
Kwa nini basi watu hawana matokeo??...kama nilivyowahi kuripoti siku zilizopita ni kuwa matokeo yao yalifungiwa kutokanana wengi wao kushindwa kulipa ada wanazodaiwa....yaani kumalizia asilimia ya ada ambayo bodi haijamlipia mwanafunzi..........
Nilivyoongea na wengi wa wanafunzi ambao hawajalipa...inadhihirisha kuwa engi wao hawana uwezo wa kufanya hivo!!...Nilipoongea na viongozi wa DARUSO yaani viongozi wa serikali ya wanafunzi wakasema kuwa wanajitahidi lakini utawala bado umekataa kuyatoa matokeo hayo.....
Ukweli ni kwamba mitihani ya supplementary imeshafanyika na wasio na matokeo ina maana mitihani imeshawapita na chuo kimeshafunguliwa kwa mwaka mwingine wa masomo......
Habari nyepesi nilizozipata ni kwamba bunge la wanafunzi linakaribia kukaa muda wowote wiki hii na hatujui ni nini wataamua...lakini kama ninavyojua imani ya wanafunzi ni kuwa mgomo utawasaidia....... Sijui itakuwaje na Bunge litaamua nini?
Bado hali ni tete UDSM na wanafunzi wengi hawana amani kabisa na wengine bado wanasita kuhamia chuoni.....Kwa wale wanaoanza mwaka wa kwanza ndio balaa zaidi!!ntawapa situation yao baada ya kufuatilia kidogo....
TABU TABU TABU KUSOMA TANZANIA!!...BALAA BALAAKUWA MASIKINI!!.....POLENI MARAFIKI NA TUNAAMINI BODI ITAWAFIKIRIA NA KUWAPA FEDHA ZENU NA CHUO KITAWAPA MATOKEO.
Wenu,
William aka Bill Jax