Tuesday, December 23, 2008

KWELI ATHARI ZA MIGOMO NI KUBWA....!!

Kutoka gazeti la Mwananchi la leo.

MARA baada ya kutolewa kwa amri ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kusimamishwa masomo na kutakiwa kuondoka chuoni mara moja, mambo mawili makuu yaliumiza vichwa vya wanafunzi walio wengi. Mosi watakwenda wapi na pili wataishi vipi ndani ya muda wote chuo kikiwa kimefungwa.Kwa wakazi wa Dar es Salaam, mikoa ya jirani na hata wale wenye jamaa wa karibu mambo haya hayakuwasumbua kwa kuwa walijua nini cha kufanya. Kibarua kilikuwa kwa wale wanaotoka mikoa ya mbali na wakawa hawana kitu mfukoni.Ni mwezi mmoja na ushee sasa tangu kufungwa kwa chuo hicho uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho wameamua kujiingiza katika biashara ya ukahaba kwa kile wanachodai kupambana na ugumu wa maisha unaowakabili baada ya kukosa njia za kurudi makwao.Safari ya gazeti hili kutaka kujua ukweli wa tetesi kuwa baadhi ya wanafunzi waliofukuzwa wanajiuza mitaani zilianzia hosteli ya Mabibo.

Dada mmoja (jina tunalihifadhi) alikuja pale kuomba hifadhi kwa wenzake wanaosoma Taasisi ya Mawasiliano ya Umma na Uandishi wa Habari (IJMC) ambao wao walikataa kugoma.Akizungumza huku akibubujikwa na machozi alisema alikwenda kuwaomba wampe hifadhi baada ya kuchoka na manyanyaso nyumbani kwa mjomba wake aliyekuwa akiishi kwake tangu chuo kilipofungwa. Anamtaja mke wa mjomba wake kama sababu ya kuchukua uamuzi wa kuhama kwa mjomba wake ambaye alikuwa safarini.Huu ndio uliokuwa mwanzo wa kujua kama yapo mambo mengine yanayowasibu wanafunzi wa chuo hiki kikongwe nchini.Nilipomsaili hakusita kusema kuwa kufungwa kwa chuo kumesababisha wanafunzi wengi wa kike kufanya biashara ya kuuza miili yao maeneo mbalimbali ya jiji hasa kumbi za sterehe na burudani."Hamuwezi kuamini nendeni hata hizi baa zilizopo hapa jirani na hosteli utawakuta wanafunzi kama hamuwafahamu mimi nitawaonesha wanajiuza, wanavaa mavazi ya kubana wana weza kununua bia moja au soda kuanzia mchana mpaka jioni wakiwa wanasubiri wanaume, na sio hapa tu hata kule maeneo ya Sinza , makumbusho na Mwenge, kwa kweli hali inatisha sana nyie wenzangu msicheke" alisema kuwaambia wenzake huku akisikitika.Ushabiki wangu wa kutaka kujua zaidi hasa nikitilia maanani hii ilikuwa kazi niliyopewa na mkuu wangu wa kazi nililazimika kumuomba dada huyu twende katika moja ya baa alizozitaja ili nikajionee fahari ya macho.Alikubali na tulijongea baaz ya jirani ambalo naomba kuhifadhi jina lake.Pale niliwakuta akina dada kadhaa alini macho yangu yalituwama kwa mabinti wawili walikouwa wameva nguo fupi huku wakipiga simu na kutoa matusi. Nakumbuka mmoja alikuwa alimaka:‘"inakuwaje mwanume kama huyu atusumbue akili zetu kama angekuwa hana pesa si angesema tusije hapa, shoga nakuomba kuanzia leo usimtafute kama ataamua atakutafuta mwenyewe"Kuanzia hapa nikaanza kupata picha fulani ambayo punde tu ukweli wake ukaja kujidhihirisha baada ya yule dada niliyemuomba kunionyesha hao machangudoa aliponambia maneno yafuatayo:"Kaka umewaona watu wako uliokuwa unawataka ndio hao, hapa ni kidogo tu wewe ukitaka kuwaona wengi nenda Makumbusho ,Mwenge au Sinza kila baa utawakuta wanafunzi, wamesheheni wakiwa wanasubiri wateja wao kama hawa, watoto wadogo lakini ndio hivyo tena.”Baada ya kujionea ya hosteli nilimwomba tena mwenyeji wangu anipeleke eneo la Mwenge kujionea hali ilivyo huko.Hapa nilishuhudia idadi kubwa ya wanawake na magari.

