Wednesday, September 10, 2008

UNAJUA KINACHOENDELEA UDSM KWA SASA??

Ni machungu tu kwa wale watoto ambao ni kutoka kwa familia zinazoishi chini ya dola moja kwa siku!!
Hii ni kwa sababu tarehe za suplementary zinakaribia na hawajapata matokeo yao na wameambiwa bila kumalizia ada wanazodaiwa hawatapata matokeo yao...Hii inasababishwa na matokeo yao ya means testing ambapo inatakiwa baadhi ya asilimia walipie wao!!
sijui itakuwaje lakini vijana wamekata tamaa sana ...na hawataweza kupata fedha zao za kujikimu kwa sababu hawana matokeo na bodi ya mikopo haiwezi kumpa fedha mtu asiye na matokeo....
mh!! Sijui itakuwaje??

8 comments:

Anonymous said...

Kwakweli hili linasikitisha mno. Ila ni changamoto kwa chuo na bodi ya mikapo halikadhalika. Kama kweli chuo kipo tayari kupoteza wanafunzi kwa sababu tu bodi ilifanya makosa na uzembe kuwatathmini wanafunzi vibaya.

Pia bado nao kama kweli wana haja ya kuwasaidia wanafunzi basi hicho ni kipimo kimoja wapo wanaweza kukitumia kwa siri. Kwani mwanafunzi/mzazi hawezi akabania hela wakati matokeo yake/mwanae hayajui.

Anonymous said...

Nyie waambieni hawa CCM wahudumie jamii. we taifa masikini hivi unadai gharama za masomo. Serikali inatakiwa ilipie wanafunzi woote ghrama.

Anonymous said...

Kimsingi utaratibu wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu bado haupo sawa!
kwa mfano nimemsikia Rais wa UDSM anasema kuna mapacha wawaili wapo faculty moja lakini wamepewa mikopo ktk viwango tofauti mmoja B na mwengine C! LAKINI watoto hawa ni mzazi mmoja,uwezo wao kifedha upo sawa! sasa hiyo RE MEANS TESTING ni hipi wasomi?
kama serikali imeshindwa kutoa haki ya msingi kwa raia wake ni bora waibinafsishe hiyo bodi ya mikopo!
kwa sababu watu wanakopa na watarejesha hata kwa riba,cha msingi mtu usome kwa raha,sio mara mgomo kisa fedha zimechelewa,hiyo ni elimu gani wasomi ya kugoma goma!
mwisho nawapa pole wenzangiu wa UDSM,ila mtambue viongozi wenu wanawatafutia ufumbuzi! naamini yatakwisha!

Anonymous said...

Pindueni serikali

Anonymous said...

You guys are always whinning, and want all the benefits all ways.
Pesa mlishapewa mkasaini mikataba kwamba kuna sehemu fulani ya kulipa nyinyi wenyewe.
Sasa hamtaki kulipa hicho kiasi mlichosaini mtajilipia na mnataka muone matokeo ya Supp zenu bure na mnataka kila kitu kiwe sawa na haki. Basi mlipe la sivyo mfukuzwe tu , then atajiunga msomi mwingine, mkipata fedha ya kulipia mtarudishwa na kuanzia mlipomalizia.
Wenzenu wanaosoma nje mbona wanajilipia na ndio maana wanafanya kaziza kuosha vyombo migahawani na bado wasipolipa wanakosa status zao na kuondoshwa chuo, nyinyi mnataka bure tu kila siku.

Anonymous said...

ivyo nyie kwanini hizo pesa za mikopo hamzitumii kulipa hiyo ada ilobaki badala mnaishia kutumbua na kutanua?

matokeo yake ndo hayo sasa kama una akili vyema hiyo pesa ya matumizi ungeitenga ukalipa hiyo amount ilobakia bila kumshirikisha mzee.

lakini wanafunzi wenzangu mnapenda kutanua bila kujali umuhimu wa hizo fedha na naweza sema kwamba unashindana na serikali kwanini haikulipii 100 persent?

ni lazima tufikirie serikali ina mambo mengi ya kufanya,na lazima tuwe na malengo sio kila kitu utegemee tu...abebwae hujikaza na mtumai cha ndugu hufa masikini na dhani iko wazi

Anonymous said...

Kama serikali haioni umuhimu wa kusomesha raia wake basi ipigwe chini tuu. Migomo imetuchosha. Nchi haina miundo mbinu muhimu ya kutosha ya kufanya mkulima amlipie karo mtoto.

Nawe unasema mikopo yakula ndo walipie karo sasa wenyewe wafe njaa?

Anonymous said...

apo hakuna kufa njaa,eti mikopo ya kula,pesa ya pombe mbona inatoka humo,wikiendi kwenda disco na vimwana ni pesa ipi mnotumia? ingekua ni pesa ya kula tu basi inatoka na ya kuripia karo,if na ya kufanya mambo mengine unayoyaona we ni muhimu kuliko masomo yako endelea kugoma na muda wa kuepo chuo uzidi mrefu bila kumaliza hapo....

acheni kushindana na serikali,nasi pia wanafunzi tunaishi kwa hiyohiyo mikopo ya serikali na karo tunalipa na kuishi tunaishi.

tumechoka kufosiwa kugoma na watu wachache ambao wanahisi mgomo ndio suluhisho la tatizo lako.

tupo tunotaka masomo yaendelee lkn eti kwa kua kikundi fulani tu kimeanzisha mgomo na kuchelea threats zao inatufanya turidhie.ukweli tunataka peace vyuoni tatueni matatizo yenu kwa njia ya peace hatutaki migomooooozzzzz!

PUSSYCAT