Friday, September 5, 2008

HEBU TUAMBIENI BASI MAANA SISI TUNACHANGANYIKIWA!!

Bado wanafunzi wengi sana wa kitanzania waliopo hapa nyumbani wana ndoto za siku moja kuishi Ulaya au Marekani......Na nia yao ikiwa ni kupata maisha bora zaidi ya hapa nyumbani na kupaata Channel nzuri za kutoka maishani mwao!!
Sasa je ni kweli kuwa huko nje kuna maisha mazur zaidi ya hapa nyumbani au tunajidanganya...maana mimi mwenyewe mdau bado nina AMERICAN DREAM humu kichwani!!
Mliopo nje tayari mnaonaje?Je tuendelee kuota kuja huko ughaibuni au??...Na sisi tuliopo nyumbani tunasemaje au ndio tunazidi kupotoka??
MDAU LAZIMA SIKU MOJA NIKANYAGE STATES!!....AM I WRONG!!

46 comments:

Anonymous said...

niki kwambia kwasasa wakati umevaa tai,umechomekea shati lako safi,na simu mkononi kwamba uende ukanisaidie kumlea mwanangu hadi jioni na kunifulia nguo kisha nita kulipa pesa yako kila wiki nadhani utakasirika sana.maana unaona aibu kwa demu wako,washikaji zako,n.k na pia unauhakikia kuwa una mahali pa kulala[labda unalipa chumba 30,000/Tsh pale sinza]na hata kama huna chakula unaweza kula pale kwa mshikaji wako wa magomeni mwembechai kisha siku ikawa imetoka. lakini pia kumbuka kuna mdogo wako aliyeko kule kijijini kwenu namtumbo au mchukwi anataka sana aje DAR maana DAR maisha ni safi na kuna kazi na pesa nyingi,japo wewe umemaliza bachelor ya sociology hapo UDSM na sasa ni mwaka wa 3 huna ajira unakata mtaa,ila mdogo wako aliyemaliza darasa la saba anajuwa akifika DAR tu amewini.
PICHA niliyo kujengea hapo juu inakupa mfano wa kwanini ukifikiria watu walioko nje wanawini au kufail ktk maisha. swali ni hili:-
1.JE kama umeshindwa kupata heshima ukiwa nchini kwako unadhani utaipata ukiwa nje?
2.kazi unazo zikataa ukiwa hapo nyumbani mfano kunifulia nguo na kumlea mwanangu kwakuwa una degree unadhani ukiwa nje utajivunga?
kwa ufupi ni hivi,watuwengi wanao kimbilia nje kwa matarajio ya ku-make life hujikuta ktk mazingira magumu sana yanayowafanya kufanya kazi ambazo wakiwa home wangejivunga,lakini kwa vile nje hakuna cha babayako wala mamayako,kinacho kufanya mtu ni fedha yako basi hiyo fedha utaitafuta hata kwa kazi za aibu ambazo normaly ukiwa bongo hutazikubali!na hii ndiyo siri pekee ya mafanikio ya watu hao.maana kama matarajio yake ya kufanikiwa ilikuwa ni kwenda USA na sasa yuko USA na halihalisi anayoiona ndiyo hiyo,sasa asipojituma kufanya hizokazi za kijinga jinga anatarajia ataenda kufanikiwa wapi tena?kongo?kenya?hahaaa!hapa sasa inakuwa ni ama kufa amakupona. tena wengi anakuwa huenda alitosa shule bongo akaondoka kwa nyodo akijuwa amewin life,sasa ngoma akiikuta ndivyo ilivyo inabidi apinde kiuno tu liwalo na liwe! na wengine hata pesa ya kurudia home inakuwa haikusanyiki maana maisha ni ghali hivyo analazimika kuendelea kubana hukohuko,japo anazeeka na hakieleweki.je unadhani mkiwasiliana naye atakwambia mzee nateseka kinoma!hahaa la hasha! atakusifia tu jinsi anavyoishi ili na wewe uende mkasaidiane machungu,ukibisha wee nenda uone hata mshikaji wako mliyekuwa mabest bongo atakuwa anakukacha unapokuwa na shida hasa ya kifedha.
msijidanganye vijana,maisha na heshima utavipata pale kwako unapoheshimika,unapoweza kutambuliwa na watu kama binadamu mwenye hadhi yake .bora tu uwe na mipango madhubuti na mitazamo chanya na uache ujinga ujinga wa kuchezea muda na fedha.vinginevyo nenda kwanza nje ukapate lesson,ili ukipata mtaji tu utajuwa namna ya kuutumia maana tayari umeondoa tongotongo na ujinga ulio ujaza kichwani kuhusu maisha ya nje.
nje kunawatu wanaelimu zao wengine hadi phD na wangeweza kuheshimika home,lakini kama phD yake haihitajiki hapo alipo atafagia barabara na kuwa tax driver ilimradi tu mkono uende kinywani.lakini angekuwa home pengine angekuwa na ofisi safi na makazi ya heshima tu. ila phobia ina mfanya aogope kurudi maana hataelimu aliyopata amekwisha sahau,kwakuwa anafanya kazi zisizo za profession yake.
wasomi nchini wanapaswa kuwa chachu ya kupractice elimu yao kwa vitendo ili nchi iendelee,vinginevyo tuaishia kusubiri ready made life. mkiomba research lengo lake sio kupata suluhisho la tatizo unalo fanyia research,bali unataka ununue mercedes benz!hahaa.kwa mtindo huo hatuta endelea.hadi watu wafikie mahali wafikiri kama watu wa race nyingine duniani wanavyo fikiri.yaani wakotayari ku-risk hata afya yake ilimradi tu atengeneze jina na aache kumbukumbu duniani.lakini sis wala!!ndio maana wahindi,wachina,wa indonesia,wakorea wanatoka nyuma wanatupita siku hadi siku. mtu mweusi amejenga dhana ya kutumikishwa na race zingine kwa ujira wa kumpa mkate ndio maana hata serikali zetu zinakesha zikibembelezea misaada na mikopo.
mbona wazungu wasikufundisheni kuzalisha technology kama wao?si wanajuwa mtashindania soko!wataishia kukupeni misaada ya mashart huku wakikutawala kifikra century after century! their principle is one:-
'KEEP YOUR SLAVE PHYSICALY STRONG,BUT TAKE HIS MIND" kwa mtaji huu tuapewa misaada,mikopo n.k tunazalisha kwa maguvu wakati mentaly we depedent on them.
get up you first and me lets change our land into a green pasture!no running to abroad anymore if we are determined!tutakwenda kutalii tu na kurudi kama wanavyo fanya wao.hata black americans ilikuw ngumu sana kukubalika ktk jamii ya wazungu,lakini yote yamepita.
black colour has always been associated with failure,and we don't see any need to change that trend!do we?mataifa mengine yalianza ugunduzi tangu karne nyingi 12th AD,AU HATA KABLA lakini africa tumedumaa hadi wanakuja akina vasco da gama wanakuta babuzetu wana okoteza matunda na kuwinda wanyama wako comfortable!!! akina shaka wanauza watumwa kwa kioo cha kujitazamia,na hii ilikuwa ni karne ya 19, kweli huwezi kuona kuwa we have a serious problem?wahindi walitawaliwa ,lakini wanakuja juu kwa kasi nzuri,je sisi tunafanya nini?
kilasiku kilio tu kwa serikali!unazaa watoto 10 mwenyewe,kisha unalia eti serikali haiwapi dawa wala shule,wakati wewe mwenyewe huwajali wala kupanga mkakati kwa ajili yao!lets be serious with life and be focussed guys!individual development will lead to a collective recognition as a developed society!wasaidieni watu vijijini sio kwa kuwapa fedha ,bali kwa kuwafundisha how to think properly!to be organised in their life.bila hilo mtaishia kukimbilia nje kuwa watumwa kwa hiari vizazi hadi vizazi huku waafrica wakibezwa kwa umaskini na magonjwa,maana that is what we want to be identified with!
madini tunayo,tunashindwa kuyachimba kwa ukosefu wa vifaa na wataalam[wakati tuna UDSMA INAJISIFU KWA KUTOA DEGREE NZITO ZA MECHANICAL ENGINEERING NA MINING],tuna waita wazungu wanayachimba wana uza kisha walipa 3% ya faida,huku wana piga risasi wanchi wanao ishi maeneo ya jirani wakiingia kambini kwao,na kuwadhalilisha watoto wadogo wa kike kwa kuwafanyisha mapenzi na mbwa!huku mipro.yenu inajisifu kuwa inawapa elimu bora,ikishika na ku disco watu kwa sana! can we see this as a problem or we don't see it?tuna maji ya kutosha tena kulima kwa kumwagilia lakini tunakufa njaa na kuagiza chakula,kisa hakuna technology ya kuyafikisha maji hayo mashambani!tunakosa maji safi watu wanaugua typhoid,cholerae,n.k wakati maji yako umbali wa chini ya 15 km toka tunapoishi,kuya kusanya,kusafisha na kuyasafirisha hatuwezi,kisa hakuna technology! lakini matatizo yote haya yanageuzwa kuwa siasa na kusema sisi ni maskini hatuna pesa!
BRAIN CAN CHANGE LIFE,BRAIN CAN MAKE MONEY!