Wanaume walikuja na kuwachagua wanawake kama vile mtu anavyochagua chungwa gengeni."Unamuona yule mwanafunzi yule kashachukuliwa masikini kama angeniona hapa sikui ingekuwaje, lakini ndio ameshaamua jamani yaani hata Jati (jina si rasmi) na yeye anajiuza kweli hali imekuwa mbaya"alisemaKwa kuwa ilikuwa usiku kiasi mwenyeji wangu aliamua kuondoka, nilimshukuru nami nikaamua kwenda kumalizia uchunguzi wangu Makumbusho katika baa moja maarufu eneo hilo . Niliyoyakuta huku ni sawa na ya Mwenge ila hapa kidogo nilipata ugumu kung’amua nani mwanafunzi nani si mwanafunzi. Hata hivyo niliweza kuwabaini baadhi baada ya kuwasikia wakichanganya lugha za Kiswahili na Kiingereza katika mazungumzo yao. Nilihisi walikuwa wanafunzi na ndivyo ilivyokuwa.Niliamua kumfuata mwanadada mmoja aliyekuwa ameketi peke yake, nilimsalimia na kuomba ruhusa ya kujiunga naye katika meza. Nikapata muda wa kurusha ndoano yangu ya kwanza.Sikiliza majibu yake “"Kaka ikiwa unataka kutoka na mimi leo tafadhali nihakikishie kuwa utanipatia elfu kumi kwa usiku mmoja , pia ujue chakula kitakuwa ni juu yako na vinywaji sawa?nadhani umenielewa kaka vinginevyo itakuwa ngumu kaka yangu"Kwa kuwa mimi si mkware na wala sikwenda pale kwa kile ambacho yeye alikifikiri kwa mara ya kwanza nilitaka kuzungumza naye mambo mengine ambayo kwa bahati nzuri alikubali kwa roho moja.

Mwanadada huyo aliyeonekana mdogo kiumri alianza kuniambia kuwa yupo mwaka wa tatu Chuo kikuu cha Dar es Salaam akisomea fani ya sheria, alisema hafanyi biashara hiyo kwa kupenda bali ni kutokana na maisha kuwa magumu“Usione hivi kaka hapa nilipo nipo katika wakati mgumu sana kwani najua ni aibu kufanya hivi lakini, sasa nifanyeje tunakaa chumba kimoja maeneo ya kinondoni tupo watu wanane na wale wenzangu uliowaona wamekaa hapa na kila siku tunatakiwa kula na kufua wewe unafikiria tutatoa wapi hizo pesa" alifafanua sababu ya kufanya uchangudoa.Kwa hali yoyote haya ndiyo matokeo ya kukaidi amri ya chuo na ile ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Jumanne Maghembe, iliyowataka kusitisha mgomo na kurudi madarasani wakati wizara ikishughulikia madai yao.Si wote waliogoma lakini mwisho wa siku ilibidi rungu la serikali kuwaangukia waliokuwemo na wasiokuwemo.Inasikitisha.

http://www.mwananchi.co.tz/

JAMANI JAMANI VIONGOZI WA WANAFUNZI HEBU TOENI FIKRA MBOVU VICHWANI KUWA MIGOMO NDIO SULUHISHO LA MATATIZO YETU.

18 comments:

Anonymous said...

Mimi roho inaniuma sana,najisikia vibaya sana kwa hali hii.

Anonymous said...

anselm,unasema huko ndio kujiajiri nilikukuwa napazungumzia?

Anonymous said...

Sawa tu hamana maana, maana mnajifanya sana kutoa dharau. Mkome mkae nyumbani kwenu huko Ngara na Sumbawanga mpaka mchoke. Tutasomesha wanafunzi wa vyuo vingine kama Tumaini, St Augustine, Makumira na vingine ambavyo wanafunzi wake wanataka kusoma sio nyinyi wa UDSM na wenzenu mnaopenda migomo.
Muuze , mfe, mkonde , shauri yenu.
Kuna watu wengi wamesoma na hawana kazi hapa Dar na wala hawapati fedha mnazochukua kila mwezi. kazi kununua MATV, MASTEREO na MASHATI YA MIKONO MIREFU na BIA za SURVEY, Mkome kabisa. N amkome tena sana. Mbaki huko huko nyumbani kwenu na mwaka kesho wawaingize wanafunzi wapyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.

Anonymous said...

Na kweli wajinga hao waliogoma , Sasa wanatuambia wanapata shida kwani walikuwa hawajui wakati wanagoma.

Anonymous said...

We annon wa December 23, 2008 11:09 PM, vipi utaweza kusomesha vilaza wawe vipanga? Nchi itaaendelea kuwa na filures. You must train the trainables. Na trainability ina kipimo:kufaulu kwanza.

Anonymous said...

Anselemu, hawa mabinti wanafanya wakati huu mgumu tuu, wale wa IFM, DIT, na CBE na sekondari za huko kati ya mji hufanya kila siku kwa mwaka.

Anonymous said...

Ni bora hawa angalau wanapata hela wakati wa kupoteza utu (dignity) wao, two birds in one: pleasure and money.

We mademu wenu mbona hata hela hapati wanapoteza utu wao kwenu bure bila malipo ila ahadi hewa za kuowana? Wangapi wameshatoswa.

Hivi hili hamlioni kiakili? uisjidai "mi nina mpenzi mmoja." Kwani mmefanya naye mara ngapi?Kumbuka hata ukifanya sex na fiance wako ni zinaa tuu. Na adhabu ya zinaa ni ileile. Msione hawa wadada wachafu saana eti kwa sababu tuu ya hizo hela wanzopokea.

Hivi changudoa anayepata wateja watano kwa siku ya jumamosi tuu kwa jumla ya matendo matano, na hao mnaowaona wasafi lakini kila siku asubuhi na jioni na boifrendi wao wapi wachafu zaidi.

Ila na nyie madada acheni hiyo, tukiomba kuwaoa siku za amani mnajidai ghali hasa sasa bei yenu mbona yazidi kudidimia? Careers will get as to hell.

Anonymous said...

KSB....eeh,sasa unafikiri kuna kujiajiri kwa aina gani kwingine kusikohitaji kujipanga,maana ulikazana kuniambia mimi ni ovyo ksbb nasoma ili niajiriwe,kuna mtu akasema kujiajiri na kuajiriwa ndo kinacholeta utofauti kati ya wahitimu wa UDSM na other Learning Institutions,kumbe sasa ndo nimetambua...kumbe wenzetu huwa mnajifunza kujiajiri tokea mkiwa bado Chuoni,aisee hongereni sana.

Anonymous said...

Sasa Blog imeanza kunoga,siku chache zilizopita nilikuwa peke yangu humu mwenye mawazo chanya,inaonekana watu wameanza kutambua sasa upi ni mchele na zipi ni pumba.

Anonymous said...

anon wa 24dec 12:04
nakubalianza kwamba boyfriend na wanaojıuza zote ni zinaa,na zinaa imekatazwa,lkn kwa kusema watu hawa ni sawa nakataa koz kwa huyu anaetembea na watu mbalimbali ni rahisi kupata sexual transmitted deseases(std) kuliko boyfriend mmoja kama ni waaminifu kweli.

hata hivyo unaweza kua na boyfriend usifanye nae sex kwani mapenzi sio lazima sex,kuna mambo mengi mnaweza kushare mkaridhiana bila sex mpaka pale mtapoamua kufunga pingu za maisha.

kuhusu hao kina dada wanaojiuza,kwanini wasirudi makwao kwa wazee wao mpaka ufumbuzi utapotokea,kwani kabla ya kuanza chuo walikua wanajiuza au walikua wakiishi wapi?ni tabia ya mtu na kutoridhika na mola alomjalia kuna pelekea kufanya mambo kama hayo,wasichana kama hao kabla ya hapo walishawahi huo mchezo naamini au hata chuo kıkıwa wazi hicho kitu wanaweza kufanya kusingizia hela haitoshi.

otherside nakubaliana na mwandishi migomo haina maana,ni waste of time.

