Tuesday, October 7, 2008

E BWANA KUFOJISHA VYETI MPAKA CHUO KIKUU!!

Hii imetokea kwa wenzetu Chuo marafiki cha Dodoma...Maarufu kama UDOM

Kama tunavyofahamu kuwa vyuoni kwa sasa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanaendelea kujisajili yaani registration...Sasa wakati tukio linaendelea ndipo alipogunduliwa mdada mmoja ambae jina tunalihifadhi kuwa amefojisha cheti cha form four kwa sababu matokeo hayo hakuwa nayo na cheti kilionekana kabisa kuwa sio cha baraza la mitihani....

Kwa sasa kesi inaendelea mahakamani na dada huyo hana chuo tena...Pole sana dada ila usihofu ipo siku nawe utapata Elimu ya juu japo utasubiri sana.........

nilikuwa siamini kama hali hii huwa inatokea katika vyuo vikuu vyetu...ila ndio hiyo imetokea.

Kila la heri kwa mwaka wa kwanza Tanzania nzima mnaoendelea kujisajili ili muingie kwenye huu mchakato wa Elimu ya juu....Nimeona wakiendelea kujisajili mitaa ya IFM na UDSM na tunawakaribisha sana...................




4 comments:

Anonymous said...

pole sana dada..ila naamini ndio utajifunza na wote wengine wenye mtindo huo kuweni makini....
kwa nini we kilaza afu unajifojisha kuwa sio kilaza??

Anonymous said...

Ukienda makazini unaona hadhi walionayo watu wenye bachela, hasa jeshini, utatamani nawewe uipate kwa gharama zoote hata kama ulipuuza shule siku zile.

Hapa bongo fojari ndo jadi, nani asiyefoji. Watu wamefoji tarehe na vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya masomo, hati za biashara n.k.

Kila cheti cha shahada bongo kinatumika kuajiri watu wawili nadhani kwa asilimia 40 hivi

Belo said...

Mkubwa hii issue mbona hata UDSM imetokea

Anonymous said...

Hii mbona ni kawaida tu mi sishangai kuona haya yanatokea maana kuna wengi tu wako vyuoni kwa hivi sasa kwa vyeti vya kubumba tu na wanaendelea kama kawaida na matokeo yao ni mazuri tu pindi wajiungapo na elimu ya juu. Ndo hali halisi ujanja ni kuwahi tu maana hivi sasa nchini kwetu ni mwendo wa mchakamchaka tu, bora elimu ndo umekuwa mtindo wetu. Wako mbona hata viongozi kibao wa serikali walio na vyeti vya kubumba. Anyway wanaokamatwa ni kwa bahati mbaya tu. Tchao, keep on going. Apfle.