Friday, December 5, 2008

WANAFUNZI NA VIONGOZI WA WANAFUNZI MMEKOSA MEDITATION!!


Saalam Wadau,

Ninaomba kulileta hili swala nikiwa na masikitiko makubwa sana.

Ninadhani wanafunzi wengi wengi waliingia kwenye migomo bila kufahamu ni nini impact ya migomo au bila kufahamu nini wanachodai au bila kufahamu kama maombi yao yatakubaliwa au lah....!!

Lakini vile vile nadhani walikuwa wamekosa meditation ya kujua ni njia nyingine ipi wanayoweza kutumia ili kufikisha madai yao!!

Ninasema hivyo kwa sababu mnamo leo asubuhi nilipita chuo kikuu cha Dar Es Salaam na kuona wanafunzi wengi sana wakiwa wamejazana internet cafe ya hall one kuchukua form za kuikubali sera ya kuchangia elimu ya juu ili warudi Chuoni...Sasa swali ni je kama waligomea sera hiyohiyo kwa nini sasa wanajaza form za kuikubali?? Je mlikuwa mnataka likizo fupi ya kukaa nyumbani au mlikuwa hamfahamu mnachodai??..mimi naona ya kwamba mmepungukiwa upeo na mmekosa meditation!!

Viongozi nyie ndio kabisa hamna kitu kwa sababu mliwekwa madarakani kusaidia wanafunzi,lakini sasa msaada wenu uko wapi endapo matatizo mliyotakiwa kuyashughulikia kisomi na kwa busara mnayaleta kwa wanafunzi wayashughulikie kwa njia ya migomo.......mmekosa meditation na nyie..hamfai kuitwa viongozi wa wanafunzi bali ni viongozi wa migomo.....nikiwa nimefocus moja kwa moja kwa DARUSO na wengine kwa sababu hamna mlichowasaidia wanafunzi mpaka sasa zaidi ya kuwa mmewaongezea matatizo na saivi mmekaa kimya!!

wanafunzi ada walizogomea ndio hiiiizo wanalipa ??sasa mmewasaidia nini wakati saivi wanahangaika mtaani kusaka ada ili warudi chuoni..........wengine siku walipofukuzwa chuo walilala vituo vya mabasi na watoto wa kike wakalala sehemu ambazo hazielezeki na za aibu na wengine wakaanza kutafuta nauli kwa njia zisizo nzuri.....

hamna mlichotusaidia wazembe nyie,.......................................!!..na wanafunzi msishabikie tu migomo bali muwe mnawaquestion viongozi ni steps zipi wamezifuata zikashindikana ndio sasa suluhisho ni mgomo!!...........

Mwisho nimeamini kuwa baadhi yenu mlitumiwa na vyama vya siasa kuendesha migomo na mlikuwa mnalipwa kwa kila siku ya mgomo.....!!


YOU BETTER CONTROL YOUR MINDS AND MEDITATE!!

14 comments:

Anonymous said...

Moja kwa moja nakubaliana na Mdau mtoa mada,sincerely majority ya viongozi wetu bado hawajui hasa nini wanachotakiwa kufanya wao kama viongozi wetu,am sorry nilikuwa sijajitambulisha mimi ni Mwanafunzi wa mwaka wa'3 IFM,halafu kinachonishangaza sasa,viongozi wangu pale utafikiri ni mapacha na waheshimiwa wa Daruso,yaani watu wanaitisha mgomo bila kuangalia hiki tunachogomea kinawezekana kurekebishwa au tonapoteza tu muda ambao kimsingi unatuathiri sisi Wanafunzi moja kwa moja.
Embu fikiria watu wanagoma sera ibadilishwe,sisi kama wasomi tunatambua Duniani kote sera haiwezi kubadilishwa asubuhi 1,yaani leo unaleta pendekezo lako kesho asubuhi watu wanatoa version mpya ya Sera,haiwezekani...kuna taratibu zake,sasa watu wanachukua hatua ya kugoma tena kwenye some cases kuleta mpaka vurugu/kupigana kung'fu na kila aina ya uhuni wa watu wasioenda shule kisa,kushinikiza sera ibadilishwe,uliona wapi?
Haya sasa watu wamefumaniwa Library sijui wapi huko wakigombea form za kujaza kuikubali sera hiyohiyo,hii ndo nini sasa?
Na sisi Wanafunzi tuachage ulimbukeni,inabidi ifike wakati tuweze kuchambua zipi ni pumba na zipi ni mchele tena bila kuoneana haya,mimi binafsi sikubali kugoma tu ilimradi kugoma,nitashiriki kwenye mgomo ambao nitaridhika katika upeo wangu nilionao wa kuelewa kuwa mgomo huo ni logical na kuwa na uhakika kuwa results za mgomo huo zitakuwa positive,huu ndo msimamo wangu hata pale IFM.

