Wednesday, August 27, 2008

TUWAPE USHAURI WANAFUNZI JAMANI!!

Tunashukuru sana kwa maoni mbalimbali ambayo wadau mmetoa hasahasa kwenye mada ya kwanini watu wanaofeli vyuo vikuu ni wengi sana!!Ukiangalia historia za watu hao wengi wao walikuwa wazuri sana kwenye elimu ya sekondari…Sasa wanafunzi wafanyaje ili wafaulu katika mitihani yao vyuoni??....Maana discontinue zimeongezeka sana kwenye vyuo vya umma vikiongozwa na Chuo kikuu cha Dar es Salaam,Supplementary pia zimekithiri vyuoni mfano ikiwa ni IFM na vyuo vingine vya umma.
Nyie mliopo makazini mlivuka vipi huu mchakato?...Au elimu imekuwa ngumu zaidi siku hizi?..Hebu tuwape ushauri vijana waliopo vyuoni kuhusiana na vitu gani wazingatie na vitu gani wapunguze ili wafanye vizuri katika masomo yao!!
Tuwape ushauri sasa maana hapo chini mwanzoni kabisa wadau mmeongea mengi sana kuwahusu wanafunzi waliopo vyuoni.......
Au haiwezekani?..Kwasababu disco zipo kuanzia miaka mini sana iliyopita mpaka leo….WAPENI USHAURI WANAFUNZI JAMANI ILI TUJENGE WATAALAMU BORA KATIKA NYANJA MBALIMBALI

11 comments:

Anonymous said...

Mie nawashauri kwanza kuacha kufuatilia mafeki na hili limechangiwa na tabia hiyo tangu chini. La pili kusoma kwa zimamoto si kuzuri kunasababisha ufahamu wa jambo kupotea matokeo mtu hukariri badala ya kufahamu. Na wengine hasa wasichana wapunguze starehe na tamaa kwani zinachukua nafasi kubwa kiakili badala ya kufikiria shule mtu anafikiria mabwana kwasababu hakuna mtu wa kumzuia

Anonymous said...

Sababu za wanafunzi kushindwa vyuo vikuu ni vingi na zinachangiwa na vitu vingi. Kuna sababu za binafsi, za kimazingira, mabadiliko na ufundishaji, na zinazotokana na walimu/wakufunzi.

Hizi sababu zote ni pana sana. Ila kwa manufaa ya wale mlioko vyuoni, nitasema machache.

1. Unapoingia chuoni, sahau "ur past glory", kwa maana ya zile 'A' ulikuwa unapata O'level na kidogo A'level. Chuo ni different game. Lakini pia unaposahau ya nyuma, usisahau mbinu/stamina iliyokuwa inakufanya unapata As huko nyuma. Ila sasa ujue kupata 2/10 kwenye test ni kawaida, sawa na kupata 10/10. Ila ni jitihada binafsi na wakti mwingine group wise (team work). Chuo chochote kile kinahitaji mtu kukaa chini na kusoma. Na kusoma maana yake si kukariri. Hapana, kuelewa topic na logics behind. Elimu ya chuo inakuandaa kuwa thinker/problem solver kitu ambacho ni tofauti sana na elimu za awali. Ila kama huko nyuma ulikuwa unapata marks ambazo zi zako (kwa maana ulikuwa unatumia leaked exams and the like), then chuoni si pako.

2. Mazingira mapya yanachangia especially kutokana na uhuru unaopatikana ktk vyuo tofauti na shule za chini. Mara nyingine uhuru huu unaweza kuwachanganya baadhi ya watu na hivyo kujikuta wanashindwa kuji-control.

3. Elimu yetu ya Tanzania (ya sasa) hasa Chuo Kikuu (UDSM) imekuwa haitabiriki kwa wakati mwingine. Hii ni kutokana na walimu kufundisha vingine na mitihani kutungwa vingine. Hivyo wanafunzi wanajikuta wanakariri madesa ambayo mengine ni ya toka mwaka 1988 (Huu ni ukweli). Hakuna kitu kibaya kama kukariri na bila kujua logic behind. Hii ni mbaya zaidi kama hili linafanyika katika ngazi ya Chuo Kikuu.

