Wednesday, September 17, 2008

THE LETTER FROM MY FATHER

Mwanangu mpendwa,
Niligubikwa na furaha isiyo na kifani nilipowasiliana nawe,baada ya kimya cha muda mrefu.Mimi na shughuli zangu na kufanya mambo yale yote, kama ujuavyo,Mwananchi anayotarajiwa kufanya nchini hapa.Ni hivi karibuni nimerejea nyumbani nikitokea London, Uingereza,nilikopelekwa kufanya kazi zilizohusu masuala kadhaa ya kiserikali, majadiliano kuhusu masuala ya fedha na kadhalika,
Ni kutokana na safari zangu nyingi za kikazi,ndiyo maana nakosa muda wa kukuandikia.Lakini, hata hivyo, nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kutafuta jinsi ya kuwasiliana nawe kuanzia sasa.
Bila shaka utafurahi kusikia kuwa kaka na dada zako huku hawajambo na wanakusalimia sana.Kama ilivyo kwangu, naona wameridhia uamuzi wako wa kurudi nyumbani mara utakapo hitimu masomo yako.utakapofika, ndipo tutakapokaa pamoja na kuamua muda utakaotaka kukaa hapa nyumbani kwako.
Barrack, hata kama ni kwa siku chache kiasi gani lakini ni muhimu kwako kuwafahamu nguguzo, vivyo hivyo kujua kwako ni wapi.Nakutakia kila la Kheri na nisalimie Mama yako,Tutu na Stanley.
Natarajia tutawasiliana nawe muda si mmrefu.
Baba yako.

Hii ni barua kwa Rais mtarajiwa wa Marekani (BARACK OBAMA) kutoka kwa Baba yake mzazi BARACK HUSSEIN OBAMA SR aliyomwandikia kijana wake kumtaka aje nyumbani (KENYA) kupajua anapotokea na kuwajua ndugu zake waliopo Kenya.Kama kuna kitu cha muhimu ambacho Mzee Obama (mzazi) angejivunia kama angekuwa hai hadi sasa, basi ni Damu yake hii ambayo ina asili ya kiafrica aliyoizaa, Damu hii inataka kuleta mabadiliko ya kihistoria katika nchi hiyo ya Marekani, mshikaji nia anayo kweli,uwezo wa kufanya hivyo anao ,hilo hakuna mtu asiyelijua, ushahidi tunaoendelea kukuona jinsi anavyowachachafya wapinzani wake katika chaguzi za awali na kwenye campaign zake za kufa mtu ni kielelezo tosha kabisa!!!!!!!!!!!!.
Nini kitatokea, tusubiri uchaguzi mkuu ambao unafanyika November mwaka huu kuona kama kweli ndoto ya Mwafrica huyu mwenzetu zinatimia..............
Francis philip

No comments: