Monday, February 16, 2009

MASOMO YAMENOGA,WENGINE WAKO LIKIZO,WENGINE HAWAJUI MUSTAKABALI WAO!!

SAlam wadau,
Ninatumaini mu wazima na munaendelea vizuri na shughuli za kila siku,samahani sana kwa kuwa kimya ni kwamba shule ya UDSM imenoga,wametupokea kwa fujo sana ikiwepo matest,maassignment na mavurugu yote.
ila hatuna wasi kwani twamshukuru mungu kwa kurudi chuoni ili tuendelee kulisukumiza gurudumu la maendeleo liende mbele............

Wenzetu wa IFM wako likizo,twawatakia likizo njema marafiki,bila kusahau UDOM sina habari za MZUMBE ila ARDHI nao ndio wameruddi chuoni baada ya kukaa mtaani kwa muda wa miezi ipatayo sita,POLENI sana marafiki na hongereni mlio likizo.

Ila katika vyuo vilivyofungulia baada ya ile crisis ya mgomo kuna watu mpaka leo hawajui mustakabali wao kwani hawajarudishwa vyuoni sababu ya kutolipa ada au kutojaza fomu,kwa wale wa UDSM ambao hawajamalizia ada wameambiwa muda umekwisha warudi septemba kurudia mwaka, na wale ambao hawakujaza fomu wameambiwa wao elimu ya juu waisahau,poleni sana marafiki na laana iwarudie mliosababisha wenzetu wapatao 138 kwa mlimani tu kupoteza sifa za kuwa wanachuo,hasa hasa DARUSO mliopita,ndugu Mchibya, Owawa na Silinde damu za hao watu ziwe juu yenu!!...hawa watu hawastahili kurudishwa kwani kwa mawazo yangu ndio waliotupotezea marafiki zetu!! ufinyu wa mawazo yao ndio uliosababisha yote haya,athari nyingine walioileta ni kufutwa kwa mazoezi kwa vitendo kwa mwaka huu,yaani field....zitafanyika next year!!


mungu tubariki wanavyuo wote Tanzania......tupe hekima na tusaidie kutatua matatizo yetu kisomi,na tusaidie tulete mabadiliko nchini.....marafiki mliopotea poleni ila mungu hamtupi mja wake!!

25 comments:

Anonymous said...

Aisee hivi uko mwaka wa ngapi? Una mambo mengi ya kujifunza.

Unaongea kama katoto kadogo ka sunday school vile. Jitahidi kuongea pointi halafu siyo kulaani laani kila saa viongozi.

Hata hao viongozi wa nchi hufanya makosa.

Anonymous said...

Alaah!
Kumbe kuna watu muda huu wanapigika kwa lectures,assignments na ma'test,ooh poleni sana na next time mjifunze kutumia japo kidogo tu akilizenu zilizowafanya muwe hapo.
Otherwise Anselm nipo nakula shushu hapa nikisubiri Chuo kifunguliwe hiyo tarehe 9 nikamalizie ngwe yangu

Anonymous said...

Anselm huonekana pakizungumzwa adhabu kwa vipanga. Wakati mwengine, not reachable. hasa alipoulizwa kuwa the best of AD inakuwa sawa na degree daraja la pass negative au lower pass(yaani GPA<2.0).

Anonymous said...

poleni wadau kwa yaliyowapata.next time mujifunze,mmejipotezea muda na hakuna mlichopata!!
tatueni matatizo yenu kisomi,ona comment ya kwanza hapo juu kudhihirisha kuna watu hawapanui mawazo na kuchambua hoja.

Anonymous said...

We jamaa hapo juu kilichokuuma ni sunday school au bloger kushindwa kutoa critics zinazojenga. anatakiwa apunguze negativity na aongeze creativity.

Anonymous said...

yaani kama tz nyie ndio intellectual basi twafwa......kuanzia kwa mwenye blog anaandika kweli kama katoto ka sunday skul....
hana hoja za kuchambua na huyu anslem simlaumu ndio kwanza yuko first sem nitaongea nae akimaliza adv dip....

Anonymous said...

bloger,no problem with blogger.okay pamoja na udhaifu wake ila alichoongea ni reality!!nadhani kama wasomi jengeni hoja halafu mumtumie bloger azipost!!

Anonymous said...

Point of correction kwa Ronald.
Niko 3rd year,na nimemaliza semister ya kwanza rasmi tarehe 6/02,kwa maana nyingine nimebakiza semister 1 tu niachane na haya mambo ya underground.
Vp tunaweza kuongea au utasubiri nimalizie hii semister ya mwisho?

Anonymous said...

Pale juu nilikuwa namaanisha mambo ya undergraduate,waosha vinywa msije mkafikiri tunazungumzia Bongoflavour hapa.
Anony wa Feb 19, 9:57 mimi nipo katika hoja zote kama nafasi inaruhusu ksbb hapa lengo ni kuwekana sawa.

Anonymous said...

Kama ndo unamaliza Diploma na uwezo wako wa kuelewa ndio huu tunaouona hapa, basi elimu imeingiliwa.

Anonymous said...

Huu ushuzi unaosemwa na hiki kijinga hapa chenye mawani kinaonyesha IFM ni chuo cha aina gani. Nafikiri ndio maana visichana vyao vinapiga picha za uchi, soma ze utamu uone.

Hivi kidploma tu kinakupa kibri ungekuwa Udizm si ndo ungetubandikia mpaka chupi?

