Monday, October 6, 2008

POLENI SANA WADAU WETU WA ARDHI UNIVERSITY!!


Ni mkasa mkubwa ambao uliwakumba wenzetu wa Ardhi University mnamo siku ya Ijumaa iliyopita....Na hii ilitokana na wanafunzi wenzetu kufanya mgomo kwa wiki nzima wakidai haki zao za msingi ambazo wanahisi kuna watu flani wanazizuia................
Migogoro migogoro vyuo vya Tanzania....na kuna tetesi kuwa UDSM hali si nzuri kwani nao pia wamenyimwa matokeo yao mpaka leo na kuna watu hawajapewa fedha za kujikimu na ni wiki ya pili ya masomo....Balaa zaidi ni kuwa hawajui matokeo yao.
Uchungu huo ndio ambao ulipelekea wenzetu kudai haki zao na walioshika mpini wakawaumiza walioshika jembe.....................
Chuo hiki cha ardhi kimewasimamisha masomo wanafunzi wa mwaka wa pili mpaka wa tano kwa muda usiojulikana.............
POLENI SANA WADAU NA NINAAMINI IPO SIKU TUTAIMALIZA HII GAME NA TUTASEMA KWA HERI KWA HAYA MAMBO YOTE...........

6 comments:

Anonymous said...

punguzeni migomo nyie vijana wa vyuoni...mnajiumiza wenyewe na hiyo sio njia ya kutatua matatizo yenu!!
tafuteni njia nyingine acheni kuwa na mawazo yaliyokufa...

Anonymous said...

kugoma tangu nchi izaliwe, hivi na usomi wenu hamwezi kufumbua njia mpya? Lakini hata sirikali ukienda kiupole itapuuza tuu, gomeniiiiii

Anonymous said...

kugoma sio suluhisho.mna viongozi ambao mnaweza kuwatumia kufanya ma zungumzo na kutatua matatizo yenu.ratiba ya chuo iko pale pale na kumbukeni kuwammeshika makali na upande wa pili wameshika mpini.kama mnaweza kuishi ingawa kwa shida mngevumilia.hasara ni yenu,wenzenu hawafundishi ila mishahara yao iko pale pale.plz think twice

Anonymous said...

wazembe wazembe wazembe sio shule tuu hata wafanya kazi wake kwanzia kwa bursar na dvc na VC MWENYEWE MZEMBE codination yao fake hadi usomi wao pia sifuri only titles in place no actions potrayed let them retire if the are worked up new fprce needed in place eyes open in every where

Anonymous said...

Kwa mwanadam mwenye busara na utambuzi atakubali kuwa huu ni ukiritimba uliovuka mipaka,na kwa hakika hatojutia muda wake atakaotumia kuliombea taifa hili la wanyonge walojaa dhuluma na maonevu na kundi dogo la wanyonyaji ambao hao baba wa taifa hayati mwl.Julius K.Nyerere alisema,"Nchi bila ya wasomi ni sawa na kumsukuma punda mwenye njaa",nasema haya yote huku nikiwatizama ndugu zetu walio mavyuoni namna wanavyohangaika kuitafuta elimu,halaf hao ndo

Anonymous said...

Hivi nyie viongozi wa Taifa hili maskini hamna huruma kiasi gani juu ya vijana hawa wa vyuo vikuu,au kwakuwa vijana wenu hawasomi ktk vyuo hivi vilivyojaa manyanyaso na ukiritimba usosemeksna,hivi mnataka kusema hamyaoni haya au kwakuwa hayawagusi,jiulizeni mfano baba wa Taifa hili leo hii afufuke akaona mlipolifikisha taifa je atawapa kipi mnachostahili?,kuweni na huruma mioyoni kwani mtaenda kuulizwa mbele za Mungu juu ya myatendayo,dunia ni mapito tuu haya tusijisahau sana.