4. Walimu wengi wa vyuo vikuu hawana motisha ya kutosha (lack of motivation), hivyo hawajitumi katika ufundishaji. Wanafanya ufundishaji kwa sababu tu ni ajira, lakini they don't go extra mile in ensuring students get what they deserve to now.

5. Wako waalimu wachache, mfano UDSM, ambao kwa sababu wanazojua wenyewe, wameamua kuwa "wanakamata" wanafunzi kila mwaka. Mifano ipo. UDSM(Economics,Sociology, Electrical,Mathematics etc). Kibaya zaidi walimu hawa hawa wanarudia tena na tena kila mwaka, lakini uongozi wa Chuo huwa hausemi chochote.

Bottomline, kusoma chuo si LELEMAMA. Bank on ur past achievements BUT you have to be determined to SUCEED othersiwe utakuwa frustrated na marks unazopata na utakata tamaa. Chuoni hutakiwi kukata tamaa kwani panakujenga for more challenges in life.

My few cents.

Anonymous said...

kaka hapo wanafunzi wa udsm ama vyuo vingine vya tz inabid wakamuke sana mosuli, sio kama sup hakuna hata vyuo vya nje nope zimejaa tena ziko nyingi cuz wanafunzi wanajiachia sana, hivyo like tz univs wanafunzi wanajiachia sana baada ya kusoma kwa bidii, kuhusu discont mmmh kweli hapo vyuo vya tz vimezid hata mie nilikuwa kichwa kinoma but ilibid niiteme coet pale udsm course ya telecom eng cuz ya maneno ya watu juu ya kudisko, now hapa poland sijawahi kusikia kuhusu kudisko wala nn sema watu wanasup kama kawa kama husomi, cha msingi ni kukamuka tu kama martin chegele
mdau kutoka poland
suna bufungile
lodz university of technology

Anonymous said...

Mi nasema:

Hamna mwalimu anayefanya roho mbaya. Elimu imekuwa kutokana na kukua kwa teknologia kwa hiyo mawazo ya watu wa makazini si lazima yawe na manufaa kwani mitihani ya sasa inarelect elimu ya sasa komavu.

Pili wanafunzi kufeli ni lawama kwao wenyewe: zima moto mbaya mno. Watu badala ya kutumia vihela vidogo kununua vitabu wanashona suruali za vitambaa. Usinunulie nguo hela ya shule.

Halafu kudisco siyo kubaya saana. Maana wajao kesho hawatacheza, watajifunzia kwa hawa.

Tumedisco tokea seminari.

Anonymous said...

