Thursday, August 28, 2008

WADAU HILI SWALA LIMENIUMA SANA!!

Kuna mtu nimekutana nae leo asubuhi katika kupiga nae stori nikamuelezea mambo ya wanafunzi wa vyuoni akaniambia hataki hata kusikia…….Nikamwuuliza kwa nini?...Akasema eti sisi wanafunzi wa vyuoni ni wahuni sana!!...
Akachukulia mfano wa vyuo vya hapa Dar…UDSM,IFM,CBE,MUHIMBILI,DUCE na ARDHI UNIVERSITY.
Akaongelea maswala ya Night clubs,Bars,Shows…Uvaaji wetu na kila kitu akijumlisha Ulevi,U…. yaani mpaka vingine sivitaji!!
Hivi alitumia vigezo gani huyu mzee….Maana ni mzee wa makamo kidogo na anafanya kazi ofisi nzuri kidogo!!
Jamani ni kweli haya tunayoambiwa kuwa sisi ni wahuni?…Tufanyeje tuondoe hii dhana mbovu kwa baadhi ya watu?......Au ndio sababu hatufanyi sana vizuri masomoni?
Lakini bado siamini na limeniuma sana ngoja niwasikie nyie wadau…Nilikuwa nimepanda nae gari la Mwenge-Posta asubuhi hii wakati ananiambia hayo maneno…Ni mengi sana aliyosema na ameongelea pia migomo na kusema ni uhuni tu..
JAMANI JAMANI…………………..

7 comments:

Anonymous said...

Habari za Mchana,
Mimi pia nimewahi pata shutuma kama hizo na zikaniuma sana, lakini nilishindwa kuzikataa au kukzikubali moja kwa moja hadi nilipofanya uchunguzi na kubaini yafuatayo:-
1. Ni kweli baadhi ya wanavyuo (tena walio wengi)tabia zao ni za kipumbavu haziendani kabisa na Kiwango cha Elimu, ukiuliza utaambia ooh kila mtu ana haki ya kufanya chochote na kudai ya kwamba hivyo ndivyo ilivyo na ndivyo ajuavyo.
2. Pia nimegundua ya kwamba wanavyuo walio wengi hawafahamu hasa nini mtazamo wa wanajamii/Raia wa kawaida juu yao(wanavyuo).
Wanashindwa kutofautisha hasa ni nani mwanachuo na ni nani mtu wa kawaida, hii ni hasa kwa kinadada
Nadiriki kusema haya kwani nimeyashuhudia mwenyewe pale UDSM nilipokuwa student,
Inafikia hatua mtu unajiuliza hivi kama Binti wa chuo kikuu anashindwa kutofautisha mavazi je huyu ataweza kutofautisha ukweli na uongo kwenye Policies zetu??????? Unakuta vazi la Usiku tena kwenye party yeye kavaa Lecture room,Au Kimini babkuubwa (cha club na mpenziwe)anakivaa lecture rooms.
3. Wanaume nao ndio balaa tupu walevi ile mbaya na wakinywa basi ni vurugu tupu, bangi kwa kwenda mbele (hii niliishuhudia pale Mabibo Hostel uwanjani), kugombania vibinti vidogo mtaani eti kisa ni 'Msomi' basi title mtaani.

4. Madada zetu na hata baadhi ya wanaume wameendekeza sana dhiki na kupenda vitu nje ya uwezo wao, hivyo hujikuta wanafanya mambo yasiyoendana na Kiwango chao cha elimu.
Imefikia hatua huku mtaani mtu anakwambia ukitaka demu mzuuri tena kirahisi we nenda Mlimani/Mabibo UDSM, CBE au IFM wao ni dezo tuu tena hawana tatizo ni pesa kidogo tu au mpeleke Club kwisha habari yake.

USHAURI.
Ni lazima tubadili mtazamo wetu wenyewe kama wasomi, tuwe watu wa kufikiri (Reasoning)zaidi kuliko kuchukua mambo kama yalivyo. Pia tuifanye jamii ituone ni watu wenye msaada wa kimawazo kwao siyo kutuona kituko.
Huyo mzee anaweza kuwa sahihi japo uamuzi wake wa kujenga chuki na wanavyuo si mzuuuri sana

Huo ni mtazamo wangu na niliyoyashuhudia.
Hoja ni msingi wa mabadiliko, naomba nijibiwe kwa hoja.

Daudi.
" ....Emancipate yourself from mental slavery...."

Anonymous said...

well kitu kikubwa nikukubali kwamba kukosolewa ni kuimarishwa na sio kudhoofishwa.
change accordingly if possible.

g7
uk

Anonymous said...