Anonymous said...

nikweli ulichosema anon hapo juu!nashangaa inakuwaje wasomi tulio nao hawayaoni mambo haya kwa mtizamo wa kuyabadilisha. mfano kunavijana wengi wamemaliza bcom hapo UDSM na vyuo vingine,lakini hata kujiunganisha wakafungua kampuni ambayo ingeweza kuomba ufadhili serikalini ili iagiza vifaa vya kuchimba madini kisasa,kisha wangeweza hata kutafuta kampuni ya nje ambayo ingewasaidia kutafuta soko na kisha ikawalipa 10-20% na asilimia iliyobaki wakalipia gharama za vifaa na kodi serikalini,kulikoni 3% serikali inayopata kwa sasa. kwanza ajira kwa wazawa zingekuwepo,fedha inayozalishwa ingetumika ndani ya nchi na huduma za kibiashara zingeboreka zaidi maana matajiri ni wazawa.lakini wanadumaa kifikra hadi matapeli wanatoka marekani kuja kuanzisha kampuni za richmond bila kuwa na mtaji hadi wanatajirika na nchi inalia na umaskini. lazima tubadilike.

Anonymous said...

Wacha kila mtu aandike historia yake. La msingi ijulikane ufyeka nyasi, kudeki choo, kulea watoto, kufua nguo kunalipa Dar/bongo kuliko kijijini kwetu ambako sanasana utalipwa mlo tuu.

Vile vile zinalipa saana magharibi kuliko afrika.

Anonymous said...

nasikitika sana kwanini nilizaliwa mwafrica,maana ku-deal na mwafrica ni kazi ngumu kuliko ku-deal na mnyama wa kufugwa.a hasa huyo mwafrica anapo kuwa ni mtanzania.maana jambo la kufanya kwa dakika 10,litageuzwa siasa na mtabishana wiki nzima na lisifanyike.ilimradi tu kiswahili kiingi na umaskini una tuuwa.
kuna mijitu imekariri kufanikiwa kuwa nilazima uende marekani au uingereza n.k. walikuwa wanakimbilia south africa, tangu waanze kuchomwa moto wameogopa.hata south kwenyewe weusi[wakoza na wazulu ]ni wachovu tu.maendeleo yameletwa na wadachi.
haya bwana kutengeza vyenu hamtaki mnataka mkatumikishwe na wazungu ilimradi mkono uende kinywani mkidai kunalipa.si ajabu hata mnaweza kubali kufanyiwa vitendo vya hovyo vya kudhalilishwa ilimradi tu hakuna anaye kuoneni kwa ajili ya vijipesa.
nakuhakikishia mzungu bora afe kama ameshindwa kabisa kuyamudu mazingira yake kuliko akubali kumsujudia black!lakini waafrica kwa kujirahisisha utadhani wamerogwa!mimi sishangai maana hata mademu wa kibongo akikutana licha ya na mzungu bali na hata mmalawi tu basi yuko tayari kumtosa boyffriend wake wa kitanzania ambaye angalau yuko poa,akakimbilia kwa mmalawi!! au kujirahisha kwa waarabu na wahindi ilimradi tu naye kajiona kawin.
sasa kwa midume nayo inaanza kuhusudu wazungu na kutorokea huko huku kwao kunawaka moto!kama zamani wanaume walikuwa walinzi na watetezi wa jamii,inakuwaje wanaume wa sasa kushirikisha bongo zao ili waifanye nchi yao mahali pa kutamanika iwe ni kitendawili?
labda ni uzembe wa kufikiri ndio unatupelekea kuwa watumwa wa kifikra.maana punda haendi ila kwa mjeredi. huenda unawacheka wapiga debu kukacha kijijini kwao ambako wangelima nyanya wangetoka kimtindo,lakini nawewe unakacha ualimu unakwwenda kubeba mabox USA ukidai inalipa!ni kweli inalipa,lakini heshima ndio tena hakuna.uhuru haupatikani hadi mtumwa agundue kuwa naye ni binadamu mwenye uwezo sawa na master wake,na anahaki ya kujiongoza peke yake na kuwa huru kama alivyo master wake. bila kuliona tatizo huwezi kulitafutia suluhu.mtaenda mkatumikie wee,nguvu zikiisha mnarudi na mlicho kifanya hakipo zaidi ya kudhalilika tu siku hadi siku mnakimbizana na polisi,wenye nyumba,uhamiaji n.k maana mmezamia.hata wengine wanakimbilia pia hapahapa africa kama botswana,namibia,n.k yote maisha tu jamani.anayetaka kwenda aende!ila mimi huko sitokanyaga kwa kubeba box,nikienda ntaenda kusoma tu au kikazi au kutalii!maisha nihapahapa bongo!wanakuja wanachuma hapa wanakwenda kuzitumia kwao sie tunaziangalia wala hatuzioni.kudadeki zetu!!!

Anonymous said...

Katika dunia hii ya globalization kazi ni popote unapoipata. Kama unataka kubaki nyumbani nenda kijijini kwenu ulikozaliwa, usiende hata bongo.

Anonymous said...