hakuna sehemu duniani yenye shule rahisi,isipokuwa mazingira ya usomaji,ufundishaji,upatikanaji vitendea kazi,jitihada binafsi na mbinu za usomaji zinatofautiana mahali hadi mahali.
kwa tanzania nafahamu watuwengi wanatumia system ya kumeza[kukariri maswali na majibu] na hii huwafanya wengi kujenga tabia hiyo tangu shule za msingi,sekondari,na hadi vyuoni. kwakuwa watuwengi ukijaribu kuwachallenge huwa hawawezi kutoa logical reasoning,ndio maana mitihani ikibadiliskidogo tu wanapotea maboya maana wanataka wakute kile walichokwisha pitia.
huku ninakosoma mimi kwanza wakati wa mtihani kilamtu darasani anapewa maswali yake yasiyo fanana naya mtu yeyote,provided yanatakiwa kuwa ktk sylabus yakuwa covered ktk level hiyo,then unapewa takribani dakika 10 kuyapitia na kisha examiner anayachukuwa,then unaanza kuyajibu oraly kwa kutoa maelezo ya kina tena mbele ya wanadarasa wenzako,huku examiner akikupiga maswali ya ziada akikutwist huku na kule hadi nje ya topic kuhakikisha kuwa unachokieleza hujaegesha bali unafahamu kwa ufasaha,then ufasaha wako wa kujibu,flexibility ktk kuunganisha logic,na time ndizo hudetermine grade unayopewa na examiner anasema mbele ya darasa wewe hapa nakupa A,au B, etc.hivyo kama umeonewa wotewatakuwa mashahidi,na kama umepaliwa mwenyewe pia wote wanakuwa mashahidi.
kuhusu mazingira nikweli kwamba inawezekana wanavyuo wengi hapo tanzania kwakuwa wakonyumbani hujiona wamefika chuokikuu na kuiona degree kama ndio mwisho wa mamboyote,hivyo kurelax. ama huenda mazingira ya kusomea pia yanachangia kwa kutobalance ratio ya wakufunzi kwa wanafunzi,hapa maximum huwa ni 1;14 na sio zaidi,hivyo mkufunzi atahakikisha unaandika lecture zote,unafanya dailly asigniments,unazi defend asigniments zako darasani daily,na unaparticipate kujibu maswali ya topic husika kuhakikisha kuwa uliisoma kabla ya kuingia darasani ipasavyo,then yeye atakupa knowledge ya ziada pale mnapokwama.
pia napenda niweke wazi kuwa wakufunzi wengi hapa ni maprof,hivyo unakuta hanautata wala kigugumizi ktk field yake,anakupa full nondo bilakinyongo maana yeye kama prof wajibu wake ni kukufanya uwe gado ktk somo analokufundisha,na hivyo hatakupa nafasi ya kupaliwa hovyohoyo.maana utakuwa unamdhalilisha yeye.
materials pia upatikanaji wake huwa zipo tu,labda ushindwe kifedha,lakini vinginevyo zille materials ambazo ni current zote zinapatikana,na maranyingi maprof na accademic wa hapa chuoni wanatunga vitabu vya kufundishia wenyewe,na kila wakati wana update materials kutokana na mambomapya kugunduliwa na kupitiwa kwa kuhakikiwa na kuingizwa ktk matoleo mapya,vinginevyo yanakuwepo ktk lectures.
jitihada binafsi: kutokana nakuwa wanavyuo wengi huwa wamezoea vituvilivyokwisha tafunwa na kupikwa hasa ktk tuition za A'level wanapvyuoni hushindwa kuwa wanacope na elimu inayo kufanya uitwe uko chuokikuu,hasa kwa hapo tanzania ukizingatia lugha ya kiingereza ni msamiati kwa wengi,wakati mwingine huwafanya watu kushindwa ku-comprehend materials hivyo kuchukua superficial knowledge,au sometime uwezo wa kujieleza unakuwa mdogo kutokana na kupata kigugumizi cha lugha.pia kuridhika kuwa tayari yuko chuokikuu.lakini huku unajikuta vijan unaosomanao wanamiaka 17,ktk miaka 21 tayari mtu anadegree,23,24 wana masters na kati ya 27-31 wana phD unakuta kunakufanya usome kwa bidii sana ukiwa na malengo makubwa zaidi ya bachelor,na kwakuwa competition inakuwa kalisana kwao wakiwania nafasi za kupata masters,inakulazimu nawewe kupigashule ili usiwe unakuwa nyuma kilawakati.
mafunzo kwa njia ya vitendo pia nadhani kwa hapo tanzania huwa ni kidogo kutokana na ukosekanaji wa vifaa,au vinakuwepo lakini havitoshi na sio vya kisasa.huku kila practical inayotakiwa kufanyika wanahakikisha inafanyika na kila mtu anafanya na kukaguliwa,hivyokuwezesha kuelewa kile unachokisoma sio tu theory yake bali na practical application yake,tena bila kuwa na kigugumizi cha jinsi ya kufanya.
CHUKI BINAFSI: hapa pia napenda niseme kwamba wakati mwingine kama navyodhania japo sinuhakika,huenda wakufunzi wengi wa vyuo vya hapo nyumbani wanakuwa wanaelimu ya kawida kama bachelor,masters hivyo wanahofia wakiwafundisha wengine vizuri na kuwafanya wafaulu vizuri itapelekea kuwakosesha nafasi za kwenda kusoma wao,hivyo huishia kuvizia hizo nafasi wakiwa kama proffesional students na kuwafanya wengine wawe ktk mazingira magumu ili kupunguza ushindani ktk hizo nafasi,iliwao ndi wa qualify kuzipata na kuendeleza monopoly ktk field hizo.
japo kufeli,ku krudia,n.k vipo tu hata hapa lakini nikama kweli wewe na shule ni kama media player na file zisizo ingiliana@@@!!!
yangu machache kimtizamo tu !
mdau ughaibuni masomoni.

Anonymous said...

Quote " Hamna mwalimu anayefanya roho mbaya. Elimu imekuwa kutokana na kukua kwa teknologia kwa hiyo mawazo ya watu wa makazini si lazima yawe na manufaa kwani mitihani ya sasa inarelect elimu ya sasa komavu. "

Quote " Tumedisco tokea seminari."

Hivi ni kweli hakuna walimu wenye roho mbaya? Hivi umewahi kusikia wanafunzi wanakamatwa 50% kila mwaka kwa somo lile lile, tena madarasa tofauti, na Mwl asiwe na roho mbaya ?

Na vipi kuhusu walimu ambao kwao mwanafunzi hawezi kupata A miaka nenda rudi ?

Hii mifano si ya kufikirika, ni halisi imetokea na inaendelea kutokea. Kama haijakutokea kwako, wapo wengine imewatokea.

Hivi kweli tunaweza kufananisha level ya ku-disco at seminary level na disco at univ level ? Huu mlinganyo si sahihi.

Uki-disco seminary at least kuna alternative. Unaweza kumalizia shule nyingine. Unapo-disco mwaka wa 3 chuoni unaanzia wapi ?

Elimu imekua- ipi hiyo ? Teknolojia ipi hiyo ambayo TZ tunaitumia ktk kufundishia vyuoni kwetu ???

Anonymous said...

we suna acha uzush unasema ulipata udsm ukapija chini.sio vema mwana kudanganya.ww ulienda poland baada ya kukosa kabisa chuo tz.uliapply mzumbe sua na udsm kote ukakosa kutokana na matokeo yako ndo ukapata poland ambako hakuna ishu kabisa njaa tupu mnategemea pesa ya bod leo unataka kudanganya kuwa ulipija chin udsm.?sio vema kujipaisha mzee kwasababu watu wanakujua mzee.poa ni mm mwanao wa ukweli.

Anonymous said...

Narudia, hakuna mwalimu anamfelisha mtu kwa makusudi kwa roho mbaya. Kama kuna mwalimu huyo basi huwezi kuthibitisha kwa sababu hamna kosa kikatiba linaitwa roho mbaya au chuki. Pia sheria ya tz haiweki vifungu vya kuthibitisha roho mbaya au ubaguzi, hivyo ni uzushi na visingizio vya kushindwa.

Ili mradi mhadhiri alifundisha, na external exerminer akathibitisha mtihani ni fare, basi hamna sababu ya kufeli.

Halafu usidanganywe, mtu huvuna alichopanda. Huwezi kumuangukia mwalimu eti hatoi A wakati umeshindwa kuipata mwenyewe. Hivi A zagawiwa ovyo? We mtu umeingia na vi-C halafu unataka A? Kuna vyuo vya kugawa A mnavijuwa nendeni huko mkagawiwe.

Halafu ndio, ukidisco chuo kikuu utajiju kama utahamia chuo kingine (ambavyo inashindikana kutokana na rank, huwezi kudisko Tumaini, St Joseph au Augustine halafu ukamalizie UD, japo ukidisco UD unaweza kumalizia Tumaini shule ya kifeza).

Unalaumu kulinganisha disco za secondari na Chuo? Kama wajua chuo si mchezo mbona wadisco sasa? Kawaida level ya adhabu inakuwa kadiri unavyoenda juu.

Anonymous said...

Hii ni kweli huwezi "reward A for the sake of rewarding". Lazima mwanafunzi aonyeshe yeye ni A kweli. La sivyo tutaja pata madaktari wa kubadili wagonjwa, wa kichwa kafanyiwa mguu and vice versa.

Waalimu ndo marefa wetu, sasa akikusingizia A si ataumbuka ukienda kazini au masomo ya juu?

Halafu hakuna uonevu katika kusup na disco. Maana mitihani ya UD ni uniersal, mtu aliye chuo chochote duniani anaweza kuufanya kwa kiwango cha international. Na ndio maana ma-external exterminer hupitia mitihani kama ni fare(not weak not strong) na pia hupitia matokeo.

Unknown said...
This comment has been removed by the author.
Unknown said...

Kwan ni lazima kurudi chuo ulichosoma baada ya kuclear supplement.. Is that there is no chance for any student thought the other universities had already started studying?