Thursday, October 9, 2008

MBEYA INSTITUTE OF TECHNOLOGY NAO WAANZA KUTOA BACHELA....!!

Hii ndio MIST(Mbeya Institute of Science and Technology) chuo kilichopo kusini mwa Tanzania na kinaaminika kuwa ni chuo bora huko nyanda za juu kusini.....Nimepata taarifa kuwa nacho kimeanza kutoa bachela badala ya advanced diploma kama walivyofanya wenzetu pale IFM...sina uhakika sana kama je kimequalify au vipi..??kwa sababu sifahamu vizuri vigezo wanavyotumia kukiruhusu chuo kutoa bachela...........

Je nao wataandamana kama IFM walivyotishia au wao wameridhika kuwa miaka iliyotangulia yaani kuanzia mwaka wa pili na kuendelea wapate zilezile diploma ambazo kwazo walisajiliwa..??

Kila la heri lakini kubwa ni kwamba wasomi tutazidi kuongezeka nchini kwetu na nchi itaendelea.................

11 comments:

Anonymous said...

Sasa angalia safu za wahadhiri wao, wengi wana AD na PGD halafu wanafundisha BEng.

Chuo hiki kilikuwa hakijajiandaa kutoa digrii.

Anonymous said...

Imefika wakati na wahandisi nao wafanye CPA ya fani yao (namaanisha mitihani ya bodi yao kwa usajili). Maana vyuo vyao viko vingi sasa hivi, 4.

Anonymous said...

we anony wa 11:19 PM ni kwamba kuna bodi ya wahandisi tanzania inayohusika na usajili wao, nao pia hufanya mitihani waki qualify hupewa kibali maalum kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli zao kitaaluma.

Anonymous said...

Ni vizuri kuwa na shahada ama kwa kila chuo kudhamiria kufanya hivyo lakini vile vile tuangalie athari zake. Tumejiandaaje kuhakikisha kila mmoja anaendeleza taaluma yake baada ya kuhitimu? Nafikiri hili ni suala la msingi kabisa kufikiriwa kuliko kukimbilia kuwa na hizi shahada ambazo hazitatusaidia iwapo hatutaandaa mazingira mazuri ya kuzitumikia. Asante.

Anonymous said...

Serikali inatakiwa kuongeza vyuo vya ufundi sanifu (OD/FTC) wa kutosha ili pawe na mawasiliano laini kati ya wahandisi hao (COE, DIT, MIST) na mafundi stadi (grades/craftsmen-VETA).

Serikali inaweza kuongeza vyuo na tija katika taalauma ya uhandisi kiwango cha OD-fundi sanifu.

Bado ncih yetu iko nyuma kihandasi.

Anonymous said...

vyuo vingine vijengwe magharibi

Anonymous said...

Serikali isipokuwa makini hawa jamaa wa Beng ndo watatumika kama/mbadala ya mafundi sanifu (kufaciliteti baina ya wahandisi na mafundi na vibarua).

Iongeze vyuo vya mafundi sanifu na bumu pia ili vijana wangi watie timu.

Anonymous said...

We anon wa October 10, 2008 12:29 PM, bodi inatowa mitihani kwa watu wenye AD tuu. Wenye bachela wanapita free. Kusajili free watu waliofundisha na wahadhiri wenye AD na PGD ni mbaya, hawajaiva kwa sababu mhadhiri ni mbichi.

Hebu soma linki hii

http://www.erb.go.tz/examinations.htm

Anonymous said...

Nuliwahi tembelea hichi chuo mwaka 2000 kwa kweli kina scenario nzuri sana ya kuwa chuo.Hata workshop zao ziko bomba.
Wanastahili kutoa bachela:Nadhni serikali sio wajinga;ni lazima wameandaa walimu wenye sifa za kufundisha bachela.
Nakumbuka kikwete ktka kuazimisha siku ya mainjinia alisema Tz tuna upungufu wa engineers naona huu ni mpango wa kuongeza wahandisi.

Anonymous said...

Kujenga majengo tu haitoshi,pia na huduma za ufundishaji nazo zidumishwe ktk vyuo vyetu vya ufundi na vinginevyo.

Anonymous said...

What's up colleagues, how is everything, and what you wish for to say on the topic of this piece of writing, in my view its actually remarkable in support of me.

Stop by my website special compilation