Wednesday, April 29, 2009

UJUMBE KUTOKA KWA MDAU ANSELM!!

Hello,
Tulifikiri baada ya Test na end of semister examinations kumalizika Mzee utarudi kwa kasi na nguvu tele katika kuindeleza hii blog yetu,lkn tunashangaa kulala kunaendelea,inakuwaje Mkubwa?

Anyway naomba utundike hii kitu kwenye hii blog yetu ili wanajumuiya wapate ujumbe,hii ni katika kuambiana ukweli Kaka,atakayechukia na achukie.

TABIA SUGU ZA WANACHUO
1.Hupenda kwenda baa na kumbi za starehe kuliko Lecture na Semina.
2.Hushinda room kuliko Library.
3.Hufahamu mitindo ya mavazi kuliko Module.
4.Huogopa CARRY,SUP na DISCO kuliko dhambi.
5.Hufahamu waziri wa mikopo kuliko wahadhiri.
6.Huudhulia birthdays,harusi na starehe weekend kuliko Ibada.
7.Hutoa zawadi kubwa kwa boyfriend au girlfriend kuliko kwa yatima na wajane.
8.Hulinda ATM Cards na PENZI kuliko DESA na VITABU.
9.Wapo makini na ratiba ya BOOM kuliko UE.
10.Wanapenda haki ila wanakosa mbinu sahihi ya kuzipigania.

Ni hilo tu kwa leo.
Anselm Mwenda

DUNDULIZA DAR-ES-SALAAM
dundulizanselm@cats-net.com
Tel: +255 22 2126676
Mob: +255 713 238627.

"Samahani wadau kwa kuwa kimya ni vijimambo flani flani vya kukaribia kumaliza shule ndio vinavyochanganya kichwa kwa sasa hivi" William.

1 comment:

Anonymous said...

Anselm umenena kweli ila hizi tatu haziko kwa wanachuo tuu


4.Huogopa CARRY,SUP na DISCO kuliko dhambi.
(hata wfanyakazi huogopa kufukuzwa sababu ya kufukuzwa, humuogopa bosi kuliko Mungu)

6.Huudhulia birthdays,harusi na starehe weekend kuliko Ibada.
(si wanafunzi tuu hata watu wa kawaida na viongozi, kwa sababu sehemu ya ibada inatisha kwa masuala ya jehanamu lakini kwengine ni kula fun)

8.Hulinda ATM Cards na PENZI kuliko DESA na VITABU.
(fedha na penzi ndo malengo ya kazi ukishavipata unahangaikia nini? Hata kwa wafanyakazi wa kawaida, ndo maana ufanisi huwa haukui kazini mtu akishakuwa na fedha)