Wadau nafahamu kabisa kuwa mnafuatilia vyombo vya habari na kwa hiyo ili ninalolileta si geni kwenu!!........Mnamo juzi hapa mwanafunzi mwenzetu alikamatwa pale chuo cha ustawi wa jamii akimfanyia pepa ya supplementary girlfriend wake(his sweetheart ofcourse)....Alivyokamatwa alipigwa picha na runinga maarufu hapa nchini na alikuwa anajaribu kujificha lakini walinzi walimshika kwa nguvu mpaka wakapata clear picture ya kuwapa wananchi.....mhh jamani!!
Mshikaji ni mwanafunzi wa chuo chetu marafiki wa MZUMBE na mdada ni wa palepale USTAWI na kozi wanayosoma inafanana na ndio maana jamaa akapiga pepa!!............Kwa hiyo jamaa alitaka kuonyesha ushujaa kwa mpenzie na kwamba mapenzi yao yako level nyingine!!
Kwenu wadau...jamani tumefikia hatua hiyo ya kusacrifice masomo yetu sababu ya mapenzi duh!!...hawa watu nadhani wote wawili watakosa chuo na sijui kama mapenzi yataendelea...!!Labda watakuwa wanaoneana huruma kwa hiyo watafarijiana...mh sijui!!
Tabia za kufanyiana mitihani ya sup na ya mwisho ni tabia iliyokithiri sana vyuoni...either kwa kulipa hela ufanyiwe mitihani au kwa sababu binafsi kama hiyo ya kudhirisha mapenzi ya dhati!!......Jamani mapenzi sasa yanatupeleka kubaya!!..Tujirekebishe jamani wanavyuo na tujue haya mapenzi yana jinsi ya kuyachukulia na yana mipaka yake..........
POLENI NYIE WAPENZI WAWILI LAKINI TUNAAMINI FAMILIA INAENDELEA KUWEPO!!
Sunday, September 21, 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
10 comments:
Huu sasa ujinga. paper ya Sup unaweza fanya bila kutoa utambulisho.
kama chuo kimefikia hatua ya kushindwa kujua mwanafunzi wake basi , hakina hadhi ya kuitwa chuo na masomo yake pia hayana hadhi kabisa.
Ujinga huu ninauona sasa TZ, katika kesi za waliofoji vyeti kujiunga na benki.
Kuwapeleka mahakamani ni kutumia fedha nyingi.
Rahisi ni kuwafukuza kazi na kutoa gazetini sababu za kuwafukuzisha kazi. Pia kwa wale waliongia vyuo kwa vyeti vya kugeza ni tabia hiyo hiyo ya kuwafukuza na kuwapa muda wafanye hio mitihani waliosema wamefaulu na wakishinda warudishwe kuendelea na masomo.
Tatizo ni pale wanapobaki kusoma au kufanya kazi wakati hawana hicho kisomo.
hay mnaosema vyuo vyenu quality ya degree za nguvu sasa mnayaona wenyewe mnavyofaulu mitihani.hii hata kuitwa aibu haifai.mmhhh haya yangu macho.kisha mnao faulu kwa mtindo huo mnaanza kulia eti ajira hakuna.mkiambiwa jiajirini si inakuwa kizunguzungu maana kama paper tu kupiga mwenyewe umeshindwa hadi uagize majeshi,je kuplan mwenyewe mkakati kisha uutekeleze inakuwa imekaaje!imekaa vibaya hiyo wasomi wetu wa bongo!
Cheating? Unajichiti mwenyewe. Mi ningeomba serikali iwachukulie hatua za kisheria, na wakimaliza adhabu wapewe second chance.
Kujaribu kumwonyesha prof unajuwa kumbe hujui ndio sababu kuu ya kutoeleimika. Hata huyo dada angepasi bado asingeweza kutumia elimu hiyo kwani hana.
Kwa nini basi wasitumie njia sofistiketedi, ok chuo kichanga, lakini wangeuliza vyuo vikongwe wenye mchezo wa kuchiti wanafanyaje wasikamatwe.
Kuchiti chiti pakiwa na vichaka (wenzio) kwenye mitihani ya kawaida, mnapanga namba za wachezaji kabisa nani ampasie nani.
Supu usifanye mchezo huo.
Jamaa alitakiwa akimbie mara tu siri ilipofichuka, hakukuwa na haja ya kusubiri media.
Jifunzeni kwa wazee wa COE na DIT.
Sema tu watanzania tulio wengi uwezo wetu kifedha ndo hivyo lakini tufikie hatua tu admit ukweli, elimu yetu ya Tanzania ni kwamba hamna kitu kabisa, asilimia kubwa tunasomea mitihani lakini ujuzi hakuna kabisa, hatuwezi tuka demonstrate kile kilichotufanya tuwe chuoni kwa miaka mitatu ama minne na ndo maaana utendaji wetu wa kazi unakuwa mdogo kabisa. Sishangai kuona mtu anasema amemaliza chuo chuo kikuu lakini utendaji wake wa kazi unakuwa ni wa kubabaisha tu. Mimi nasema kama ningekuwa na fedha ya kutosha basi ningeenda kusoma kwenye nchi zingine na kisha kurudi nchini ku implement ujuzi wangu. Kwa kweli ki elimu tuko nyuma sana.
Sanka.
We anon wa September 23, 2008 9:41 AM mahubiri yako kaa nayo tuu, huna haja ya kuzunguka. Tunahisi tunajuwa kwa nini unasema hivyo. Nani kakutuma.
Kuchiti Co ishu ngeni vyuoni mwe2!
Ila ni kma football technics zinatakiwa uliza DIT na wansoma medical assistant.
