Tuesday, August 19, 2008

WELCOME KING MSWATI TO BONGOLAND!!


Kama mnavyoona mfalme Mswati wa Swaziland akitoa salamu kwa Watanzania waliofika kumlaki uwanja wa ndege hapo jana!!
Nadhani wote mnafahamu lifestyle ya mfalme huyu...naomba mtoe maoni yenu hapo chini...je yuko sawa au hayuko sawa??
Nadhani wasomi wote tunafahamu kuhusu dunia ya leo inavyoenda na kwamba kuoa wanawake wengi kuna hasara na faida zake... ina maana mfalme haoni hayo!!
Pale uwanjani kulikua na mzee mmoja aliyeshuka naye alikua akimfuata pembeni akitoa maneno ya kumsifia mda wote tena kwa kupiga kelele!!
Alikuja pia na mke mmoja kati ya wale kumi na tatu alionao pia alikuja na watoto wake wawili...na kila mwaka anaongeza mtu!!
Je ni sawa afanyavyo na yungali kijana mdogo??
YOUR COMMENTS FRIEND...LAKINI KWA UPANDE WANGU YUKO RIGHT KABISAAA....SABABU NDIO MILA YAO BWANA!!

11 comments:

Anonymous said...

Guys mnajitahídi,keep it up

emmino said...

Cant believe that is the same Mswati I have been hearing about.
I understand many of u who will read this article have ever come across stories about life style of this man. I hardly believe he is the one in the posted picture. Being aware of his manner of life,how can he be healthy like that?
Mswati is an international player,he is good at the game more than any one you have ever seen,read or heard about, if I try to compare his women with a population group then it's equivalent to all students at university of dar.Can you imagine that?one man to manage thousands women!now that is quite typical of him to handle them and he finds much pleasure to do so.Despite his age,responsibilities and being an international figure he doesn't seem to care less about what he may look to them,you can see him smiling in the picture,duh!how eccentric is this man?
now being an expert player isn't a big deal as it can seem after all,but the problem
arises as how do these awkward and dirty behaviors affect Swazi people?
The guy uses National resources to invest in his behavior extensively,last year he placed a special order at Benz company of 25 expensive new brand cars for his chicks and delivered them by plane to Swaziland from Germany,and he used the government funds simply because he is the president.
the president is educated but he is not intellectual that's why he doesn't change his bad characters in spite the fact his habits jeopardize the country's economy
As a suggestion African countries should reevaluate the traditions and norms of their lives so as to make their ways of life up to date and beneficial for their welfare.
kwa haya machache ningependa kuwakilisha kwa spika ili nipate mwongozo

Anonymous said...

Watu wengi wanaompinga Mswati ni kwa sababu ya mfumo wa mawazo usio huru kwani umejengwa kukidhi mafundisho ya kibiblia kuwa ndio sahihi tuu. Japo kuna shahidi nyingi kwenye biblia zinazoonyesha mitala mf. Abraham (watatu),Jacob/Israel (wanne), David (watatu), Solomon (alfu)n.k.

Kama vile kila jamii ina haki ya kutunza, kuendeleza, na kulinda mila zao, jamii ya Mswati pia.

Kwa sababu hii ni aina ya demokrasia yao na watu wameridhika, basi waachwe wajiamulie life style.

Sidhani kama utamaduni wake unadhuru maisha ya mtu kama zilivyo mila ziitwazo potofu mf. kutahiri mabinti, n.k.

Haya masuala ya kuowa wengi ni makubaliano kati ya wanandoa wenyewe na walioridhia. Hata makabila ya kibongo mengi yanaruhusu. Kabila langu ndo usiseme, babu yangu alikuwa nao saba, baba 6 mimi bado nafikira. Ndio maana hata serikali ya TZ ya kisekyula haiingilii.

TUDUMISHE MILA ZETU na tuvumilie mila za wengine, kwani hata zetu zinaweza kuwa zinawaudhi wengine lakini wanavumilia ndo maana hatusikii kitu.

Anonymous said...

kuwa msomi haina maana kuwa hustahiki kutunza mila zako zaid unapaswa kuziheshim.kwa upande wa kina mswat kwa mila zao yupo sawa ishu hapa ni kwamba awe na uwezo wa kuwaridhisha wanawake wote hao pasitokee mmoja wapo akalalamika kuwa haridhishw ikitokea ivo basi izo mila hazifai lkn kwa upande wangu had sasa sijasikia malalamiko ina maana kuwa wanaridhishwa na utamaduni wao kwaiyo yupo sawa.ila kwa upande wetu ss waislam mwisho wa kuoa ni wanawake 4 tu.

