Salamu Wadau
Samahani kwanza kwa kutoonekana kwa muda mrefu wala kutopata updates kwa muda mrefu!!
Ila ninafahmu wengi wenu mnaelewa kilichokuwa kinaedelea na hamtanilaumu kwani nilikuwa katika kipindi kigum mdau wenu,kipindi hicho kigumu kimesababishwa na viongozi wa chuo changu na wanaharakati feki kwa kuanzaisha migomo wasiyojua itatupeleka wapi.....kwani mpaka leo hii ninavyoongea mdauu wenu jina langu halijatoka na sijasajiliwa na masharti yote nimetimiza ila kwa mbinde.....!!
Nimepitia uzoefu flani mgumu katika maisha yangu ya elimu,uzoefu wa kugombana na chuo na serikali....na mwishowe nime concede defeat kwani chuo na serikali ndio vimepata ushindi na wenzetu wengi bado wako nyumbani hawajui hatma yao!!mungu wasaidie kwa sababu sio kosa lao kosa ni la siasa ilivyoingia vyuoni na viongozi wa wanafunzi wabovu na wanaharakati feki wasiotumia hoja na usomi bali nguvu!!wanafunzi wapatao 2000 inasemekana wamefutiwa udahili japo bado sijaaminiamini vile,na wengineo masikini wasioweza kulipa ada bado wako nyumbani....laana kwa viongozi mlioandaa mgomo na wanaharakati feki,na nyie chama cha siasa cha CHADEMA muwe makini siku nyingine mkiandaa mgomo,mmetupotezea marafiki wengi,vita vyenu na CCM pelekeni nje ya chuo!!vyama vyote vya siasa tawala na msio tawala tuko chini ya miguu yenu msitupotezee muda wetu wa masomo kama ni haki zetu tunazijua na tutaidai wenyewe hatutaki mikono yenu!!
Swali langu ni kwamba fujo zote zilizofanyika na masharti magumu yaliyowekwa na chuo..je wanafunzi watasoma vizuri kweli....maanayake wengi wako affected psycologically.........hata hao endapo chuo kitakuwa na huruma ya kuwarudisha sidhani kama watakuwa kawaida...mungu tusaidie!1Nakuja kwenu chuo kikuu cha Dar Es Salaam....Salamu kwako proffesor mkandala...baba naomba uwarudishe marafiki zetu chuoni,wengi sio kosa lao wanakuwa punished kwa kitu ambacho hawajafanya,kosa ni la wanaharakati feki na wachochezi ambao mimi siwaungi mkono na niko tayari hao wapoteze chuo na sio hao 2000 wasio na hatia,na nina mifano ya baadhi yao ambao hawakugoma kabisa...lakini inaonyesha hawatarudi chuoni...ninaomba uwasamehe mkuu!!
ninaongea haya kwa uchungu sana na ntaongea tena post ijayo!!
waliotimiza masharti ndio hivyo tayari wanarudishwa na wameshapewa vitambulisho vipya na karibia wanaanza masomo!!...mungu wangu wasaidie waliobaki ba wasaidie waanzae masomo vizuri ili wasiathirike na uzoefu mgumu waliopitia....!!...na ninaomba wanafunzi wabishi mpunguze ubishi wenu na tusolve matatizo yetu kisomi!!
Asanteni,Mdau Wenu
William!!
My faves handbags on Sale..
4 months ago