Nakumbuka niliwahi kusoma mwaka m1 DIT wale jamaa wanajua vzri mchezo huo.
By the way mazingira fulani ndio yana changia wanafunzi kutojiamini na kuamua kuchit.
Eg baadhi ya walimu pepa zimekuwa ni miradi ya kujipatia fedha! Nakumbuka wkti huo kuna dada mmoja mrembo alikataa kuchit na akaenda kwa ticha ticha akamwambia atoe laki 3+akampe penzi hotelini ucku kucha ili amwonyeshe pepa ya sup!Imagine dada alikuwa akisomeshwa na kampuni kufeli kwke ni kufukuzwa kazi.
Pia pepa zinafanyika kwenye mahall makubwa sna!imagne wa2 zaidi ya 300
kwenye hall 1 hapo hkna udhibiti.
Ila nawaasa wadent wenzangu!Tabia hii c nzuri unapichiti huna tofauti
huna tofauti na fisadi aliyeghushi na kula kubeba fedha za EPA.
Huyu mwnz2 amefanya kosa kubwa sana!Amevuka mipka ya kuchit.
Kwanza ameidanyanga serikali ya jamhuri ya muungano hivyo anapa swa achukuliwe hatua kali sana za kisheria.
Pili ametudhalilisha sana!Sasa tuna wapa msemo hata makonda na wa sioenda skuli wote!Coz kama kusoma ni kuchiti hata wao wangeweza.
Kupenda gani bwana!sasa shule wanaikosa na wenye fedha zao demu watamchukua.
Mambo haya si Tz tu,ni africa nzima.
Waafrica hatujiamini kma tunaweza fanya jambo lenye mafanikio bila ktia hila fulani.Mfano baadhi ya wanafunzi hawaamini kuwa watafaulu bila ya kuwa na FEKI.
Kadhalika viongozi we2 hawatapanda vyeo mpka wafanye uchawi.Hawatapat mafanikio ila kwa kuiba mali ya UMMa
Hata Taifa stars,Yanga na Simba pamoja na kuwa na makocha wa kigeni bado hutumia hela nyingi kwenye uchawi.
Hata kuna cku TFF ilifoji umri wa mchezaji fulani wa serengeti boys. hatimaye ikajulikana na tanzania tukapokonywa ushindi wote.
Nimefutilia Documentary nyingi za nchi za kiafrica matatizo hayo yapo.
Wakati wazungu hata mwanao tu akilia sana ucku basi unaweza fikishwa kwenye dola achilia mbali kuchit!
Well nachukua nafasi hii kuwapa pole wenze2 hawa.Nawafariji kwa kuwa tabia hii ipo africa nzima wao si wa kwanza.
Nyota ya mchzo wa kuchit haikuwa yao cku hiyo JUMBA BOVU likawaangukia.
Wawe tayari kwa adhabu yoyote na huo ndio utakuwa msamaha wao duniani na na AHERA
Mambo haya si Tz tu,ni africa nzima.
Waafrica hatujiamini kma tunaweza fanya jambo lenye mafanikio bila ktia hila fulani.Mfano baadhi ya wanafunzi hawaamini kuwa watafaulu bila ya kuwa na FEKI.
Kadhalika viongozi we2 hawatapanda vyeo mpka wafanye uchawi.Hawatapat mafanikio ila kwa kuiba mali ya UMMa
Hata Taifa stars,Yanga na Simba pamoja na kuwa na makocha wa kigeni bado hutumia hela nyingi kwenye uchawi.
Hata kuna cku TFF ilifoji umri wa mchezaji fulani wa serengeti boys. hatimaye ikajulikana na tanzania tukapokonywa ushindi wote.
Nimefutilia Documentary nyingi za nchi za kiafrica matatizo hayo yapo.
Wakati wazungu hata mwanao tu akilia sana ucku basi unaweza fikishwa kwenye dola achilia mbali kuchit!
Well nachukua nafasi hii kuwapa pole wenze2 hawa.Nawafariji kwa kuwa tabia hii ipo africa nzima wao si wa kwanza.
Nyota ya mchzo wa kuchit haikuwa yao cku hiyo JUMBA BOVU likawaangukia.
Wawe tayari kwa adhabu yoyote na huo ndio utakuwa msamaha wao duniani na na AHERA
Mi nasema mabinti wananyanyasika saana masomoni. Off course hawafanyi jitihada saana, ila kuna dalili nyingi zinaonyesha kuwasukumia katika kutoa rushwa ya ngono kwa walimu ili wawafaulishe, au kwa vipanga ili wawakochi au wawadeseshe. Ili mradi msichana asumbuliwe kuhusu mwili wake.
Nawalaumu madada wanotumia miili yao masomoni kwa ajili ya kupata manufaa ya kielimu. Unatakiwa kutumia akili siyo mwili. Na kwanini muone mwili ni silaha.
Haya masuala hufika mpaka makazini wadada wataka ajira au promosheni kwa kutumia mwili na siyo kwalifikesheni zao.
Dada zangu zama zimefika za kujikomboa na utumwa huu. Ninyi ni watu na mna uwezo wa kiakili sawa na wanume. Fanyeni jitihada, anzeni kwa kutotumia wakati wenu kutongozwa. Muda wa kutongozwa unaweza kutumika vizuri kusoma. Watu wanawatongozeni wakishamaliza homuweki zao. Matokeo yake ni mabaya ukiacha maradhi na mimba, unafeli masomo na hutoki kwenye "vishazi saiko of seksi." Utaendelea kutumia seksi kama silaha mpaka unakufa.
HIMAA akina dada!! O'yeah I am crazy, go ahead and have sex, the only liberty u've known.
Post a Comment