Tanzania maprof hawafundishi wanafunzi waelimike bali wajibu mitihani.Na wanafunzi hawasomi kwa kujifunza bali kujibu mitihani maana akidisco ni home.

Watajifunzaje kujiajiri wakati ajira haitishi kuliko hilo disco?

Tusiwalaumu ndugu zetu wanaosoma Tz kwa kweli hawapati muda mwingi wa kujifunza nje ya darasani.Hebu tazama kile leo migomo kwa ajili ya posho.Posho ndogo mnayopata bado mna make kwa ajili ya mambo fulani ya libeneke mtakapomaliza.C unajua ajira zinachelewa smtyms.

Nimepata bahati ya kutembelea nchi kadhaa europe na africa!U guys mnaosoma elimu ya juu Tz mnaongoza kwa kuvaa tai shingoni!ok yani mko smart sana!Conglatulations.

Personality yenu isiishie kwenye mavazi!Muwe smart hata kwenye akili na feelings zenu.
Kwanini usiwe na ndoto za kuwa Rais wa Tanzania au Waziri wa Jamhuri ya Muungano?au uwe gavana wa bank kuu!Ok kote mbali basi uwe Chief accountant wa TRA!

Wezi,wauza Unga,wahuni na wengi wasio na elimu wanawaza kwenda ulaya au america!!je nawe msomi una mawazo kama hao!

By the way uko huru kwenda kuishi popote duniani!But stay knowingly that matatizo yapo kila sehemu huwezi kuyakimbia.

Wasalaam!

Anonymous said...

sikilizeni vijana,jana nilikuwa ktk lecture moja hapa mahali ninaposoma. prof.mmoja baada ya kupiga lecture iliopkwisha alisema jambo moja ambalo lilinikuna kichwa na inka notice tofauti kati ya mwafrica na mzungu.
alisema" nchi yetu haijawahi kushindwa vita duniani na wala haitakaa ishindwe kwa halihalisi nayo ifahamu kwa sas ktk dunia hii,ila vita kuu ambayo inatushinda kwa sasa ni mmomonyoko wa maadili na hii itatumaliza kama hatutakuwa makini,maana nguvu yetu itapungua"kisha akasema jambo jingine" HUWEZI KUWA TAJIRI KWA KUNUNUA,unaweza kuwa tajiri kwa kuuza tu,na kitu unachoweza kuuza kwa uhakika ni kile ulichokipata kwa knowledge uliyo itafuta,knowledge hainunuliwi vijana,ila hutafutwa tena hatua kwa hatua,kwa kufikiri na kutenda na lengo likiwa ni kuyamudu mazingira yako na kuyatawala vile unavyotaka!kama mnataka kuwa watuhuru msio tawalika kama tulivyoishi sisi hapa duniani,tafuteni maarifa.nchi hii tume ifanya imeheshimika karne hadi karne,sasa jukumu hili nilenu kuliendeleza kwa vizazi vijavyo"
kwakuwa mwafrica pekee nilikuwa mimi,nilipiga picha ya huko home,nikapata fikra na ukweli kwamba mataifa haya makubwa yana focus ya kudumisha uhuru na heshima ya kila mwananchi wake asitumikishwe kokote duniani,lakini sisi ni kinyume,tuko radhi kutumikishwa kwa ajili ya mkate wa kilasiku,na wala hatuna mwelekeo wa kubadili trend hii.nchi zetu zikihitaji afya bora zinataka msaada,maji safi -msaada,kila kitu ambacho ni basic hakiendi bila msaada toka nje.nasasa tunajadili namna ya wasomi kukimbilia ulaya wakauze nguvukazi-kwa maneno yaleyale ya wasio na shule-MTAJI WA MASKINI NI NGUVU ZAKE MWENYEWE! hapana vijana!mimi nasema yote yanawezekana pale tu unapokuwa na nia ya kubadili mwelekeo ulio kufanya uwe dhaifu. kwenda kubeba box ulaya kutakuondolea njaa ya leo na kesho tu,ila hakuta badili maisha ya vizazi vijavyo!SASA NIMEELEWA KWANINI J.K.NYERERE watu hawakumuelewa alikuwa na lengo gani.alikuwa na malengo mazuri ktk mahali pasipo sahihi.
itakuwa vigumu sana kumbadilisha mtu mweusi kumfanya awe na uwezo wa kufikiri kujiendesha bila kutegemea brain ya race zingine!!!!!!OUR ENEMY IS IN OUR OWN MIND,UNLESS WE SIT DOWN AND DECIDE TO BE FREE FROM THAT FEAR AND MENTALITY,THERE SHALL BE NO CHANGES generation to generations.
this nightmare is haunting us,but we can conquer it if and only if we are determined to create respect of a black man on earth,but until we are not ready for this freedom,lets keep saying WHO IS GONNA GET THE DOGS OUT!!!!and our master is telling us "you are not ready for freedom" OUR ENEMY DOESN'T EXIST IN REAL,IS JUST IMAGINARY IN OUR OWN MIND,running away from our own shadow!!!
the time is now guys to make our country a promised land.no body will do it for us.

Anonymous said...

Haya mawazo ya kizalendo yanatolewa na watu amabo hawajui kutatua matatizo ya ufa. tafuta chanzo cha ufa utatue, sio kufunika ufa.

peoples migration (driving force) unaweza kuizuia au kuigeuza direction kwa kutengeneza vivutio kwa wataalamu sio kuhubiri uzalendo njaa. Hata mapenzi yana sababu. Na haya mahubiri yamefanywa na nchi nyingi lakini hayajafanikiwa.

We jifikirie wewe na ukoo wako mtaendeleaje. We unasema watu wajiajiri wakati mitaji ya kuwekeza hawana, lazima waajiriwe kwanza. Na ili upate mtaji haraka, kafanye panapolipa zaidi. Acheni kushauri watu wa-underemploy/underutilize utaalamu wao.

Anonymous said...

Kwali bwana iweje USA wamejaa wahindi na wachina halafu sisi tunalaza damu.

Anonymous said...

