Monday, August 25, 2008

KAULI YA SPIKA SITTA!!


Wadau hebu turudi kwenye siasa kidogo!!
Mnamo Alhamisi iliyopita baada ya Rais wa Tanzania kumaliza hotuba yake bungeni Spika Samwel Sitta alipata nafasi ya kumshukuru rais......
Alisema kuwa inabidi kuweka kando haki za binadamu katika kuwashughulikia watuhumiwa wa Ufisadi hasahasa swala la EPA(External Payment Arreas).... Hii ilitokana na Rais kusema kuwa wameongezewa muda mpaka oktoba 1 wawe wamerudisha fedha hizo benki kuu lah sivyo watafikishwa mahakamani!!
Je kama msomi unaona kuwa Spika alikuwa sawa??..Au alikuwa anamrekebisha rais wake??..Wewe unaonaje,je Rais yuko sawa katika hilo swala??...Spika yuko sawa?....
Hebu toa maoni yako hapa chini na uongezee kuhusu maswala mengine aliyozungumzia Jakaya Kikwete!!

4 comments:

Anonymous said...

siasa mchezo mchafu!!
wanasias bongo kila siku kuonge pumba tu...
kwaiyo hiyo kauli ya sitta ilikuwa pumba kwa sababu rais yuko sawa...
na hii itasaidia fedha zote za EPA kurudi...asingewapa muda wasingerudisha na kama wangepelekwa mahakamani ndio ingekuwa mwisho wa mchezo.

Anonymous said...

comment ya kwanza, nakuomba uishie hapo kama unasoma maana ukimaliza utakuwa haribifu bora uwe mkulima itasaidia huna mawazo endelevu. ukitumia hiyo busara shule utaishia kurudia mitihani na kuandaa migomo tu. ok

Anonymous said...

Mh spika, alijaribu kumueleza rais hali halisi inayoendelea katika nchi za Asia ambazo kwa sasa zinamafanikio makubwa sana katika mifumo ya kiutawala na kukuza uchumi kwa haraka sana kiasi kwamba zinatishia mataifa makubwa. Mie binafsi ni mtanzania ambaye niko masomoni katika moja ya nchi hizi za Asia ni kweli kabisa hawana msamaha kwa kiongozi yeyote ambaye anahujumu uchumi wa nchi, pia umakini katika mikataba ya serikali, unyeti wa utawala wa sheria, uhuru wa taasisi za kuzuia rushwa ni mojawapo ya mambo ambayo yanazingatiwa sana na ndio kipimo cha wananchi kwa serikali wanazozichagua.Spika alijaribu tu kutumia busara kwa kuwa alikuwa anaongea na raisi maana yake ilikuwa anamuonya rais aache kukumbatia marafiki wanaohujumu serikali akiwa na maana ya kuachia vyombo husika viwashughulikie kwa kufuata sheria za nchi.

Anonymous said...

vyuotz.blogspot.com is very informative. The article is very professionally written. I enjoy reading vyuotz.blogspot.com every day.
quick loans
payday advance