamaa zako wa Tuma watang'ang'ania kuchukua mastaz UD ili wapande kiwango tuu, mbona wasichukulie hiyo mastaz huko tumaini? Na mbona hatuoni watu waliomaliza UD wakichukulia mastaz tumaini?
Utasema tuma hamna mastaz, tutasubiri tuu tuone.
We jamaa umepitwa na wakati. Tumaini wanayo mastaz MBA programu lakini wahitimu wao wa BBA wanapenda UD ili kufukia udhaifu.
Sasa kama walishindwa kukubaliwa wakati wana score ndogo A level kuja chuo UD mwaka wa kwanza, iweje degree zao za kwanza za Tumaini unazosema ni mbofu mbofu zikakubalika kusoma na watu waliokuwa na degree kali kali wote masters hapa UD.
Kwa lugha fupi basi basi zote degreeza kwanza za Tuma na UD ni sawa tu, ni sisi wajinga tunapenda uongo.
Ukianza kusema magwiji kama Shivji, Mvungi,Mwakyembe, Migiro nk, angalia vyuo walivyosoma , sasa unaamaana hivyo vyuo ni vikali zaidi ya UD kwa kuwa viko nchi jirani au nje.
Angalia pia lamwai walimu wake UD walikuwa akina nani, kabla hajabaki hapo na kuendelea kusoma hadi kuwa prof. Pia angalia sana unaposema mabo ya Law, mtu kama Lamwai hayuko katika Bar Association yoyote nje zaidi ya hiyo ya Tanzania.
Elewa degree zote ni sawa tu ndo maana uliona hata degree ya Open university ya Sumaye ilimwezesha kwenda kusoma Harvard, huko US.Watu wengi wanaomaliza Tumaini, St-augustine nk huwa wanakuja Dar kwa ajili ya kazi, maana kazi ziko Dar , na ndio maana huwa wanasoma UD masters zao.
Kama kazi zingekuwa Iringa wangebaki Tumaini na masters zao wangesoma huko huko, au Mwanza wangesoma huko huko.
Mimi mwenyewe nilikuja hapa UD kutoka mikoani kwa kuwa nilifuata Elimu na nilenda iliboru A level kutoka mtwara kwa jili hiyo hiyo.
Nikipata kazi Uganda basi Masters yangu nitasoma Uganda.
Angalia sana na utoto wako wewe soma na usubiri kazi.
We kama unataka usawa wa degree basi jijue una superiority complex ila umejikuta umeangukia pabaya sasa unataka kurekebisha kwa kutushauri tukubaliane na wewe kuwa degree ziko sawa ili uridhike.
Hao tuma wanoenda dar ni kwa sababu ya know who.
wewe anony wa sept 25,saa 9:42 ninakusikitikia sana kwa kufikiria kuwa basi ukipata 1.3 na mwenzio akapata div 2,au 3 basi wewe utaendelea kuwa mkali ktk maisha yote na yeye atakuwa nyuma kimasomo,kimaisha n.k
ukweli ni kwamba maisha sivyo yalivyo,labda kweli IQ za hao watu ziwe geneticaly ziko determined kuwa ktk kiwango hicho ndipo hakutakuwa na changes. lakini kama swala ni mazingira basi tambua yote yanawezekana labda bado utoto unakusumbua.
mimi kwa taarifa yako nikwambie kwamba hata hiyo UDSM Unayo iita kali,inashika nafasi ya 20 ktk vyuo bora vya afrika.ikiwa imetanguliwa na vyuo kibao tu toka south africa,egypt &less to mention. na chuo tunachosoma na hao waliotoka shule special usidhani walikuja kwakuwa ni cha kichovu,maana ni chuo cha 10 kwa ubora kwa ubora kwa fani hii duniani ktk viwango vya UNESCO. na tuliingia huku kufuatia vigezo mbalimbali na interview na paper tofauti tofauti kwa nyakati tofauti.