mtu awaye yote anayeshabikia kukimbilia kulikoiva tayari huku akikwepa kutengeneza kwake ilinako kuive wengine waje,huyo ni mwoga wa kuzikabili challenges za maisha.na hatakaa afanikiwe zaidi ya leo na kesho tu.huu ndio ukweli.
wazungu na nchi nyingine zilizo endelea walipata wapi mitaji ya kuwafikisha walipo kama hiyo sio sababu ya kiuzushi tu kujisafisha uonekane mjanja kukimbilia nje eti unataka mtaji?MTAJI WAKO NI BRAIN YAKO PALEPALE ULIPO. ukiwa baharini na hakuna meli,mmtaji wako wakukutoa baharini ni jitihada zako.sio uzubae eti lazima jahazi lije!watu wanao endekeza dhana za uwoga kwamba kwakuwa USA kuna wahindi na wachina nao wanataka kwenda wanashindwa kutambua kwamba USA nitaifa ambalo wenyeji wake ni RED INDIANS, wengine wote ni watu wakuja.na wakipiganisha vita pesa zikipungua za kulipa wastafu wao pensheni wanatumia ujanja wa GREEN VISA ili kuvutia cheap labour toka mataifa mengine wakatumikie wakati wao wanabana matumizi.sanasana ukitaka wakuajiri serikalini ni ktk jeshi ili ukafie iraki na afaghanistani.
zaidi ya hapo wanataka cream za brain,ukiwa kichwa safi haijalishi unatokea wapi,watakupa pesa uwape utalaam wako,uwe mjapan,mchina,mhindi,jew etc.
sasa unasema uzalendo sio deal je unadhani miaka yote vizazi hadi vizazi watu wawe wanakimbilia USA?hata hujiulizi kuwa resources za mataifa mengi kamavile mafuta ya DAUD ARABIA yanategemewa kuisha baada ya miaka 90,je kama hawata tafuta njia nyingine ya uchumi vizazi vyao vitaishije? au una myopic vision-mtazamo wa kiganjani wa kuganga njaa leo,ya kesho yatajiju!well ,nendeni lakini ukweli huu hauta pingika,babuzetu walizubaa leo hii sisi tunataabika na kukimbilia kwa watu,tunawalaumu wao!na sasa sisi tuzubae na kwenda kutumikia huko,ili vizazi vyetu navyo vije vitulaumu. MAANA KAMA ELIMU ULIYONAYO HAIKUSAIDII KUJIKOMBOA NA UJITAWALE MWENYEWE KTK MAZINGIRA YAKO SASA HIYO NI ELIMU GANI?yakukufanya uwe tegemezi zaidi? may be that is you!but doing this is cheating to yourself. you and i know the problem,lets face it and solve it,there is no need to alleviate it!

Anonymous said...

huwezi kuuga mbwa kwa kutegemea mavi ya walevi!tanzani tuna techology gani?hatuna!tunajisifia wanyama,milima,madini,mito,maziwa 1sawa kabisa .lakini hivyo ni natural resources tulizokuta duniani hivyo tusijisifu maana vinaweza badilika na hata kutoweka. jitokezeni basi wasomi tutengeneze matoi na electronics nasisi tuuzie mataifa mengine.
maana muda si mrefu USA watapiga marufuku kwa nguvuzote watu kutia timu kwao.sasa sijui njia itageukia wapi!ujerumani?au uarabuni?hahahaaaa mimi sina la zaidi.maana tunafundishwa kujibu mitihani kwa kukariri past papers,ukipata gamba unasubiri ajira,ikikosa unakufa njaa,na kuomba wazungu walete msaada,lakini hujui hatakuwa wengine wao ni vilema lakini wanafanya kazi kwa masaa mengi wanalipwa kidogo ila wanataka jina tu,ndio hizo fedha wanazojitolea na kuleta hivyo misaada wakati mijitu mizima umeweka viuno chini ikisingizia umaskini!NDIYO SISI NI MASKINI WA FIKRA. NA UKIWA MASKINI KICHWANI BASI MFUKONI NI LAZIMA WALA HUTAKWEPA. akili sio lazima uweumekaa darasani.

Anonymous said...

nani aliwapa mtaji akina newton,galileo,hypocrates,pavlov,mendeleev,ford,tom edson,alexander bell n.k ambao matokeo ya brain zao dunia inayafurahia hadi leo hii!jibu ni moja tu!PENYE NIA PANA NJIA. alivumvua bulb ya umeme alifanya experiment 1000 times,ndipo ikawaka. na kwa taarifa yako aliye tengeza filament iliyo ndani ya bulb ni black kama wew! sasa wew kimbia tu USA ukapate suluhu. kwa taarifa yako hata hao blacks wa USA hawakupendeni kabisa maana huwa mnakwenda kuwa dhalilisha kwa kuwasujudia wazungu kwa kazi mbovumbovu!

Anonymous said...

Kutafuta maendeleo binafsi ndo bora kabisa wakati huu wa umasikini wa kutupwa. Wataalamu wengi wanakimbia kwa sababu ya kunyimwa nafasi ya kutumia utaalamu wao. We angalia madktari wa muhimbili, wanakaa hata miezi 3, 4 bila kulipwa na wanalipwa kidogo, kwanini wasikimbilie UK au US.

We ukienda mikazini utakuta ntimanyongo roho korosho kibao. Mtu kapanda cheo basi wengine kwa waganga. Aa fulani hatakiwi kufikia kiwango fulani.

Muongezee kodi yule jamaa anakashifu chama chetu. Na utumbo mwengine mwingi tuu.

Anonymous said...

Acheni rohombaya, acheni ufarao, waacheni watu waende nchi za ahadi.

Anonymous said...

kimsingi wenzetu wametuacha mbali sana kimaendeleo! uwezi kuamini hata CHINA ambayo ni dunia ya tatu kama ss lakini wanatupita kwa kila jambo! kweli wenzetu wanakimbia ss tunatambaa! uwa nakaa najiuliza ni umaskini gani tulionao ss?
mpaka tunakaa chini kuwaabudu watu ambao wanapata maendeleo kupitia raslimali zetu!
uwa nachukia kumsikiliza kiongozi anatangazza eti tumepata MSAADA toka nchi fulani!
JAMANI WASOMI HIYO NI MISAADA AU NI FADHILA TU WANATULIPA?
mm kwa upeo wangu naona wazi hizo ni fadhila tu,ndivyo tulivyo binadamu tunapenda kulipa mema kwa mtu aliyekutendea mazuri!
WANAFUNZI waache wawe na ndoto za uko mm mwenyewe nimechoka kuishi nchi hii ya MAFISADI,NCHI YA WACHACHE,ISIYO JALI WATU WANAOWATUMIKIA!
Hata vitu vya msingi hatuypewi,jamani nchi gani hh?
kila kukicha migomo ktk secta muhimu! Mara vyuoni,mara mahospitalini,tunakwenda wapi jamani,
wao wanatibiwa UK & USA!
WACHA VIJANA WAWE NA NDOTO ZA KWENDA UKO,SABABU WANAONA ADHA YA NCHI HII.

Anonymous said...

Safi saana Kim from Tia. Ila hamna mtu anaabudu wahisani na pia china si dunia ya ttu bali ilikuwa.

Fagilia watu waende kutumia utaalamu wao kwenye soko zuri la utaalamu. Sio kukaa wangoma au kulipwa kidogo au kulipwa kila baada ya miezi mitano.

Tumechoka kuajiriwa kwa mkopo. Na kufilisiwa. Kama hutaki kuajiriwa ujuwe dunia nzima watu wanaajiriwa.

Anonymous said...

Mbona botswana wanaajiri wataalamu wetu wengi na hatusemi?

Anonymous said...

Ama kweli ukoloni umetuharibu, mpaka leo kuna watu wanaheshimu mipaka ya nchi badala ya kuchuma mali kokote!

Anonymous said...

wazungu nasoma nao hukuhuku,kazi ambazo wewe unataka kuja kuzifanya USA wao hawawezi kuzifanya maana sio za hadhi yao,sasa kama wewe na elimu yako umeamua kuidhalilisha kiasi hicho ili uonekane ni binadamu wa daraja la pili au tatu unakaribishwa sana USA ugange njaa zako.lakini kama unajali hadhi ya ubinadamu wako ktk dunia hii basi tuliza boli hapoulipo jiajiri mwenyewe. kuna anoni mmoja hapo juu au sijui kama ni ma anoni wengi nimeona point zake ni zamaana,tena kama sijakosea lazima na yeye atakuwa yuko nje ya africa na anafahamu anachokisema.maana kabla hujatoka africa utoe tongotongo usoni unakuwa unamawazo sawa na asilimia kubwa ya waliohuko hata kama umesoma. mawazo tegemezi ya kutarajia miujiza,unakihi ukipanda ndege tu basi mafanikio hayoo kiwanja!!utakapo tia timu huku hiyo dolar 100 unayo isikia huko bongo kama bonge la mshiko utaipata kwa siku au siku mbili lakini mahitaji yako yatakulazimisha uitumie iishe na usione ukubwa wake,kisha ndugu zako unaodhania ukija huku utawasaidia wataishia kukulaumu kuwa umewatosa ndio maana huwatumii pesa ,kumbe wewe mwenyewe kamba shingoni. elewa kwamba sio wote wanao kanyaga hapa USA wanafanikiwa,na kama kuna wasiofanikiwa usidhanie wewe ni mjanja kuliko wao au wao ni mafala sana hata washindwe ku-make hiyo mitaji.funga safari uje lakini ujuwe shilingi ina pande mbili,na inaweza kuangukia upande mmoja au mwingine.ila kumbuka nabii hapati heshima kwao.siku utakapo jikuta una 40yrs hujaoa,huna nauli ya kurudi TZ,na huko TZ hata nyumba ya kufikia huna, na kazi za suluba huku zinakushinda maana afya na umri vimekutupa mkono ndipo utakaa unikumbuke kuwa mimi nilikutabiria sahihi.GOOD LUCK BOYS&GIRLS!!WELCOME TO THE WORLD!

Anonymous said...

We jamaa acha roho mbaya yaani unaona wenzio wakienda ngambo wamefaidi saana, we kama unataka kukaa bongo si ukae tuu. Na haka ni ka tabia ka watz wengi walio nje. Hawataki uwafikie daraja, we mbona hiyo 100 inakutosha? Waache watu wagange njaa zao.

Anonymous said...

Isingekuwa wasomi waliosoma nje hata hiyo nchi isingekuwepo.
Tusingekuwa na walimu wa kuwafundisha walimu wetu na tusingekuwa na wasomi.
Mambo ya maisha ni sasa ndo tunayajadili kwa kuwa sisi wasomi wa TZ tunataka kukaa katika meza tukimaliza chuo kikuu.
kama wewe umemaliza chuo kikuu TZ na kazi hata TZ huna kwa nini ubaki hapo miaka mitatu unazunguka ku-bomu. Chaguo la kuondoka ni lako au kubaki.
Hii dhana ya kusema watu hawana nyumba kwa kuwa wako Nje, mimi huwa silielewi kabisa. Hawa walio nje wengi wao huwa bado ni wanafunzi . Bado wanasoma na wengi huwachukua takribani miaka sita kumaliza degree zao za kwanza hapa nje. Sasa kitendo cha kuwalazamisha wawe na nyumba au kazi nzuri katika muda wao wa kusoma eti kwa kuwa wako nje ya nchi ni kuwabebesha mizigo mikubwa ambayo sijui kama kuna wanafunzi wa chuo cha TZ wakati wanasoma huwa wanakuwa nazo( au wanaweza kuwa na) hizo nyumba.
Ukiangalia sana wanafunzi
Wengi hapa nje huendelea na masomo yao ya masters hivyo jumla kuwa na miaka minane ya kusoma. Yaani sita ya first degree na miwili ya second degree sasa iweje leo mwanafunzi huyo aambiwe awe na nyumba TZ?
Ninachosena ni kwamba tuanze kupima maisha ya nje na TZ kwa wale waliokaa huku nje na kumaliza shule zao baada ya miaka nane na kupata kazi ndani ya mwaka na sio miaka waliokaa huku nje wakifanya kazi za kulipia vyuo.
Japo nimeona pia bado wengi walioko nje wanaosoma bado wanweza kufanya hivyo vyote, yaani kujilipia vyuo vyao kwa kazi zakishenzi, kutuma fedha kwao za kusomesha ndugu zao, kujenga nyumba pole pole kwao kama walikuwa hawana , pia kuishi hapa nje kwa kuwa na gari na APT zao bila ku-boom fedha.
Usilinganishe mwanafunzi aliye nje na mfanyakazi wa TRA aliye tanzania na aliyemaliza chuo.
Linganisha mfanyakazi mtanzania anayefanya IRS hapa marekani na mfanyakazi mtanzania anayefanya TRA. Wote wakiwa na elimu sawa ni nani anaishi vizuri.

emmino said...

Hi friends!
I quite expected a great deal of discussion and comments on this topic because it is probably contraversal to every youth in developing countries like Tanzania.
I have read each comment posted against this topic and now its time for me to toss mine.
I wonder why people are trying to look just at one side of the coin and leave the other idle? or maybe you really have no idea what is like to be at United States?or people who have ever been to US have been trying harder to make you believe it's no good being in there!!!
let me tell you guys,US is US!!there is everything beautiful that you have been dreaming of and never succeeded to get them.
from the weather,her people till food are just incredible.I cant hide this feeling men,I wish I would be there for the rest of life.
moreover you can get amazing and very challenging exposure,and added to that if want to be rich stay with the rich,dont you know that?ni hayo tu mannies,jiachie

Anonymous said...

well,my ideas may look dogmatic,but i still hold on the fact that "IS VERY REDICULOUS TO START LOOKING FOR A GOOD JOB,INSTEAD OF MAKING OUR JOB GOOD! so does with our country,we should abandon such phobic ideas that we will reach nowhere if we stick fucussed in our own land TO MAKE IT GOOD like other countries which we are dreaming about to visit,instead of searching THE GOOD COUNTRY.
when shall ours be good for others to come,are we lost hope and is never? if not you and I ,then who else will do that?

Anonymous said...

nani alikwambieni binadamu anatajirika kwa kuajiriwa?after all tambueni hili,kuwa anaye kupa utajiri ni yule anaye kupa mawazo ya kimaendeleo au ya kujikwamua moja kwa moja,japo maisha ni kupanda na kushuka.USA wenyewe wanafurahi sana wanapoona watu wanaitukuza nchi yao,na nchi zote zinazokuja juu kwa uchumi huru kama china,korea,USA inazipiga vita sana.
waungwana fungueni macho jamani mbona wagumu wa kuelewa na wepesi kusahau?mrusi hapigwi mkwara na USA ,unadhani ni kwanini?sie kazi yetu kuwaza kwenda tu,kama tunavyokimbia toka vijijini kwetu na kuishia kulundikana DAR wakati vijiji vinabaki na huduma mbovu,miundombinu mibaya hata unaona aibu kujiitia kijiji chako,wakati baadhi ya sehemu kama wichita ni kukavu tu kama tabora,ila kwakuwa basi ni state na wamekufanya poa basi utakacha tabora uende wichita.bahati nzuri mimi nimezunguka nchi nyingi za ulaya na USA pia nimekaa miaka 3,amini usiamini nimejifunza jambo moja tu,ukitaka heshima jenga kwako utakuwa mtu huru.vinginevyo hayo mazuri utayapata kwa njia ya mtaji wa maskini.wazungu ni wajanja sana.yuko tayari akupe pesa ule,lakini hayuko tayari kukushirikisha kuipata hiyo pesa.waafrika sijui tulisha laaniwa ndio maana hkila unapo pata wazo kuwa jikomboe uwe huru,picha inayokuja kichwani ya kwanza ni kuwa lazima uwe ulaya au USA,AU KOKOTE TU ILIMRADI KUNA WAZUNGU!!!sipingi maendeleo wala watu kuwa na fedha kwa kufanya kazi,ila nachosema ni hiki "kwa mtaji huu wa kukwepa jukumu la kuifanya nchi yetu ipendeze' hatutafika kokote,ni kama mfungwa anaye achiwa huru lakini anaogopa kwenda home akilalamika eti si bora wamuache aendelee kuwepo jela.maana hajui ataanzia wapi kule home!lakini ukweli ni kwamba anaweza kufanya ya maana akiamua tu,ila phobia inamfanya asijiamini na anapoteza mwelekeo naonekana mjingamjinga kama tunavyokwenda kuonekana kwa wazungu.tunachekwa,kubezwa,kutukanwa,lakini tunajifanya hatusikii ilimradi tu tupate hifadhi tugange njaa.
simkatishi mtu tamaa,anaye taka kwenda njia ikowazi atakwenda atapata atakachopata,na wanaye pia watakwenda,na wajukukuu pia na vitukuu na vining'ina navyo watakwenda,ilimradi tu vicious circle of poverty which has gotten no concrete solution!
nendeni pia hata botswana,namibia,south africa,ghana n.k. maana wao pia kwao sio kubaya. sie oooh mbuga!mbuga! mbuga! hadi unakufa mbuga tu!

Anonymous said...

Mi nashauri watu kuliko kukaa wanapoteza muda kujikimu miaka miwli baada ya grad hujui hata pa kuanzaia, nenda kwenye soko la ajira utapata hata experience kama na wewe unataka kujiajiri. Maana part ya kujiajiri ni kuajiri watu wengine katika campuni yako. Unaweza ukajifunza mengi ukiwa umeajiriwa kabla hujajiajiri.

Na unaweza kuja kuwa na kampuni la kimataifa.

Tunaishi miaka sanasana 60, tunagraduate na labda 25. Miaka 35 ni michache kufanya kazi (safi bila fisadi) zisizolipa ukarudisha mtaji(gharama za kujisomesha) na faida (maisha ya familia yako na ndugu).

Huu ni ulimwengu wa utndawazi. Usibanwe na mipaka ya wakoloni, hii dunia ni ya watu woote. Usisikie wivu eti Wa-USA wanajitapa unamaindi nchi yao. Ukumbuke waswahili walisema "Tumikia kafiri upate mradi wako"

Anonymous said...

Sijaona topiki iliyochangiwa saana kwenye globu hii kama hii(topiki).

Mi naona watu wawe huru kuchagua sehemu ya kusoma, kuishi na kufanya kazi.

Tusilazimishane kuondoka au kubaki, acha iwe uchaguzi binafsi.

Anonymous said...

nani alikwambia mipaka niya wakoloni,hizo ni excuse wanazotoa watu wanaotaka kukimbilia nchi zilizotaabikia maendeleo waliyo nayo.usione vyaelea ujue viliundwa! mipaka ipo sehemu zote hata ambazo huyo mkoloni hakukanyaga kama vile israel,binadamu aliumbwa akapewa maeneo yake yanayo endana na alivyo umbwa.ndio maana mzungu ukimuweka hapo afrika ktk jua kali si ajabkupata cancer ya ngozi.na wewe ukitupwa ktk barafu la siberia au alaska wala huhukuwi round kama hutavaa vizuri.hii inathibitisha kuwa mipaka ipo na itakuwepo.hata zamani makabila pia yalikuwa na mipaka.lakini hapa swala sio mipaka kwa ujinga wanaojazwa na wazungu eti globalization huku kumbe ni njia ya wao kutanua masoko yao nanyie mnatafsiri vibaya mkidhani globalization ina act on your favour.nyerere aliwashawishi watu waanzishe south south comission wapate soko lao wakadidindisha mishipa,matokeo yake ben alivyoingia madarakani tu,haoo wakamfuata na kumpa umakamo mwenyekiti wa tume ya globalization ili auwe vizuri zile idea za kuendelezwa wazo la south south comission[sijuihata kama unaielewa].na ndicho alicho fanya ben,matokeo yake vijidhahabu mlivyo navyo vinakombwa vinakwisha,badala mchangamke nyie mnawazia eti mkatafute soko la ajira marekani. unadhani kuna mtu atakupa kazi za ofisini huko?changamkeni muache ujingaujinga muwe na mawazo endelevu ya kuanzisha kampuni zenu za kizawa.msitegemee kufanikiwa ni lazima mtaji wa fedha,mtaji ni kichwa chako mwenyewe. you can never get rich by chassing money,but you can get rich by making money follow you!and this is possible only by coming up with something which is found nowhere else except with you only as did BILLGATE.crake your head you wil be rich,na sio kwenda kuzoa takataka marekani na kuwa mlinzi au kulea watoto ukitarajia kutajirika.MMESHA LAANIWA NYIE hamsaidiki,anaye wafumbua macho nikama anampigia mbuzi gitaa. bora hata wazungu wanao tengenezeni mibunduki ya kukutawalia kisha ikizeeka wanaidample huko nyie mnaona deal mnatumia kuuwana,mara kongo,mara burundi,ilimradi tu wao wanachota dhahabu na almasi zilizo huko.vikiisha sijui itakaa vipi.maana nahisi hizo VISA watablock kisha mtajiju.mwafrika ni mwafrika tu,ubongo wake nimzito kuelewa hasa inapokuwa ni swala linalo hitaji creativity.anataka kitengenezwe aige!kisha anajiona mjanja.mimi ujinga huu umenitoka baada ya kuketi darasa moja na wazungu,wachina,wahindi,wajapani na nikawapeleka puta,nikatambua kuwa tunauwezo mkubwa tu ila fear ndio inatufanya tujione watu wa chini tusio weza.na creat ideas na experiment ambazo wao wenyewe wanazigwaya.kisha mtu anakwambia kuliko kukaa miaka mitatu bila ajira si bora niende marekani nikafanye vibaruwa.natamani nikutukane tusi la nguoni maana nahisi unatia kichefuchefu. mnaomba pesa za kufanya research badala ya kufanya problem solving oriented research, mnaishia kujaza ndugu zenu hata wasio juwa hiyo reseach ina husu nini ilimradi tu wapate pesa.kisha ma coock data ktk computer mnawatumia wazungu wanaziumia kuwatukania kwa kuionyesha dunia.mnajiita wasomi,nyie wasomi uchwara tu.semeni mmekwenda darasani lakini hamjaelimika kabisa.ukielimika kunakitu kina kupush toka ndani kikikwambia it is possible to make it!sio mnarudisha viuno nyuma na kujisifia umasikini ktk dunia hii wakati rasili mali mnazo.wanakuja wanachota wanatajirika nyie hamjui namna ya kuzigeuza kuwa pesa na assets. BORA UKIMWI UWAUE TU MAANA HAMNA CHA MAANA MNACHOFANYA KTK DUNIA HII.you are useless people used by other races for experimenting their sciences and arts,and theit theories and hypothesis,you make me feel like ican puke!!though i know you have ability but you don't realise that!! you don't deserve poverty and disshonor,but lets wait when you are ready you will make it,though iam sorry that you will be too tired and exhausted,poverty striken,hunger striken,disease striken, with a BEUTIFUL NAME which sound "HIGHLY INDEBTED POOR COUNTRIES" oh my god!poor you and me.