Anonymous said...

WELCOME KING MSWATI AT BONGOLAND!!

Replace that AT with TO, Hii Ni Blog Ya wasomi Bana, au sio!?

BooSt3D.

Anonymous said...

Hongera Hongera students! Emmino it is the same King Mswati you have been hearing about. I agree being an expert player is no longer a big deal.Thank God most Tanzanian women agree with Swazi women he is a nightmare! Can you imagine Mwalimu or Mkapa promoting him? look at the picture,poor JK what an image! Bet you RA and Lowassa must be laughing. They are having a ball at his expense. What message JK is trying to give to women, but who cares he is the King!

Anonymous said...

kweli huyu ndie mswati niliyekuwa nikimsikia?
ni kijana, mtanashati pia aonekana mwingi wa furaha, tabasamu nk...
na hiyo ni moja kati ya sababu nyingi ambazo msichana au mwanamke yeyote kama mimi atavutiwa nazo....
nadhani jambo moja ambalo angetakiwa kuzingatia ni kuepuka kujichagulia vigoli na kuwaingiza kwenye himaya yake...tena mbaya zaidi kwa kutumia mfuko wa serikali otherwise to me its ok.


lilian.

Anonymous said...

Kuna watu wanaonyesha hawana ufahamu wa uongozi na socialization. Kuwa kiongozi unatakiwa ku-accomodate watu woote almuradi sio criminals.

JK kafanya kosa gani, kwani huyo Mswati mbona huenda hata ulaya na amerika na kupokelewa vyema.

Halafu watu msichanganye dini na mila, mtu kama ameamuwa kufuata mila zake mwache. Haya masuala ya wakristo wanaruhusiwa mmoja tuu na waislamu wanne, nani kakwambia yeye afata dini hizo?

Mengine eti anajichagulia vigori, he ulitaka achaguliwe na nani? kila mwoaji huchaguwa mwenyewe. Halafu vigori wenyewe wameridhika na wanapenda hadhi ya umalkia. Hawajalazimishwa, tena wengine wana degree. Wacha pia serikali ienzi familia ya raisi wake.

Kwa sababu jamaa huyu huoa mabikra tuu, na siku ya kuowa wanakuwepo mabikra wengi wanaowinda umalkia ambao huchagua mmoja tuu, wanume wanotaka kuonja ladha ya bikra wangekwenda kuoa wasiochaguliwa. Namaanisha mfalme akishachaguwa wake, na sisi tunaanza kwani tunajuwa hawajaguswa. Si gharama kubwa, waweza kwenda hata kwa basi.

Anonymous said...

kuna mila zinapaswa ziendelezwe na kuna mila ata ukiziacha hazileti hasara kwa jamii.ata kama ni mila za kwao kuoa wake hao tele haimaanisha kama akioa mmoja ndio kuna kitu kitaharibika.

na kama yeye nikigezo kwa raia wake anawafunza nini wananchi wake?yeye anao uwezo kwasababu yupo madarakanbi sawa!lkn kuna wananchi hata uwezo hana wa wake wengi lkn kwa kua mila inahurusu anaoa na wanawake na watoto ndio wanahangaika.tabia hii ipo ata hapa kwetu tz.kuna baadhi ya vijiji machifu wana wake wengi na watoto ata idadi hawaijui na kuwashuhulikia yeye si kazi yake isipokua ni ubwanyenye.

mi naona si mila nzuri inopaswa kuendelezwa.tuendeleze zile zenye manufaa kwa jamii.

Anonymous said...

Acha mawazo yanayoridhisha dini wewe.

keyala said...

weel, si uongo. mimi daima napenda kuandika kwa lugha moja na sipendi kuchanganya lugha. Kuandika kwa lugha moja tu na ukaeleweka haimaanishi kuwa haujasoma. Sasa wale wanafunzi wanaofikiri kuwa wanajua lugha hasa ya kiingereza nawaomba sana wanapoandika basi waandike kitu kinachoeleweka.
Andikeni kwa uhakika jamani na siyo bora kuandika tu!
Nina wasi wasi sana kesho utakuwa na viongozi wanaotaka kufanya mambo nusu nusu tu au kupata mambo kiurahisi ndo hapo wanapoingia katika UFISADI!!!