sasa napo kwambia kuwa kwa sasa washikaji wanavuta shati usidhani ni wachovu,wanatisha pia japo ndo kama navyokwambia kuwa huu ni uwanja tofauti na gemu tofauti imebidi wasalimu amri maana mimi pia sikuwa mchovu nilitetereka tu kuipata hiyo TWO ya 12 kwa sababu ya matatizo ya muda tu. na wao AAA zao sio za divinity ni za combination zao.hivyo usiwaite watu sub-standard maana hiyo ni dharau. kwakuwa mimi nikiomba kazi ktk viwango vya kimataifa nitapewa first priority kutokana na nguvu ya core subject zangu na program yangu ilivyo kaa.maana kwa anaye soma hapo UDSM ambako hao washikaji walikacha nafahamu degree zenu pia zinabeba masomo gani ktk fani hii,ambapo za huku zina vitu vya ziada na masaa yake pia ni mengi na practical pia nizanguvu tena ktk international organizations.
hivyo basi nakushauri usitukane wakunga na uzazi ungalipo.unao wacheka sas utajikuta ndio mabosi wako,au malecturer wako ktk level za juu.
Unasema kufeli masomo ni kufaulu maisha? usilinganishe masomo na maisha. Masomo hayana refa lakini maisha yana refa.
Watoto wadogo bwana mna matatizo sana.
Tuliomaliza A level miaka ya mwanzoni ya themanini tunajua haya mambo sana.
Nilimaliza na division two A -level na sikuchaguliwa Chuo kikuu cha UD, na miaka ile vyuo vikuu vilikuwa UD na SUA na kama hukuchaguliwa basi unasubiri selection ya kwenda nje.
Wakati ule wizara ya elimu ilikuwa inatuma watu wa Div 2 na 3 nje ya nchi(Abroad) na kuacha cream ya Div1 chuo kikuu UD.
Kilichotokea ndo hichi ninachokisoma sasa.
Miaka ile ukienda nje ulikuwa unaunganisha na Masters, hivyo program zilikuwa miaka sita hadi saba. Na nyongeza tena ya miaka mitatu hadi minne kupata PHD.
Wengi wetu tuliorudi mwisoni wa miaka ya themanini na mwanzoni mwa miaka ya tisini kutoka nje tulipokelewa na wizara ya elimu na elimu ya juu. Tulipangiwa kazi UD, SUA, IFM nk kulingana na fani tuliyosomea kuwa walimu.
Cha kufurahisha sasa ni kwamba walimu wenzetu tuliowakuta ni wale jamaa ambao walikuwa na Div 1 zao A- level na walisoma degree zao UD.
Mambo yalikuwa ni kushirikiana , maana sisi tulikuja na technology education, maana ,mambo mengi tulisoma kwa computer miaka ile nje ya nchi tena kwa DOS. Hatukudharaulina kwamba labda mimi nilikuwa na Div 11 hivyo nilikuwa mjinga, kwani mimi nilisoma Patrice Lumumba University ,Moscow.Chuo kikuu kikubwa sana sana sana zaidi ya UD na kutoka na hons degree. Lakini pia elewa mwenye DIV 1 aliyebaki TZ ndio alikuwa mkali (tulikuwa tunawaita cream)lakini amesoma UD. Hivyo kwa ujumla nakubaliana na jamaa liyesema Div 11 mara nyingine anawavuta shati watu wa Div 1.
Kubali yaishe.
Nakubaliana na Annono wa sep 26, 5:12. Nyinyi wanafunzi wa UD mkianza kudharau degree za Tumaini, basi mkubali na nyinyi kudharauliwa na watu waliosoma Nairobi, Kenyata na Makerere university. Kwamba degree zao ni kali kuliko za UD.
Pia mkubali kwamba hao wa Nairobi, Kenyata na makerere wakubali kudhauruliwa na watu waliosoma degree zao overseas.
Nyinyi wasomoi wa UD , mmetuabisha sana sana kwa muda mrefu, maana wa-kenya na waganda huwa wanasema wasomi wa TZ hawajui kitu kabisa, na hii yote ni kutokujua lugha ndo maana tunadharauliwa namna hiyo.
Sasa na nyinyi wasomi wa UD mnahamishia dharau kwa wasomi waliomaliza Tumaini kwa kuwa hamna kibonde wa kudharau.
Dharau zenu ndo zimetuponza sana sisi siku hizi hapa TZ.