Anonymous said...

Nachoshangaa ni kwamba watu wanaopinga labor market force wako Dar, mbona hawarudi vijijini kwao walikotoka ikiwa wanajali jamii zao. Kama hutaki watu watafute ajira, wala hata wewe usiende jijini, rudi kule kantalamba ulikotokea tukaone kama utakubali na degree yako kuwa mhasibu wa katibu kata.

Maana kila mji wa nchi ndiyo center ya attraction ya labor na globally ni nchi zilizoendelea.

Hamsomi DS na global economics nini?

Hamjui hata theories za human movements.

Wadanganyenyi wajinga wakae wanagomea mishahara na kupigwa virungu na FFU au kuwa replaced na TPDF (kama muhimbili kuhamia lugalo maana madaktari wa lugalo wana mshahara wa kutisha).

Sisi ndege wajanja twakimbiza mabawa yetu.

Anonymous said...

we unosema madaktari wanachelewa kulipwa na ni kidogo,wanakimbilia us unadhani akifika huko us ataajiriwa kama daktari?
kila nchi ina taratibu zake za afya.umesoma tz md alafu ukafanye kazi us au uk? hiyo sahau kuna watu tele mi nawajua wamemaliza degree zao turkey wamekimbilia uingereza na huko hawakuajiriwa koz hawakusoma hapo.wanabeba boksi.wanawake wanaolewa anakuwa mama wa nyumbani.

mi naona hapo nyumbani we should find way to use our skills hujalipwa na serikali tafuta private hospitals or company work au find ur own mtaji to do bussiness.

tunakwenda shule kusoma life sio kupata kazi na mishahara tu....

Anonymous said...

Which means na hao walioenda kusomea nje wafanye kazi huko huko maana wakirudi hapa bongo hatutawatambuwa. Tutasema tuna tarataibu tofauti na huko walikosomea.

Life ni pamoja na kazi whether ni ya kuajiriwa au kujiajiri. Lazima dunia iwe na makundi mawili: waajiri na waajiriwa. We kila mtu akijiajiri si hata vikampuni vitakuwa viduchu. Lazima uwe na secretary, mhasibu, mwanasheria, dakrati, mafundi, na sa nyingine hata masagers. Kwa hiyo lazima waajiriwa wawepo, acha ubishi usipinge facts na reality wewe!!!!

Anonymous said...

mimi nilichogundua ni kwamba wachangiaji wengi ktk mda hii ni vijana wadogo tu huenda miaka 20-26 ambao bado wana fantasize maisha.lakini utakapofika wakati ukakua akili ikaja kichwani,basi hata hiyo degree unayoipata au uliyonayo kwa sasa utajuwa namna ya kuitumia vizuri.kwa sasa mtu akikwambia unaweza kusoma bilakuwa na lengo la kuajiriwa unahisi kizunguzungu maana hawaoni kabisa nini cha kufanya,na ni kwajinsi gani wakifanye.hivyo swala la mtaji ni kichwa kwao haliwaingii kabisa.anataka aajiriwe kisha awe anakwenda kupokea mshahara.
lakini kwa mtu aliye smart kichwani,anatambua kabisa kwamba principle ya mwajiri yeyote yule duniani ni kukutumia wewe kama chombo cha KUZALISHA FAIDA ILI ACHUKUWE KISEHEMU KIDOGO TU AAKUPE,huku akibakiwa na sehemu kubwa.na ukishindwa kuzalisha anakufukuza. sasa kwa wajanja hawapotezi muda kumzalishia mtu ili awalipe,ila hujizalishia wenyewe hata japo mwanzo uwe mgumu mwishowe wanafanikiwa tu.
nilipokuwa tanzania nilikuwa na mawazo ya kwenda nje kama walivyo wengi,lakini hatimaye nilipo kaa nje ndipo nilianza kuona nafasi za pasi za mipira inayopoea uwanjani bila kuwa utilised effectively na wachezaji walio ktk uwanja huo wa tanzania.
nnakupa mfano mdogo sana,mtu kama azam,bakresa,n.k vitu walivyopatia fedha nyingi ni vile ambavyo wengi walikuwa hawavioni kama ni pesa iliyo njenje tu. mfano ni ufungaji wa maji ktk paketi na chupa na kuyauza,na kwamtaji huo pesa ilikuwa njenje tu,lakini IDEA HAZIKUWA KICHWANI. Maana watu hufikiri mbali sana wakati majibu mengine yapokaribu sana na hapo ulipo,ila kwa kuwa wamekariri theory za vitabuni wanashindwa kuziweka ktk vitendo.
YOU CAN'T GO NOWHERE UNLESS UYOU START FROM SOMEWHERE. Kama kichwani hazimo hazimo tu,hata ungepata milioni za dolar bado zitapukutika na hutazifanyia chochote pia.si unaona akina kasusurara walipata dolar kibao lakini waliishia kukimbiakimbia nazo hapo mbeya hadi wanakamatwa wakiishi guest house na wanawake.lakini kwa mtu ambaye akili ikosmart unadhani angefanya hivyo?sidhanii!
OK bwana nyie zubaeni mimi nitakuja tena bila mtaji,kwasababu ninaona mipira mnayoipoteza nitaitumia vizuri mtaji utapatikana kisha NITAKUAJIRI KAMA MHASIBU WANGU OR WHATEVER utazalisha nipate faida nikulipe.au unaonaje?kisha niwe nakubana ktk swala la muda ili usiende kupoteza muda kijiweni kama ulivyozoea kusema na kufanya eti naenda kupoteza muda!!wakati TIME IS MONEY!!

Anonymous said...

Dunia imekaa mambo mawili kila wakati ili kubalansi ikwesheni. Muajiri Muajiriwa, mgonjwa daktari, askari mfungwa, mwanafunzi mwalimu, kiongozi kiongozwi, maskini tajiri. Hii ni cycle ngumu mno huwezi kuivunja.

sasa wewe amabye unataka watu woote wajiajiri, hivi hutaki kabisa kuajiri hata mtu mmoja. Ni kampuni ya mtu mmoja ambaye yeye ndiye mkurugenzi, meneja, katibu, mhasibu, daktari, mwanasheria, dispatch, fundi, mlinzi n.k. Yaani hii kampuni itakuwa lini kama haina human resources.

Kujiajiri ni best lakini watu wengi hata wanaoadvocate kujiajiri hawajui maanake.

Anonymous said...

Huyo Bakhresa wako mbona hafanyi kazi hizo mwenyewe kaajiri watu. Unajuwa kazi unayoweza kuifanya mwenyewe kwenye kampuni yako ni ile uiwezayo. kama tunavyojuwa hamna mtu mwenye fani zoote. Lazima utaajiri watu wa fani. Kwa hiyo huwezi kupinga watu kuajiriwa. Na kuajiriwa ni part ya mafunzo kwa pure graduates.