Pumbvu sana nyie magodo. Kasomeni acheni kujamba jamba humu.

Na wewe mwenye blogu hii uko Udzim lakini unayoyafanya yanatutia aibu. Fikiria diskusheni za maana acha ushuzi.

Anonymous said...

Anse, kweli utamaliza chuo bila kuiva, ikiwa uko hivi. Sikulaumu, ulikuwa na III.

Anonymous said...

ki"dploma" "kibri" "pumbvu" "magodo" "diskusheni"...aisee I can bet huyu Jamaa(Anony wa Feb 20,7:05pm) atakuwa ni Std VII leaver ambaye bahati mbaya hakufaulu na hakupata mtu wa kumsomesha private kwahiyo ukomo wake wa kufuta ujinga umeishia palepale na ndo maana amejaa "kujamba" "ushuzi" na maneno mengine mengi tu ambayo Intellectual awaye yeyote yule hawezi kuyatamka mahali kama hapa,hii inamaanisha akili yake ndo imejaa huo ushuzi anaokuja kuutamka hapa(na kwanini isijae ushuzi wakati akipata hela tu anaingia Cafe kuangalia ze utamu)matokeo yake anahama na lugha za kwenye ze utamu kutuletea huku,ana bahati sana nimeelimika na taaluma yangu hainiruhusu kuongea huo anaouita ushuzi hapa,vinginevyo real tungekoseana heshima.
Eti Diploma tu inanipa kiburi sasa kwnn isinipe wakati kwa kila hali inaonekana imenisaidia sana kuliko Mtapikaji wewe.
Anony wa 8:51,sijui kama itawezekana kumaliza Chuo bila kuiva(kwanza sijui ni kuiva kwa namna gani,unakokuongelea wewe) nimebakisha semister 1 na I have confident tht nimeiva angalau kwa kiwango changu whether U like it or not.

Anonymous said...

By the way kwanini Nyakua usiweke restriction kuchuja watu wanaoingia humu,kwanza inawezekana au haiwezekani?
Ingekuwa vema kama wote tunaoingia humu tungekuwa watu wa level fulani,hii ingesaidia hata kujenga mijadala ya kujenga Taifa letu,tukumbuke sisi Vijana ndo nguvu kazi ya nchi yetu.

Anonymous said...

Anse, kauli yako ya February 23, 2009 8:54 AM kuwa "I have confident " inaonyesha bado hujaiva. Na kuiva sio kuwa confident kuwa umeiva, kila mtu ana confidence kuwa kaiva lakini walioiva wanaonekana hasa katika uandishi wa mawazo yao.

Anonymous said...

Anselm, unafikiri kumaliza semister zoote ndo kuiva? Kipimo hicho sio kizuri. Afadhali ungetumia GPA, maana GPA ni kipimo kizuri cha kuelewa masomo yako katika ngazi hii. Pia GPA ni kipimo kama unaweza kuelewa ngazi ijayo. Ndo maana wenye first class hawafanyi PGD.

Anonymous said...

Atachuja ili kipi cha maana kibaki? Cha kwako na cha kwake? Hahahahahaha (mbavu zangu mie)

Ama kweli siku hizi kila mtu ni msomi kama discussion za humu ndani ndo zinaonekana kuwa na mtazamo wa kujenga mustakabali wa nchi

Anonymous said...

Nimesoma sana maoni yako wewe unayejiita Anselm, kwa kweli hustaili kujipa hadhi ya usomi.

Sikunyanyapai kwa saabu tu uko IFM ila akili yako inaonyesha kiwango cha mwisho kabisa katika uelewa wa mambo.

Anonymous said...

Anse, "class pass negative" inakusubiri

Anonymous said...

Inaonekana humu ndani ili mtu uonekane umeiva au una hadhi ya kisomi ni lazima uwe unaandika terminolgy kama za "ushuzi,"kujambajamba" na zinginezo zenye kufanana na hizo.
Sisi wengine hatuwezi,ni afadhali tuonekane hatujaiva hivihivi.

Anonymous said...

aiseee kama anselm uko last sem basi kazi ipo tanzania,comments zako zimeonyesha ni jinsi gani ur not educated......kuwa educated mind u its not all about scoring highest GPA hell no

Anonymous said...

Hii blog ni ya kibinafsi ile mbaya,watu wa Mlimani mnaidominate matokeo yake ni kuwapiga vita watu wa Higher Institution nyingine Anselem pamoja comment zake nyingine za ajabu kuna wakati anaongea vitu vya akili lakini hakuna hata wakati mmoja mlioappreciate na hii ni kwasababu wakati wote nyie mnataka kujikuza hata kama hamkuzik.
Badilikeni

Anonymous said...

Anony wa Feb 26, 2:11pm unasoma wewe? U must have been one of the all time best students in your class ksbb toka nianze kuingia kwenye hii blog sijawahi kusoma comment ya muelewa hata mmoja wa kiwango chako.
Wadau that's the reality,humu ndani ukitaka watu wakusifie una akili,msomi,muelewa,umeiva,utapata GPA nzuri basi ni lazima usifie watu wa UD regardless matusi wanayoyaandika baadhi ya hao wana'UD humu ndani.
Watu wengine hatuwezi kukubali mambo haya.

Anonymous said...

Anse, sidhsni kama hii ni sehemu ya kupeana sifa. Kama ndo unachokitafuta basi umekosa. Mbona hata wewe huingia humu kukandia vipanga?

buy review literature said...

It is not everyday that I have the possibility to see something like this.