Watu wenyewe sekondari mmesoma Makambako, Uyole, Mkwawa, mara special Mzumbe. (hiyo kweli ni special school?) Mtu anamaliza hata kiingereza hakijui .
Ndo maana wasomi walikuwa wakipeleka watoto wao Kenya na Uganda O level na Alevel na baadaye kuwapeleka University za nje. Leo wanakuja kufanya kazi stanbick na backlays na reserch za nguvu ambazo wakenya walikuwa wamezishika na nyinyi wasomi wa UD kuwa mnalalamika.
Vyuo havina maprofesa, watu wanafundishwa na ma-TA tu. Cheki web-staff: under construction.
Ma-TA ndo wanafundisha basi sehemu na vyuo vikuu kibao ukisoma nchi jirani kama kenya na Uganda au ugaibuni. Maana hao ndo uti wa mgongo wa masomo.Maprofessa muda wao mwingi wanatumia kwa reserch na kuandika vitabu na muda mdogo wanatayarisha masomo na kuwaachia Ma -TA wawafundishe watu wenye level ndogo kama bachelor.
Maprofessor wanatakiwa kufundisha watu wenye level ya Masters na kupanda juu.Wewe uliye mwaka wa kwanza, na pili ni kama ex-form six bado unataka professa wa level kubwa ya PHD akufundishe nini wewe wakati sio level yake.
Unataka kumtumia professor mzima akufundishe English, Public speaking, calculus, sociology, psychology na college Alegbra wa nini. Hata akikufundisha Physics au Chemistry 1 na 2 ni sawa na kutumia muda wake bure.
Maprofessor huwa mara myingi wanafundisha kuanzia mwaka wa tatu mpaka nne masomo mahususi ya kumalizia degree zao. Masomo ya Advanced level na sio elementary au pre-requisite kwa wanfunzi wanaoanza mwaka wa kwanza au wako wa pili.
Nimeona wanafunzi wengi ambao huwa ndo wameingia chuo kikuu ambao huwa hawana hata degree ya kwanza wanapenda sana kuona Professor mbele yao kwa kufundishwa vitu ambavyo wanatakiwa kufundishwa na watu wa level ya masters na sio zaidi ya hapo. Au hata mwenye Degree ya kwanza lakini mwenye uzoefu wa hilo somo kwa muda mrefu.
Ndio maana tuna walimu shule za Sekondari wenye degree ya kwanza na sio ya pili wanafundisha.
Maprofessor sio wa kufundisha fundisha mambo ya kitoto ambao hata mtu aliyemaliza chuo kwa hiyo degree anaweza fundisha au mwenye level ya masters.
Degree za Tumaini naona inawasumbua sana UDSM, inaonekana inakuja juu sana siku hizi na inawazibia Kazi mjini dar. Kiasi kila nikisoma hii blogu naona watu wanaiponda sana Tuma, naona inakuwa tishio siku za mbele hasa wanochukua B-Com na Law.
Wewe TA kazi yake ni kusaidia tutorio sio kufundisha. Pia TA husaidia kusimamia mitihani na kusahihisha homework tuu.
Unafikiri T/A (Tutorial Assistant) maana yake ni nini kama sio kufundisha kwa niaba ya professor.
Neno Tutorial lenyewe linajielezea - Ni kufundisha.
"To tutor", na kama hilo bado hulielewi basi wewe kweli mtoto.kama nihivyo professor angeitwa Tutorial nafikiri ndo ungeelewa zaidi.
TA sio tuta hata siku moja tena TA ni konda wa tuta. Si lecturer. Mi chuo nachosoma TA hawaruhusiwi kufundisha bali wanasaidia kusimamia tutorio, kusahihisha homuweki na kusimamia mitihani.
Endeleeni kuona TA wajuzi zaidi ya Waalimu.
kweli wewe chuo chako hakifundishwi na MA - TA ndo maana hata elimu na akili yako inakwenda mrama.
Maana una umimi mimi.Kwamba chuo changu badala ya chetu au cha wote.
Tumaini bwana kiboko!!!!!!
Kweli tumaini ni kiboko kwa kushindwa. Kama si kweli kiambie chuo chako kiweke kwalifikesheni za walimu wake matandaoni sio kuweka fizi strakcha tuu.
Post a Comment