Monday, December 22, 2008

WAKATI WA KUIMBA NA KUKIMBIAKIMBIA RAHA SAANA...LAKINI....!!!


Natuma salamu zangu kwa mjiitao wanaharakati popote mlipo....saalam pia kwa wote mliokuwa mnaimba kama sio juhudi zake baba wa taifa....salamu kwa wote mliokuwa mkitumia slogan yenu feki ya eti mpaka kieleweke......!!
ilikuwa raha sana kukimbikimbia around chuo....na ilikuwa raha sana kuimba na kukataa vipindi mkiwa na wenzenu pale chuoni.........!!
Ujinga wenu ni pale mlipokuwa hamjui ni nini na ni nani aliye nyuma ya mgomo wenu feki......!!!
Walewale waliokataa sera..haohao wanajaza fomu ya kuikubali sera..................!!
mama yangu....kweli mmekosa akili ya upambanuzi wa mambo............mlikuwa mnaona raha sana kuimba mkiwa pamoja..ila sasa kila mtu yuko nyumbani kwao na ndipo anapogundua kuwa kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe.....!!
Sasa unahangaika wewe na mama yako kutafuta fwedha ulipe urudi chuoni...........!!Ilikuwa raha sana kuimba na kutoka jasho...ila mtoto wa mwaka wa kwanza na wa pili alipoambiwa rudi nyumbani huku nauli hana mfukoni....ndipo alipokumbuka kuwa kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe....Niliwakuta Ubungo Bus Terminal wakiwa wamebung`aa na mimacho yao hawajui pa kwenda.....!!...Muwe na fikira zinazojitegemea na msiongozwe na hao wanaharakati feki wanaokuwa sponsored na watu fulani.....!!
HAYA ENDELEENI KUJAZA FOMU ILI MRUDISHWE....ILA MKIRUDI KAENI CHINI MUORODHESHE FAIDA NA HASARA MLIZOPATA....!!

5 comments:

Anonymous said...

kweli nimeamini victims wa vita siku zote ni wanawake na watoto.........!!
ukiangalia hapo juu hakuna msichana hata mmoja aliye mstari wa mbele kwenye kugoma...ila nao walifukuzwa na wakapata shida saana...vyuo muwe mnafikiria mnapoamua kufunga vyuo!~!

Anonymous said...

Aisee wee Jamaa ni noma,nimependa sana style yako ya kuongea ukweli,nafikiri wewe ni mfano wa watu bora wa kweli wanaotakiwa kuwa hapo UDSM,kwakweli watu wanahangaika sana Mwandishi mmoja wa makala katika Magazeti ya Daily News na Habari leo ameelezea bayana yaliyomkuta mdogo wake kutokana na mgomo ule,watu wamepata shida sana jamani katika issue hii,yaani kama wewe ni Mhanga wa mgomo huu na mambo yako yameendelea kunyooka shukuru MUNGU aisee.

Anonymous said...

Anselemu we shangilia tuu wenzio kupata kibano, hiyo ndo spirit ya kibongo.

Anonymous said...

Anony wa saa 12:26 sishangilii,infact nimesikitika sana jinsi vijana ambao Taifa linawategemea kushindwa kutumia busara kabisa katika kufuatilia madai yao,bado naikumbuka kauli ya Kiongozi wao mmoja(ilirushwa na vituo kibao vya Television) kuwa watagoma hata wakifukuzwa wakirudi watagoma tena,sasa hiyo ni akili au matope?

Anonymous said...

Akili ni akili tuu ipatie au ikosee, huwezi kuifananisha na matope. Hiyo ni dharau kubwa, tutakutana.