Asilimia kubwa ni wahuni kweli. Na wakifeli wanasingizia walimu waonevu, we mhuni atafaulu nini?

Wengine wanasema kuna walimu wana ada ya kunyima A. "reward A for the sake of rewarding?" Lazima mwanafunzi aonyeshe yeye ni A kweli. La sivyo tutaja pata madaktari wa kubadili wagonjwa, wa kichwa kafanyiwa mguu and vice versa.

Waalimu ndo marefa wetu, sasa akikusingizia A si ataumbuka ukienda kazini au masomo ya juu?

Halafu hakuna uonevu katika kusup na disco. Maana mitihani ya UD ni uniersal, mtu aliye chuo chochote duniani anaweza kuufanya kwa kiwango cha international. Na ndio maana ma-external exterminer hupitia mitihani kama ni fare(not weak not strong) na pia hupitia matokeo.

Anonymous said...

Hauwezi kuruka stage yoyote ya maisha. Kwa wengi walio kama mimi walicheza kombolela na kidali wakiwa wadogo. Na katika kombolela kulikuwa na kila aina ya mambo ambayo kwa sasa tungeyaita mabaya(i.e. kufanya m***i ) ingawa ilikuwa utoto.

Kuhusu sisi wanachuo. Kwanza umri unaturuhusu kufanya hivyo kwani tusipofanya sasa baadae itakuwa balaa. Kunywa bia, kuwa na wanawake wengi yote ni yetu ili tuweze kupima na kujua lipi ni lipi. Mimi binafsi nachukia sana watu wanaosema wanafunzi wa vyuo wahuni. Halafu huyo mtu ni mzee(mtu wa makamo) na ana wanawake chungu nzima. Alivyokuwa chuo alikuwa mtu wa swala na kanisa, sasa yeye mtu wa wanawake anaona sisi wahuni.

Stage ya maisha hairukwi. Tunywe bia kwa kipimo, tusizidishe, tusikere jamii. Wanawake tuwe nao ila tuwe macho na tuwe na tahadhari UKIMWI upo kweli. KWA SASA HAYO NDIO MAISHA YETU, tukiyaruka tutayakuta uzeeni.

Na nyie wazee acheni kuongea ongea tu, kumbukeni mlifanya au mnafanya nini. Kila kitu kina stages

Anonymous said...

Mbona unawalaumu wazee kuwa na wanawake kwani ni kosa?

Anonymous said...

Habari zenu waungwana!
Bahati mbaya sisomi UD and don't know much about UD stories apart from media.
Nadhani wa UD wenyewe mmekiri kuwa ni walevi,wahuni na malaya kina dada.
Unajua kuna ujana!ndio ila pale ndugu zetu mnapoacha masomo na kudai muongezwe mikopo kumbe ni ya kunywea BIA?na kuhonga?
Hapo hamtapata huruma wa watanzania!ndio maana mnapoandamana serikali huwachukulia kuwa ni wahuni kwa kuwa huwa mnapigana vikumbo na wazee wenu kwenye mabaa!!

Ok mazee by the way huwezi kuwa star bila kuwa na kashfa!au vepe!
Mfano nyie wa UD si ndio mastaa wenyewe hapo TZ bana!

Ok the Mzee was right!It was a remark to you guys so you better change!
Kumbukeni elimu yenu watu masikini wanaitegemea sana!

Aurevoir!Merci!

Anonymous said...

Huyo mzee au hao wazee lazima waelewe kila kitu na wakati wake majority of students wanaongia college na Uni. ndio wanatoka step moja ya ujana kwenda ingine so let them do whatever they want ndio muda wake la sivyo utakuja fanya vitu vya ajabu mbele ya mkeo au mmeo ila huko home watch ya move buddies which am sure u all know... Sipendi sana watu wanaojugde watu na mavazi ila zote ni kwamba they don't have explosure ndio maana they sound...
Students behaviour ipo hivyo popote ni party animals i have been different places in Euro. na nimeona hivyo na in da mean time nakaa one of da nicest students acco. yenye more than 800 students imagine kila siku ni parties na kila mtu anajua Europe uvaaji sio issue...so let peeps do their thang aiight Achaneni na wazee na watu wanaofikiri kunywa bia ni uhuni! No Unapata akili ya kutafuata hela ulitaka wakanywe mataputapu hell no wasomi wa jinsia zote wanataka viburudisho isn't?
http://www.tvu.ac.uk/paragon/What_is_Paragon_like.jsp

Londoner