Anonymous said...

hakuna anayepinga watu kuajiriwa ,nunashindwa kuelewa nachokizungumza maana tayari umejiwekea dogma kichwani.nacho jaribu kukiweka wazi ni dhana ya watu kudhania kwamba ukitoka nje ya nchi basi tayari umefanikiwa.jambo ambalosio kweli.na wengi wanaishia kujilostisha nakupoteza muda na utaalamu waliokuwa nao au ambao wange upata huko nyumbani na kuutumia kwa maendeleo ya familia zao kisha jumla yake kupelekea nchi kuwa na watu walio ukwepa ufukara. sasa kwakuwa wengi wanadhana ya kuwa hadi aone ajira gazetini inayohitaji mtu wa qualification aliyo nayo ndipo akaajiriwe wanajikuta wanapoteza muda mwingi.
nchi nyingi za nje watu wanakuwa ni multprofessionals,na wafanya kazi tofautitofauti na kujiajiri pia huku wakifanya part time jobs za qualification walizo nazo.na nimara chache sana utasikia wanasema ooh serikali haifanyi hiki.lakini tanzania kilakitu utasikia serikali haifanyi.nje mambo mengi yanakwenda kwa bima,hii inawafanya wawe active.lakini ni watu wangapi huko tz utakuta wamekaa wanakwambia mimisijaajiriwa,sinamtaji,sinahiki.
wakati tayari ana elimu naujuzi.hichi ndicho nachokiweka bayana na sio kuwa napinga ajira.utakuta mtu anatumia pesa nyingi ambazo angefanya mtaji kwenda kulipia visa ambazo hazizai matunda hata maratano.akitarajia tu lazimaaende nje ndipo afanikiwe.
inabidi sasa watu wajifunze kutofautisha mambo na kuwa na mtizamo mpana wa maisha na sio kukariri tu kwamba mlangoni ni pale,sasa kama nyumbainawaka moto hata dirisha liko wazi bado kutoka hawezi eti mlango umefungwa.
leo hii nikija huko nikaanzisha mradi bila mtaji ili watu wazalishe ilimradi nina idea mtanipiga vita sana.lakini nikimchukuwa mzungu mmoja hapa mchovumchovu hata mnaye mzidi elimu niki mpa idea zangu ili aje aziseme basi wote mtamuunga mkono na mtazalisha kisha apate faida awalipe. hikindicho kinaniuma na kunisikitisha jinsi brain za wengi zilivyo dumaa kwa inferiority complex.hayahaya mambo yanapelekea hata mtanzania akija kuomba tender zakufanya jambofulani anaweza nyimwa akapewa mzungu ambaye labda mimi ndiye nimempa mtaji kisha nimempa deal la kufanya tender hiyo. sasa tujenge tabia ya kushirikisha ubongo na kujiamini kuwa wabunifu na wavumilivu wa kusubiri tuone matokeo ya kile tunachokusudia kufanya natunachofanya tayari sasa.sio kukimbiakimbia tu bila mwelekeo kwenda kujidhalilisha.kama unakwenda kutafuta shule ni sawa.kama umepata mwaliko na kampuni inayo eleweka ni sawa na contract inayoeleweka. sio unadegree ya b.com unakwenda kulea watoto marekani wakati unaweza kubuni idea inayoweza kukufanya uwe somebody duniani,ila unajilemaza tu.that is what iam saying.but iam not you mom or your dady,you can do whatever you want provided iam not feeding you!if you you win is you and if you get lost is you!we always have choices,and we do not plan to fail,but we fail to plan. you should know that when you do an act you create a habit,when you create a habit you create a character,and when you create a character you create your destiny!so watch out before you do what you are intending to do!

Anonymous said...

Kazi ni kupata fedha. Elimu ni kukuweka wewe kuwa na ufahamu wa mambo tu.
Lipi zuri kukaa TZ miaka minne ukiwa na elimu ya degree bila kazi au kuondoka ikiwezekana kwenda kufanya kazi za ajabu lakini ukiwa na fedha.
Mambo nchi zingine yanaenda yanabadilika sasa hivi wasomi- wakigeni wanaosoma Canada watapa uraia haraka sana na kazi nzuri wakibaki Canada.Kwa nini waje TZ.

Anonymous said...

Waacheni watu wawe huru kuchagua wanapotaka kuishi na kufanya kazi. Si lazima ukisoma bcom ufanye kazi za bikomu, umaweza kuwa mwalimu, askari, mjeshi, almuradi mkono uende kinywani. Swala la kulea miguu nyumbani eti uzalendo mi nalipinga kwa 100%. Na wanaohubiri mambo ya uzalendo ni wale wako stuck.

Anonymous said...

Nyie mnapoandika maandishi marefu mkumbuke kubonyeza ENTER ili kuwe na paragraph.Mnatuchosha kusoma

Anonymous said...

we anony wa hapo juu ,nadhani ndio walewale mnao soma kwa sauti kubwa hata ukiwa mwenyewe,au kwa kutumia kidole,na kama ni ktk computer basi unasoma kwa kutumia curcor.
halafu kama sijakosea ukiangalia mfukoni mwako basi utakuwa una tooth pick au vijikaratasi vingi tu vikiwemo salfet paper za mikono.
au unasemaje?umesingiziwa na hilo?

Anonymous said...

Kwanza kuandika komenti maneno elfu inaonyesha hujui kuwa brifu. Watu wanatoa mifano miiingi, halafu wanasema comentaz ni vijana. Waacheni vijana wawe huru sio kuwapandikiza miwazo ya kizee.

Anonymous said...

always i used to read smaller articles or reviews that also clear
their motive, and that is also happening with this paragraph which
I am reading at this time.
Feel free to visit my webpage casino poker

Anonymous said...

Everything is very open with a very clear clarification of the challenges.
It was definitely informative. Your website is very helpful.
Thanks for sharing!
Feel free to surf my homepage Play Online

Anonymous said...

Hello! This is kind of off topic but I need some help from an established blog.
Is it hard to set up your own blog? I'm not very techincal but I can figure things out pretty fast. I'm thinking about creating my own but
I'm not sure where to start. Do you have any points or suggestions? Appreciate it

my web page ... safe diets

Anonymous said...

Great blog here! Also your web site loads up fast! What web host are you using?
Can I get your affiliate link to your host? I wish my website loaded up as quickly as
yours lol

Here is my page: binary options demo account

Anonymous said...

I was more than happy to discover this website.
I need to to thank you for your time just for this wonderful read!

! I definitely appreciated every part of it and i also have you saved to fav to see new things in
your web site.

Feel free to visit my homepage: take surveys earn money

Anonymous said...

I think this is one of the most significant information for me.

And i am glad reading your article. But should remark on few general
things, The web site style is great, the articles is really great : D.

Good job, cheers

Review my web-site: legal amphetamines

Anonymous said...

Hello there, just became alert to your blog through Google,
and found that it's truly informative. I'm going to watch out for
brussels. I'll be grateful if you continue this in future. Many people will be benefited from your writing. Cheers!

Check out my weblog :: novostar spiele