Tuesday, December 30, 2008

KWA NINI UDOSO MNAJITENGA NA WENZENU???

UDOSO KUTOJIUNGA NA 'UVEJUTA' NI KOSA KUBWA SANA
Serikali ya wanafunzi wa chuo Kikuu cha Dodoma (UDOSO) imeendeleakufanya madudu mengine kwa kutojiunga na Umoja wa Vyuo vikuu naTaasisi za Elimu ya juu vya Umma Tanzania (UVEJUTA).Alipoulizwa hivikaribuni,Rais wa UDOSO Bw.Joramu Malimia lidai eti kutokushirikishwakatika uanzishwaji wa Umoja huo.Hoja hiyo haina msingi kabisakiuhalisia.
Umoja huo ambao hivi sasa unaundwa na vyuo na taasisimbalimbali za Umma kama vile Chuo Kikuu cha Dar s salaam (UDSM),Chuokikuu kishiriki cha Elimu Dar es salaam (DUCE),Chuo Kikuu kishirikicha Elimu Mkwawa (MUCE,Taasisi ya teknolojia ya Dar Es salla (DIT) navingine umeendesha mgomo wa kupinga Sera mbovu ya Serikali yaUchangiaji wa Elimu ya juu,Ongezeko la Ada pamoja na mambo menginemengi ambayo kimsingi hayaendi vizuri.Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ni Chuo cha Umma,hivyo haikuwa na sibusara kwa uongozi wa UDOSO unaoongozwa na Bw.Malimi kutojiunga naumoja huo.

Viongozi wa UDOSO wanapaswa kujua kwamba kujiunga na Umojahuo si Lazima kushiriki katika kila maamuzi yao ambayo wenyewe wataonahayana msingi.Kwa madai wanayogomea wenzetu hao,ni ya Msingi kabisakwani sisi watoto wa masikini ndio tuanoumia na sera hizi mbovu zaSerikali za uchangiaji wa elimu ya juu.Nina uhakika mkubwa kwamba viongozi wa UDOSO hawakubaliani kabisa nasera mbovu ya uchangiaji wa Elimu ya juu,kama vile Madaraja ya utoajimikopo yasiojali hali za watu,ongezeko kubwa la ada,madaraja ya pesaya Vitendo na mengine mengi.Sasa hiyo hoja ya kutaka mpakamshirikishwe,sijui muandikiwe barua sidhani kama ilikuwa na umuhimuwowote.Kwa kuwa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ni Chuo chaumma,Bw.Malimi na Viongozi wenzie wa UDOSO wakae na watafakari kwakina Umuhimu wa kujiunga na Umoja huo wa Vyuo vikuu vya Umma.Hii nikwa sababu wanaweza kujiunga halafu wakakataa kushiriki katika Mgomohuo unaoendelea kuliko kutojiunga na kutoshiriki katika mgomo huowakati chuo Kikuu cha Dodoma ni Chuo cha Umma na sababu za Mgomo huoni za Msingi kabisa.

Chondechonde UDOSO harakisheni Kujiunga na UmojaHuo mpya wa vyuo vikuu vya Umma (UVEJUTA) ili nasi tuunge nguvu zetudhidi ya Matatizo yanayowakabili Wanafunzi wa vyuo Vikuu vya Ummanchini.

SELEMANI TAMBWE
BA. PSPA
Chuo Kikuu cha Dodoma

2 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Naomba mkubali kutokubaliana nami katika hili. Hakuna ulazima wa aina yoyote ile kwa UDOSO kujiunga na "wenzao" hasa kama haioneshi ni kwa manufaa ya wote hasa walio Dodoma. Na pia si lazima kugoma katika kutafuta suluhisho la matatizo yenu. Kuna njia m'badala ambazo ninyi wasomi mnaweza kuzitumia kupata ufumbuzi. Bado dhana ya akili nyingi huondoa maarifa inazidi kufunikwa na maarifa mengi kuondoa akili. Mfumo wa elimu mpaka mfumo muutumiao "kudai haki zenu" unaonekana kufuata mahali ambapo pana tofauti na mazingira na uhitaji wetu. Wahanga si wote na kunakuwa na tatizo la kutoangalia manufaa binafsi ya wenye ushawishi. Ntafurahi na kushukuru kama nitaelezwa kuwa MIGOMO NDIO NJIA PEKEE AMBAYO NINYI MMEONA INAFAA kutumia. Najua UDOSO wanaonekana kama wasaliti lakini najua kuwa wana mwongozo wao na kama hauwaelekezi kufanya yale mshawishiyo kufanya hawana ulazima wa kujiunga. Kuwa chuo cha umma ni jambo moja na kujiunga na umoja wasiouhitaji ni jingine. Ndio maana hata nchi zote za "ulimwengu wa tatu' haziko katika umoja mmoja na hata matajiri hawana umoja mmoja. Kwa hiyo naamini mwapaswa kuelewa haki za UDOSO na kujiunga na kutojiunga nanyi.
Ndivyo namna nionavyo tatizo na yawezekana namna nionavyo tatizo ndilo tatizo
Blessings

Anonymous said...

Mi nahisi huu ni wakati watu tuangalie faida binafsi zaidi ya jamii. Tutaendelea.