Wednesday, October 1, 2008

IFM INAWEZEKANA BILA YA MAANDAMANO

mambo vipi wakubwa!!! full shangwe ya iddi!!! au vpi wazee!,wiki mbili zilizopita niliwapa taarifa ya kuhusu sms niliyoipata iliyo kuwa inahusu maandamano ya wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) mara tuu wafunguapo chuo hapo tarehe 20 october mwaka huu, lengo ni kushinikiza uongozi wa chuo hicho pamoja na wadau husika wa masuala ya elimu ya juu nchini kutoa degree kwa wanafunzi wa mwaka wa pili na wa tatu wa chuo hicho mara wamalizapo wasomo yao hapo mwakani na mwaka kesho kutwa kama wanafunzi wa baadhi ya vyuo walivyofanyiwa miaka ya nyuma vyuo vyao vilipobadilishwa mitaala yao kutoka Advanced Diploma kwenda Degree.
mjadala wa maswali mengi ulianzia hapo huhusu uwezekanao wa jambo hilo kufanikiwa kwa kutumia njia hiyo ya nguvu ya maandamano ambayo imepitwa na wakati.
lakini taarifa rasmi na zakuaminika ambayo mdau wa blog hii ameipata na ambaye ndiye anayetoa taarifa hizi kwenu kutoka kwa waziri wa elimu wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho (IFMSO) zinasema kwamba, taarifa hizo za awali zilikuwa si za kweli bali za uzushi.
aliendelea kutoa taarifa kuwa suala la wanafunzi wa mwaka wa pili na wa tatu kupata Degree ni kweli linashughulikiwa na uongozi wa wanafunzi wa chuo hicho lakini si kwa njia ya maandamano kama taarifa ya awali ilivyoenea kwa wanachuo wengi.
Aliwataka wanafunzi wote wa IFM kutuliza munkali kuhusiana na suala hilo na kuiachia dhamana hiyo serikali yao ambayao walieweka madarakani kwa imani kubwa na kula nyingi kwani kila kitu hadi kufikia sasa kinakwenda sawa,
Haya jamani habari ndio hiyo !!!!wale wapenda maandamano kama ngosha (John Mayala) pale chuoni tulizeni mzuka mambo yatakwenda sawa kwa njia ya mezani tuu safari hii, hatutaki fujo.
Nawatakieni kheli ya IDDI waislamu wote duniani,lakini isije kuwa mwanzo wa kuanza kufanya maovu,mfungo hautakuwa na maana au vip maustadhi na maustadha,
Francis Philip
INSTITUTE OF FINANCE MANAGEMENT

5 comments:

Egidio Ndabagoye said...

Poleni sana.Migogoro kutwa vyuoni bongo,tutafika tu.Hili suala lilizua mjadala mkubwa Muccobs kipindi kile lakini mwishowe wanachuo tulishindwa.

Adv Dip kwenda Degree,kwanza naomba niseme kuwa Adv Diploma sio sawa na Degree.Pamoja nilisikia wanasema Adv dip ni equivalent na degree,hiyo ni siasa.

Hata leo hii ADA first class IFM hawezi kuchukua Masters Udsm,niko sawa?

Ukija ughaibuni ndio kabisa hawakusikilizi unaambiwa anza mwanzo bachelor.Nilisikia kuwa Adv dip zimefutwa na badala yake ni Higher Dip.Sijui elimu ya Tz inapelekwa wapi.

Anonymous said...

Hivi na AD zina class, nilikuwa sijui.

Hivi kweli AD ndiyo levo gani maana sielewi pa kuwaweka.

Mi naona kwa sababu waliingia AD kwa vigezo duni, wapewe hiyo AD na kama wanataka kizio basi wafanye mitihani ya kidato cha nne wafaulu halafu waombe upya. Hii ni kuwa fea kabisa.

au waende vyuo vingine wakachukue vizio, maana kuna vyuo vinapokea watu wana EEEEEE.

Ila kuliko kwenda Tuma bora mpigane mpate upendeleo (si haki) wa vizio vizio vyenu hapahapa, msijekuwa vizio duni.

Anonymous said...

we EGIDIO hauko sawa kabisa,kwanini usichukue master UDSM ukiwa na first class ya AD,huo ni ujinga wasomi toeni comment zenye akili! degree na advanced diploma mm sioni tofauti kabisa au hilo jina lake?
Au ujui historia ya AD? sema tukusaidie!
Wanafunzi wa IFM na nyinyi muwe na akili,wakati mnaomba AD,hizo degree hamkuziona vyuo vingine au mlikosa sifa kweli? mpaka leo mtake kugoma kudai Degree,mnawapa vicha watu kama EGIDIO wapate ya kuandika,
kwa kweli mnaonesha udhaifu wa hali juu,coz wenyewe mlijaza fom kuomba AD leo mgome kudai degree usomi wenu upo wapi?
Tubadile wasomi mambo mengine tukae ktkt Round table na kudiskasi wenyewe sio migomo nchi jirani mnawafundisha nini wakisikia chanzo cha migomo yenu? kwa kweli mnasikitisha wezangu!

Anonymous said...

we EGIDIO hauko sawa kabisa,kwanini usichukue master UDSM ukiwa na first class ya AD,huo ni ujinga wasomi toeni comment zenye akili! degree na advanced diploma mm sioni tofauti kabisa au hilo jina lake?
Au ujui historia ya AD? sema tukusaidie!
Wanafunzi wa IFM na nyinyi muwe na akili,wakati mnaomba AD,hizo degree hamkuziona vyuo vingine au mlikosa sifa kweli? mpaka leo mtake kugoma kudai Degree,mnawapa vicha watu kama EGIDIO wapate ya kuandika,
kwa kweli mnaonesha udhaifu wa hali juu,coz wenyewe mlijaza fom kuomba AD leo mgome kudai degree usomi wenu upo wapi?
Tubadile wasomi mambo mengine tukae ktkt Round table na kudiskasi wenyewe sio migomo nchi jirani mnawafundisha nini wakisikia chanzo cha migomo yenu? kwa kweli mnasikitisha wezangu!

by MDAU From TIA!

Anonymous said...

Huyo anayetaka wenzie wagome kwa ajili ya Degree badala ya Diploma haiwezekani. Kwasababu mwanafunzi anakubaliana na chuo kupewa Diploma au Degree kabla hajaanza kusoma.Sio swala la shinikizo ni mkataba.Kuweni kama wasomi na acheni siasa vyuoni!!Lazima wanafunzi tuwe na msimamo na sio kupelekwa pelekwa tu na hawa viongozi wanajitafutia umaarufu tu!!Na nyinyi viongozi onyesheni uongozi bora muache kufanya maamuzi yasiyo na msingi.