Anonymous said...

Mi nachofahama, kwa uzoefu wangu, wanafunzi wakigoma rudisha nyumbani, halafu kaza masharti ya kurudi. Huwa wanayakubali ili warudi, halafu nawauliza mligomea nini?

Nilivyokuwa UD viongozi walipata shida saana kuniongoza kwani nilipinga migomo wazi kwa kujuwa ahina faida mwishoni.

Halafu kama kuna wanafunzi hawataki kushiriki migomo njia rahisi ya kuwashinda wengi waovu ni kuwaripoti polisi tuu.

Na wakiwadhuru wanafunzi watiifu, basi viongozi lupango bila mjadala.

Anonymous said...

MSIRUDIE KUGOMA NYIE MSO FIKIRA

Anonymous said...

WE ANSELM futa kauli yako ya kusema eti viongozi wa udsm utafikiri mapacha na wa ifm,
lini udsm wamegoma kwasababu ya test?
au unajipendekeza na udsm?

Anonymous said...

mhhh...KSB na ANSELM kwa kubishana hamjambo....!!

Anonymous said...

KSB anataka niongee tu.
Wewe soma bwana ukajiajiri ukimaliza.
Nimegundua wewe huna tofauti na wale watoto wa O'level wanaokazana kusoma Phisics,Geography na Mathematics ili waende kusoma PGM High School,ambao ukiwauliza kwanini wanataka wakasome PGM utasikia "tunataka tuwe Marubani wa KLM"

Anonymous said...

anselm,mbona sijajua kwanini umenifananisha na wanasoma PGM?

Anonymous said...

we anselemu si ulifeli masomo ya sayansi ndo ukajida uko ati?

Anonymous said...

KSB watoto wa O level always huwa wanafikiri wakisoma kwa mfano PGM basi 1 kwa 1 atakuja kuwa rubani,na yule wa PCM basi atakuja kuwa engineer kumbe anasahau hata kama atafaulu kwa kiwango kizuri namna gani anaweza kujikuta anaangukia kwenye Uhasibu au hata Teaching,ndo kama wewe sasa na sera yako ya kijiajiri unasahau kama all factors are not constant,always ceteris peribus huwa hai'apply kwenye maisha.
Anony wa 12:21 nilisoma EGM na sasa hv nasoma Banking ksbb ya kazi.

Anonymous said...

Anselemu, EGM ni sanaa/art au ati. Sayansi ni Physics, Chemistry, na Biology na wakati kadhaa Math. E siyo sayansi ni sanaa.

Anonymous said...

Anselemu, mtu yeyote anayefanya mambo bila malengo anategemea bahati (zali la mentali) ndo wewe. Japo future huwa uncertain lakini haimaanishi mtu hawezi ku-engineer future yake.

Mi sioni kwa nini watoto wa PCM wasitegemee kuwa Eng, Comp sci, Ed, etc. Kwa sababu haiwezekani mtu wa HKL, KLF au HGL akawa Engineer au MD, never, lazima arudie asome fizikia na hesabu kwanza. Hawa watoto wanatumia falsfa ya kawaida ya maisha "expectancy."

Uzuri wa PCM ni universal, you can finaly be anaybody, accountant, teacher, engineer, lawyer, etc.

Kwa hiyo kama ungekuwa unataka watu wategemee saana bahati basi ungewashauri wasome PCM ili wa-fit fani zoote.

Anonymous said...

Anselemu, japo wewe na KSB mwafahamiana, ila umewakosea wanasekondari na elimu kwa ujumla. Mbona naona kama kazi ya elimu ni fikira na ku-design the future?

Anonymous said...

Anselelemu, mi nilifikiria utasema ulisoma EGM na sasa unasomea u MD? sasa unawalaumu nini watoto wa sekondari?

Anonymous said...

Anselm, ili mradi uko IFM basi hata kama ulisoma EGM ulifeli tuu. Au hata kama point zako unaziita ulifaulu basi hukupata wani!!!