Anonymous said...

Kujiuza kimwili ni tabia ya mtu tuu, na sioni sababu ya kuhusisha swala la kujiuza na migomo iliyotokea! Overall sidhani kama sample aliyoitumia inatosha kuniaminisha kwamba Dada zetu wote wanafanya mambo ya kipuuzi kama anavyodai.

Kama kipato ni tatizo tuseme vipi kuhusu kina KAKA?

Anatitisha ili tusiendelee kutetea fikra zetu?

Anonymous said...

wewe mwenye hii blog ni mpambe wa serikali. Usilete propaganda zako hapa kutetea serikali ambayo inanunua BMW za mabilioni huku shule za sekondari (moshi ufundi) zikifungwa kwa kukosa chakula.

Huna hata haya - najua utabania maoni yangu lakini message utaipata loud and clear. Blog nzima umewekwa anti - DARUSO messages....

peeeehhhhhhhhhhhhwwwwwwwwwww ... ona haya msaliti wewe

Anonymous said...

sidhani kama mwenye blog anaitetea serikali...mimi naona anajaribu kuadress matatizo wanayoyapata wanafunzi..keep it up mzee!!
serikali ina makosa tena sana tu...lakini bado wanafunzi nao hawatumii njia nzuri..jamani angalieni hilo!!

Anonymous said...

sidhani kama mwenye blog anaitetea serikali...mimi naona anajaribu kuadress matatizo wanayoyapata wanafunzi..keep it up mzee!!
serikali ina makosa tena sana tu...lakini bado wanafunzi nao hawatumii njia nzuri..jamani angalieni hilo!!

Anonymous said...

Anon wa December 24, 2008 4:04 PM, ndo kazungumza kisomi, kuwezi ku-infer based on one data point.

Lakini nakataa kuwa kujiuza ni tabia. Sociologically, tabia ni dynamic in time and space.

Kuna wadada wanafanya hata tabu hawana na wengine wana dhiki kweli. Hata hivyo wakati wa kawaida inasemekana kuwa wale wa CBE, DIT, IFM na sekondari zao maeneo hayo ndo magwiji.

Anonymous said...

Anon wa December 24, 2008 11:38 AM, unatetea uzinzi kwa kisingizio cha socialization. Imeandikwa, Ateteae uzinzi naye ni.....!!!

Na kusema bora ya mpenzi mmoja mwaminifu ni uzinzi tuu. Kwani huyo changu akiwa na zana wakati woote atapata wapi std?

Halafu kwa nini unataka watu wawe waaminifu wakati unajuwa walioambukizwa virusi waliambukizwa na wawapendao na waliowaamini na kuaminika?

Dawa ya mazao yoote ya zinaa ni kutoikaribia na kutoifanya.

Anonymous said...

hiyo sio athari ya mgomo na sitaki kuamini kama boycott.hiyo ni tabia tu ya watu na wanayotoka zamani,sema tu media zinapublish mambo.kila sehemu watuwanafanya hayo mabo hasa maeneo,ukifika mzumbe university u will cry sema tu watu hawaoni hayo mambo,picha za uchi ,sex ni hadharan,

Anonymous said...

Ni fikra potofu kudhani kwamba hao wanaojiuza wanafanya hivyo kwa sababu ya kufukuzwa chuo. Utafiti ulifanyika kabla hawajafukuzwa chuo na kubaini kuwa hawakuwa wanajiuza? Na kama kweli wanjiuza kwa sababu ya kufukuzwa chuo, wakimaliza chuo na wasipate kazi mapema itakuwaje?